Azimio la Arusha: Kuzaliwa upya?

Azimio la Arusha: Kuzaliwa upya?

Even if your axiom was true, still the Azimio la Arusha's Ujamaa & Kujitegemea were only practiced (slightly) between 1967 and 1977 so how come the Azimio la Zanzibar's Ubinafsi & Kunyonya have been practiced for more than 10 years and yet we are so fisadily poor?

Ku discredit Azimio la Arusha haina maana nina endorse ufisadi.

Hatuishi kwenye ulimwengu wenye options mbili tu, Azimio la Arusha au fisadi. Wrong!
 
Mkuu nakubaliana na wewe in some part. Kwamba labda kuuliwa kwa Azimio ilikua janja ya wachache. Lakini hata wakati wa ujamaa wenyewe kulikuwa na watu wenye maisha mazuri zaidi ya "common" people. Hata wakati huo kulikuwa na wenyewe uwezo zaidi. Hata siku moja binadamu wote hawawezi kuwa na hali sawa ya kimaisha na hilo ndilo lilikua kusudio kuu la Azimio.
Nami nakubaliana nawe mkuu, na hii inathibitisha kuwa ile kauri ya ujamaa na kujitegemea, watu wote ni sawa... ilikuwa ni geresha tu kwa Makabwela.
 
Ku discredit Azimio la Arusha haina maana nina endorse ufisadi.

Hatuishi kwenye ulimwengu wenye options mbili tu, Azimio la Arusha au fisadi. Wrong!

Kwa hiyo una-endorse Mwongozo?
 
Barua ya Wazi kwa Mheshimiwa Mkapa

Barua ya wazi kwa Mhe. Benjamin William Mkapa, Rais mstaafu

Mheshimiwa Mkapa,
Assalam Alaykum.
Nakuamkia kwa heshima na taadhima. Natumai u mzima wa afya, wewe na familia yako. Nakuombea kila la heri na mapumziko mema, pamoja na majukumu yako mengi na mazito ya kimataifa.

Mheshimiwa, nimeshawishika kuandika barua hii baada ya kusoma kwenye tovuti (http://businessmirror.com.ph/home/opinion/14843-the-sudden-demise-of-neoliberal-economics.html) maoni yako ambayo yamenukuliwa na mwandishi wa habari Roberto Savio akiandika juu ya kifo cha uliberali mamboleo katika gazeti la Business Mirror la 19 Agosti 2009. Umenukuliwa ukisema:

"We privatized everything the state had. Everything was bought by foreign capital because we had no national capital to compete. The foreign companies almost always closed local businesses, which were not competitive, transforming them into distributors of foreign products and driving up unemployment. The experts of the World Bank and the IMF predicted that this would happen, but they told us: Now the influx of foreign investment will lead to the creation of new, competitive and technologically current businesses that will provide the foundations for a lasting, modern development. None of this happened for us."

"Tulibinafsisha kila kitu kilichokuwa mikononi mwa dola. Kila kitu kilinunuliwa na wawekezaji kutoka nje kwa sababu hatukuwa na mtaji wa ndani wenye uwezo wa kushindana. Makampuni ya nje yakafunga mashirika ya ndani kwa sababu hayakuwa na tija na yakayageuza mashirika haya kuwa wachuuzi wa bidhaa kutoka nje na kwa hivyo kuongeza watu wasio na ajira. Wataalam wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa walitabiri kwamba hivyo ndivyo ingekuwa, lakini wakatuambia: Uwekezaji kutoka nje utazaa taasisi za kibiashara za kisasa, zenye uwezo wa kushindana, na teknologia ya kisasa, na kwa hivyo kujenga misingi ya kudumu ya maendeleo ya kisasa. Hakuna lolote kati ya hiyo lililotokea nchini mwetu".

Mzee, unasononeka; kwa kiasi fulani, katika lugha yako ya kidiplomasia, unalalamika. Lakini hata baada ya maanguko ya mfumo wa uliberali mamboleo na utandawazi, ambao uliushabikia sana wakati wa utawala wako, hukuwa na ujasiri wa kuomba msamaha wa watu wako. Sikulaumu. Huwezi kulaumiwa. Ni hulka ya binadamu kutokuona au kukiri kosa lake. ‘Nyani haioni ngokoye.' Katika hili huko peke yako. Katika mkutano wa kundi la nchi 20 (G20) zenye nguvu za kiuchumi ulioitishwa mjini London kuzungumzia hali mbaya ya uchumi mnamo Aprili mwaka huu, Waziri Mkuu wa Uingereza, Bwana Gordon Brown, alikiri kwamba ‘Muafaka wa Washington umekufa', alisema hivyo bila kuwaomba radhi watu wa ulimwengu, hasa wa nchi maskini, ambao waliathirika sana na "muafaka" huo wa nchi za kibeberu ambao nchi zetu zililazimishwa kuufuata.

