Azimio la Arusha: Kuzaliwa upya?

Hotuba ya Mzee Mwinyi inaonyesha kuwa walichofanya kule Zanzibar ilikuwa ni kutoa tafsiri mpya ya miiko ya Uongozi ya Azimio la Arusha kulingana na wakti. Ila ninadhani kuwa walikuwa na mtazamo mfupi sana kuamini kuwa wanaweza kutoboa tairi kwa sindano nyembamba sana na bado tairi hilo likabaki na upepo umbali wote wa safari.
 
..hata wakati wa Mwalimu kulikuwa na ukiukwaji mkubwa tu wa maadili ya Uongozi. Hivi mmesahau kashfa ya ndege za ATC na George Hallack?

..Kichuguu amemtaja kiongozi aliyechukua mkopo NSSF kujengea nyumba. Mwalimu naye alichukua mkopo THB kujenga nyumba. Baadaye "akaiuzia" serikali nyumba hiyo na kuendelea kuishi humo. Alipostaafu serikali, akiwa bado mwenyekiti wa CCM, "ikamzawadia" nyumba hiyo!!

..tatizo letu ni kuliangalia azimio kwa kutumia kurunzi la MAADILI ya viongozi. Viongozi wenyewe wako wangapi? Naomba tuliangalie kwa kutumia kurunzi la UZALISHAJI na TIJA ktk uchumi.

..wakati wa Azimio la Arusha mambo yafuatayo yametokea:

1.Tumetaifisha mashamba makubwa bila kuwa na ujuzi wa kuyaendesha. Matokeo yake mazao kama mkonge,chai,pareto yakadorora.

2.Tumeswaga wananchi kupeleka kwenye mapori kuanzisha vijana vya Ujamaa. Matokeo yake wananchi wakapoteza maisha. Zoezi hili ndiyo chanzo cha kuporomoka kwa uzalishaji wa korosho na uchumi wa mikoa ya kusini.

3.Tulidai tunataka kufuta ujinga na umasikini lakini tukajenga mazingira ambayo Ualimu na Ubwana shamba ni taaluma zinazodharauliwa kuliko zote.

4.Mali ya Umma ilikuwa kama mali isiyokuwa na mwenyewe. Tija, Uzalishaji,na taratibu za fedha, havikuzingatiwa kabisa ktk uendeshaji wa mashirika na viwanda.
--Makada wa CCM walikuwa na sauti na maamuzi kuliko Mameneja ktk mashirika na Viwanda.

5.Azimio la Arusha na dhana ya "mali ya umma" imemfanya mfanyakazi wa Tanzania awe mtovu wa nidhamu ya kazi.

6.Chama kilisisitiza kuanzishwa kwa maduka ya ushirika ktk vijiji vya Ujamaa. Wakati huohuo vyama vya Ushirika vilivyoanzishwa kabla ya Uhuru na Azimio vikavunjwa!!

7.Matibabu bure! Elimu bure! Maji bure!
-- are these services really free? serikali inatoa wapi pesa za kutoa huduma zote hizo bure? kwa namna moja ama nyingine wananchi tumekuwa tukilipia huduma hizo. kama serikali ilikopa nje au ndani nani analipa deni hilo?

Tusilaumu tu Azimio la Zanzibar. Uongozi, tabia, na na mienendo yetu ndiyo iliyoporomosha uchumi na zaidi kuandaa mazingira ya azimio la Zanzibar.
 
Actually ninadhani Mwinyi alielezea vizuri kabisa makusudi ya azimio la Zanzibar, na kama alivyosisitiza kwamba lengo la azimio la zanzibar siyo kuliua azimio la arusha bali kuliboresha.

na kama nilivyomuelewa, kwamba hata kama lisingefanyika wakati ule, bado ingekuwepo haja ya kuliboresha azimio la arusha.

ni dhahiri azimio la arusha liliwabana sana viongozi, lilishindwa kuona nafasi ya pili ya kiongozi kuwa mzalishaji badala ya kuwa kiongozi wa kisiasa tu.

