Azimio la Arusha: Kwanini shule za Seminari hazikutaifishwa?

Valencia_UPV

JF-Expert Member
Mar 31, 2016
6,223
7,408
Moja ya Nguzo za Azimio la Arusha la mwaka 1967 ni kutaifisha vyanzo vyote vya Uchumi ikiwamo Mabenki, Mashirika ya Bima, Vyuo & Shule binafsi.

Swali ni kwamba kwanini Shule za Seminari hazikutaifishwa?
 
Serikali iliona malengo ya kanisa yanalandana na malengo endelevu ya serikali

kupiga vita maradhi na ujinga, ndo maana hadi leo utakuta madhehebu ya dini yanatoa huduma za afyaa/elimu/ nk

zipo baadhi ya shule zilitaifishwa lakini mwisho wa siku serikali ilishindwa ziendesha na kurejesha mikononi mwa madhehebu ya dini
 
Mleta mada, shule za seminary si vyanzo vya uchumi kwani wazazi hawalipi ada. Sehemu nyingi shule hizi zimeokoa watoto wa masikini, wanajiunga wakisema wana nia ya kusomea upadre, wanapata elimu ya bure mpaka kidato cha sita. Hapa wanaomba mikopo ya elimu ya juu kwenda chuoni.
 
Unajua kwamba Kigonsera ilikuwa ni Seminari? Umewahi kuisikia shule inaitwa Tosamaganga? Umewahi kuisikia shule inaitwa Matola nk? Unajua zilikuwa zinamilikiwa na nani?
Tosamaganga ilikua shule ya waMissionary , ndio Serikali ikaichukua ikawa kama shule yao mpaka leo hii
 
Back
Top Bottom