Mheshimiwa Rais mstaafu: Ukweli ni kwamba haya yaliyotokea sasa si matokeo yaliyokuja kwa bahati mbaya au kwa miujiza tu. Wako viongozi na hasa wasomi (angalau wachache) walisema, tena kwa uchambuzi wa kina na yakinifu, kwamba mfumo huo hautufai, hautatuletea maendeleo, bali utauongeza tu unyonywaji wa watu wetu na uporwaji wa mali zetu. Mwalimu Nyerere alijitahidi sana kupinga masharti ya nchi za kibeberu, lakini hakufanikiwa. Mzee Mwinyi alifungua milango na wewe ukakumbatia, bila kuhoji mfumo huo, hasa masharti yale ya kubinafsisha mashirika ya umma. Ni kweli mashirika mengine hayakuwa na tija, ni kweli pia mengine yalikuwa na menejimenti mbovu. Lakini je, tulijaribu kutafuta njia mbadala, licha ya hiyo ya kubinafsisha ‘kila kitu'? Wasomi wako wachache waliokosoa sera zako za kiuchumi uliwaita majina na kuwafananisha na ‘wavivu wa akili'. Ulipigia sana debe utandawazi kiasi kwamba jina lako litaingia katika historia kama mvumbuzi wa neno ‘utandawazi' katika msamiati wa Kiswahili. Uliwafumbia macho viongozi wako wakati wakitumia vyeo vyao kujilimbikizia mali na utajiri wa kupindukia – au hili pia ilikuwa ni sera ya kujenga mabepari wa ndani?

Mbaya zaidi, mheshimiwa, chini ya uongozi wako tukakubali kutoa uhuru kwa taasisi za kifedha, na kukubali soko huria katika biashara ya fedha, (na kutokudhibiti akaunti ya mtaji (capital account)) bila udhibiti na usimamazi wowote wa dola. Hili ndilo hasa lilikuwa chanzo cha chumi zetu kuathirika kupita kiasi pale anguko la mfumo wa fedha wa kimataifa lilipotokea.

Nchi ambazo zilikataa soko huria katika mambo ya fedha, kama China na Malaysia, hazikuathirika kama nchi zingine. Naomba nisiendelee. Wananchi wetu, pamoja na kutokuwa na usomi au ustaarabu wako au wangu, wanahisi moyoni mwao udhaifu wa mfumo wa utandawazi na binamu yake uliberali mamboleo. Ndio maana wakati wa kuadhimisha miaka kumi tangu kifo cha Mwalimu, wakalilia sana Azimio la Arusha.

Mwalimu hakuwa malaika, alikuwa kiongozi wa kisiasa. Alikuwa na mapungufu yake lakini alijali watu wa chini, watu ambao walisahaulika kabisa katika awamu ya tatu na wanaendelea kupuuzwa katika awamu ya nne. Kila mlalahoi aliyetoa maoni yake alikuwa na maneno haya tu: Mwalimu alitujali; Azimio la Arusha lilitujali sisi wanyonge. Azimio lilitoa matumaini. Uliberali mamboleo na utandawazi ulitoa matumaini yapi kwa matabaka ya chini, zaidi ya kuwa njia ya viongozi kujilimbikizia mali bila aibu!

Mheshemiwa Rais mstaafu, sio nia yangu kurudia yale yaliyotokea. Lakini, utakubaliana nami kwamba historia ni muhimu. Kujifunza kutokana na historia yetu na ya wengine ni hatua ya kwanza katika safari ndefu ya kujikomboa na kujiletea maendeleo halisi. Kama kweli umejifunza na umeyaona madhara ya sera ulizozikumbatia wakati ukiwa madarakani, je, huoni kwamba una wajibu wa kumsaidia mrithi wako, na hasa kutusaidia sisi wananchi, ili tujifunze kutokana na makosa ya serikali yako? Je, kweli, bado unanadi na kutunasihi kwamba utandawazi hauepukiki? Je, bado unatushauri kwamba msukumo wa maendeleo ni uwekezaji kutoka nje, uwekezaji ambao umejidhihirisha wazi ni uporaji wa maliasili yetu? Je, huoni kwamba unao wajibu, kwa upande wako, wa kufanya kila iwezekanayo – na wewe sio mtu mdogo katika nchi hii – kutusaidia kuzindua mjadala wa kitaifa juu ya hatma ya nchi yetu na bara letu?