Halafu ni dhahiri azimio la arusha lisingeweza kuwa imara katika mfumo tulionao wa vyama vingi,kwa sababu mfumo tulionao ni mfumo wa wanachama, sasa kwa chama kama ccm chenye wanachama wengi iwapo wangeendelea na masharti ya azimio la Arusha, kama vile wanachama na viongozi kutokumiliki nyumba za kupangisha, au kutokuwa na hisa katika makampuni,n.k ni dhahiri kwamba uchumi wa nchi ungeparalyse. kwa sababu kazi ya hawa wanachama ingekuwa ni siasa tuu na wala si uchumi.

Kuwa na kanuni, na kufuata kanuni hizo ni mambo mawili tofauti, kwa wale viongozi wenye kuvunja sheria na miiko ya kazi zao ,huwezi kulilaumu azimio la zanzibar. Azimio la Zanzibar liliweka misingi ya kazi halali ambazo wanachama na viongozi wa
CCM wangeweza kujishugulisha nazo ili "kuexploit" potential yao ya uzalishaji. japo kuna miiko ambayo viongozi wote wanashare lakini kwa mapana zaidi kila nafasi ya kazi ina miiko yake, miiko ya raisi ni tofauti na miiko ya mkuu wa mkoa, miiko ya waziri ni tofauti na miiko ya katibu kata.kwa hiyo Kwa waziri mwenye uwezo wa kutoa Tenda iwapo atafanya makeke na kuipa tenda kampuni ambayo yeye ana hisa. huwezi kulilaumu Azimio la Zanzibar kwa kuruhusu waziri awe na hisa. badala yake wa kulaumiwa ni waziri huyu aliyefanya maamuzi kinyume cha sheria.

Actually Mwinyi alielezea vizuri kabisa makusudio hayo ya azimio la Zanzibar. Huwezi kumzuia mtu kuwa na mishahara miwili wakati ana uwezo wa kuifanyia kazi na kuitolea jasho mishahara hiyo.Nyerere aliliona hilo baadae ndo maana katika kuadhimisha miaka 20 ya Azimio la Arusha alilitolea ufafanuzi
 
Mtu wa Pwani,

Shukrani sana mzee kwa hiyo hotuba Ya mzee Ruksa, ndo maana mimi naikubali sana JF. watu wako makini sana, sijui umeichimbua wapi hii hotuba mzee.

Anyways Tuendelee kukata ishu kwa ari mpya na kasi mpya.
 
JokaKuu, uchambuzi wako ni mzuri.

Hata hivyo, sikubaliani na wewe unapotaka kutushawishi tuache kuliangalia azimio la arusha kwa kutumia Kurunzi la maadili ya viongozi. Nina sababu kadhaa, kwa nini sikubaliani na hoja yako.

Moja, uongozi pamoja na maadili ya uongozi kwa ujumla ni nyenzo muhimu katika uzalishaji. Kwa hivyo, huwezi kutegemea kuwa na uzalishaji imara kama uongozi wako ni dhaifu. Udhaifu wetu mkubwa, pamoja na wataalamu wachache tuliokuwa nao katika kipinde kile, ilikuwa ni kuwapachika wanasiasa wasio na utaalamu katika shughuli za uzalishaji . Hii pointi umeigusia katika post yako.

Mbili, umezungumza kuwa kushuka kwa uzalishaji wa mazao kama ya mkonge, chai na kahawa kumetokana na uongozi dhaifu mara baada ya utaifishaji wa hayo mashamba. Kwa kiasi fulani nakubaliana na wewe.

Kwa kiasi fulani sikubaliani na wewe kwa sababu tunatakiwa kufahamu kuwa kuporomoka kwa uzalishaji wa mazao haya kunatokana vilevile na uzalishaji wa mazao haya duniani kwa ujumla bila kusahau mfumo mzima wa biashara za kimataifa. Bei ya mazao haya imekuwa ikishuka kutoka mwaka hadi mwaka. Kwa mfano, bei ya kahawa ya tanzania inategemea brazili wamezalisha tani ngapi za kahawa kwa mwaka huo. Ugunduzi wa synthetic fibers umepelekea kuparaganyika kwa soko la mkonge!! Kwa hivyo, huwezi kulitupia Azimio la Arusha lawama zote.