Wasalaam,

Issa Shivji
Profesa wa Kigoda cha Taaluma cha Mwalimu Nyerere
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Okotoba 24, 2009
 
Who said individualism and competition does not belong in the past? You are talking as if Adam Smith and his invisible hand is our contemporary! The past is always in the present!

P.S. In the context of the global financial crisis can you also say Keynesianism belongs in the past?

Ujamaa, socialism, communism or whatever you may call it has failed. It is a fact that capitalist nations are far advanced than socialist ones. Look at the USSR? It's policies completely failed and they are now embrassing capitalism. Even China right now is opening it's doors to an open market.

The current economic crisis does not mean capitalism has failed. There is no system which has no problems. I am sure you know about the Great Depression in the 1930's. Have you read about the U.S. economy then? Most economies were in a worser state then they are in right now. In Germany a basket full of money was worth way more than the money it was carrying. The economy was in a worser state than it currently is. But that did not mean capitalism failed then and it doesn't mean that capitalism has failed now.

So mkuu if you are in support of socialism in any form maybe you should give us an example of such state which has used it and progressed. As for now I stand by my words, individualism and competion is the way to go.
 
As if that was not enough, the central tenets are self contradictory.

How can "Ujamaa" and "Kujitegemea" be mixed? the two are practically negative and positive, when you mix them they annihilate each other in a big puff, leaving you with zip, zero.

And then you wonder why are we so poor in the midst of abundance?
Why not! marriage and being independent are also positive nad negative, yet for a successful marriage, many prefer marriage partnership qualities while not loosing each other sense of independence.
Tell it to a single person he will never understand!

A country can be independent as a nation with united citizen who makes a strong spirit of resistance by being self-reliance commitment to defeat a common enemy.
 
Ujamaa, socialism, communism or whatever you may call it has failed. It is a fact that capitalist nations are far advanced than socialist ones. Look at the USSR? It's policies completely failed and they are now embrassing capitalism. Even China right now is opening it's doors to an open market.

The current economic crisis does not mean capitalism has failed. There is no system which has no problems. I am sure you know about the Great Depression in the 1930's. Have you read about the U.S. economy then? Most economies were in a worser state then they are in right now. In Germany a basket full of money was worth way more than the money it was carrying. The economy was in a worser state than it currently is. But that did not mean capitalism failed then and it doesn't mean that capitalism has failed now.

So mkuu if you are in support of socialism in any form maybe you should give us an example of such state which has used it and progressed. As for now I stand by my words, individualism and competion is the way to go.

The same argument can be used to prove that Ujamaa has not failed. We were just passing through the flirting phase which Mkapa has admitted above did not yield what we wanted. That was our economic depression.
 
Ndiyo maana mkuu nika kuomba utoe mfano wa a socialis state which has progressed. How can we say we are passing through a "flirting" phase when socialism never worked for us? If you can provide proof of a time when socialism worked for a country in the long run that will improve your argument. If you can also show a time in Tanzania's history where socialism was actually causing us to develop more that would be even better. Toa mifano mkuu.
 
Ndugu ni mara ngapi natoa hizo takwimu humu. Rejea takwimu za Tanzania kabla ya Vita na Nduli. Pia kumbuka Ujamaa sio Ukomunisti wala sio Usoshalisti wa Kimagharibi. Hiyo ni modeli yetu wenyewe ya maendeleo.
 
O.K. ndugu ngoja nitafute hizo takwimu ili tujadiliane vizuri zaidi. Kama una angalau link naomba unisaidie.
 
Mwanafalsafa,
First, Is a social democratic country (left wing) a Socialist?...
 
Mwanafalsafa,
First, Is a social democratic country (left wing) a Socialist?...

From my understanding mkuu, a Social Democracy is different from Socialism. I have a book on that so I will read it again and come give the exact meaning of Social Democracy.
 
Mwanafalsafa,
Kasome kisha nishtue maanake hizi mada hujaa page haraka sana..

Hata hivyo mkuu wangu, kuiga kitu ni uchovu wa akili, kutokuwa na vision na zaidi ya hapo hujui implications zake..Na ndio tofauti kubwa sana ya viongozi..
Ebu msome Mkapa..
"We privatized everything the state had. Everything was bought by foreign capital because we had no national capital to compete. The foreign companies almost always closed local businesses, which were not competitive, transforming them into distributors of foreign products and driving up unemployment. The experts of the World Bank and the IMF predicted that this would happen, but they told us: Now the influx of foreign investment will lead to the creation of new, competitive and technologically current businesses that will provide the foundations for a lasting, modern development. None of this happened for us."

Kisha msome mwalimu:-
Mwalimu said he had read and re-read the document several times after it was set aside and still saw nothing to change, although, he said, if given a second chance, he would have done certain things differently.
 
Zakumi,
Nyerere had several honorary degrees. Hence the title Dr. is appropriate.

Hapa tunachanganya madude. The highest academic degree aliyofikia was equivalent to bachelor.
 
Hebu acha upambe bana na wewe. Ni sisi tu Miafrika tunaopenda kuweka hizo herufi nyuma ya majina yetu hata kama hatustahili. Sidhani kama kwa vile tu wamekupa honorary degree basi na wewe au mifuasi yako i-abuse hiyo degree na kuanza kukuita kama vile unastahili kuitwa hivyo.

Watu hawataki kuumiza vichwa na ndio maana wanalilia Azimio la Arusha na hawataki kutengeneza kitu kipya.
 
Mkuu Mkandara kitabu nitakacho quote ni Keeping the Republic 3rd Edition. Nili kitumia kwenye course yangu ya U.S. Government. Hapo chini ni citation toka page 11 ya hicho kitabu.

Social Democracy
Some countries in western Europe, especially the Scandinavian nations of Norway, Denmark, and Sweden, have developed hybrid systems. As noted in Figure 1.1, these systems represent something of a middle ground between socialism and capitalism systems. Primarily capitalist, in that they believe most property can be privately held, proponents of social democracy nonetheless argue that the values of equality promoted by socialism are attractive and can be brought about by democratic reform rather than revolution. Believing that the economy does not have to be earned by the state, social democratic countries attempt to strike a difficult balance between providing substantive guarantees of fair outcomes and procedural guarantees of fair rules.
 
Mbona hili Azimio la Zanzibar ambalo ndio linatumika sasa hivi katika jumuiya hii ya Wadanganyika na lililozaa ufisadi limekushinda mpaka ukakimbia nchi yako mwenyewe?

Kusingizia kuwa Azimio la Zanzibar kuwa limezaa ufisadi ni kutoona mbali. Kwa bahati nimekaa katika nchi za kisoshalisti baada ya mapinduzi na nilichoona ni high level of corruption baada ya watu kuruhusu kuwa mabepari. Wanahita fungulia mbwa.

Hivyo kubanwa sana kwa watanzania wakati wa Mchonga kumefungulia mbwa. Badala ya watu kujitafutia utajiri kwa kutumia innovation, wanatumia short cuts.

Sheria za nchi zisiwabane watu kufanya vitu halali. Na mkiwabana watafanya mauzauza ya wale watu waliotumia ujana wao uzeeni.
 
Mwanafalsafa,
Kasome kisha nishtue maanake hizi mada hujaa page haraka sana..

Hata hivyo mkuu wangu, kuiga kitu ni uchovu wa akili, kutokuwa na vision na zaidi ya hapo hujui implications zake..Na ndio tofauti kubwa sana ya viongozi..
Ebu msome Mkapa..
“We privatized everything the state had. Everything was bought by foreign capital because we had no national capital to compete. The foreign companies almost always closed local businesses, which were not competitive, transforming them into distributors of foreign products and driving up unemployment. The experts of the World Bank and the IMF predicted that this would happen, but they told us: Now the influx of foreign investment will lead to the creation of new, competitive and technologically current businesses that will provide the foundations for a lasting, modern development. None of this happened for us.”

Kisha msome mwalimu:-
Mwalimu said he had read and re-read the document several times after it was set aside and still saw nothing to change, although, he said, if given a second chance, he would have done certain things differently.

Mkandara:

Kuna kitu kinaitwa creative destruction. Unabomoa kitu kimoja lakini unapata kitu kingine, chenye manufaa sawa au zaidi ya kile ulichobomoa.

Lakini destruction hii haitumiki kwa watu wenye vichwa vibovu. Watanzania hata tungebaki na makampuni yetu bado, matokeo yangekuwa ni yaleyale.

Vilevile mwalimu hakuona upungufu wa Azimio la Arusha kwa sababu alikosa tools za kuonyesha Earth isn't flat.
 
Back
Top Bottom