Tatu, inawezekana tupo sahihi kusema kuwa azimio la arusha pamoja na miiko ya viongozi ndio imetufikisha hapa tulipo. Pengine swala muhimu la kujiuliza hapa ni moja. Kuna baadhi ya nchi majirani zetu ambazo hazikufuata azimio la arusha lakini unafuu wa maisha yao na yetu sisi watanzania ni mdogo sana. Malawi walikuwa na azimio gani? Rwanda je? Burundi? Uganda?

Kwa sababu hizi nchi tunashabihiana nazo kwa tabia na utamaduni, ninashawishika kusema, inawezekana kumbe tatizo si azimio la arusha!
 
I have read all coments na mwanzisha hoja. Nitajaribu kujibu kwa sentensi moja tu yenye mantiki na maana ya utofauti kati ya AZIMIO LA ARUSHA na Kijiwe cha Zanzibar.Azimio la Arusha LILIWEKA MIIKO NA MAADILI YA KUFUATA KAMA JAMII YA WATANZANIA. Kule Zanzibar Tu adopt 'RUKHSA' Kwa hiyo kimsing there is no single article ya Azimio la Arusha iliyobakia. ''THE ARUSHA DECLARATION IS VERY DEAD COLD AND STILL' Mifano si mnayo jamani LINGEKUWEPO MNGELALAMIKA NA issues za UFISADI? Msekwa alichemka.
 
Mwanamalundi,
maelezo yako ni sahihi. iko miaka tulikuwa tunazalisha kahawa kuliko Brazil. Je, wao wamefanya nini mpaka wakatuzidi?

Nakubaliana na wewe kwamba bei ya kahawa imekuwa ikiyumba. Lakini naamini kabisa kwamba bei ya processed coffee imekuwa ikipanda au iko steady kwa muda mrefu. Did we take advantage of that?

tatizo letu ni kwamba tulikuwa rigid sana ktk kuendesha uchumi wetu. tulitakiwa tuchanganye mambo kidogo--tukaribishe mitaji na watu binafsi on our own terms.

kitendo cha kuwa rigid na kuchelewa kuchukua hatua za lazima ktk kuokoa uchumi wetu ni mambo ambayo namlaumu sana Baba wa Taifa.

ukirudi kwenye mkonge vs senthetic fibres, hivi ni kitu gani kilituzuia kuzalisha mkonge na kuutumia/kuu-process Tanzania?

suala lingine ni BAJETI YETU YA ULINZI. Yuko waziri aliyelalamika kwamba bajeti yetu ya ulinzi ilikuwa kubwa mno. Alishauri kuwa tuelekeze fedha na rasilimali zetu ktk kuanzisha viwanda vingi zaidi. Ushauri huo ulimfanya waziri huyo aitwe adui wa taifa na ujamaa.

Mwana Malundi, hakuna jibu rahisi hapa. Ziko nchi ambazo rushwa imeshamiri lakini zimeendelea kuliko sisi. hilo siyo la msingi hapa. Ushauri wangu ni kwamba tujiangalie sisi wenyewe na tusitafute vijisababu vya kuhalalisha umasikini wetu na uduni wa uchumi wetu.
 
Shukrani nyingi ziwafikie:
Kichuguu kwa kutupatia mjadala huu wenye msisimko na wenye maana kubwa sana nchini mwetu.
Dua - kwa kutuwekea Azimio la Arusha, ili tusiwe tunazungumzia mambo tusiyoyajua. Si nadra kusikia watu wakilibeza Azimio la Arusha, hata kama hawaelewi chimbuko lake na malengo yake yalikuwa ni nini.
Mtu wa Pwani- kwa kutuwekea Azimio la Zanzibar, ambalo binafsi nilikuwa ninalisikia tu lakini sikujua ni mambo yapi yaliyokuwemo katika azimio hilo. Tayari nimelisoma kwa haraka, lakini sijaona 'contradiction' za msingi kati ya Azimio hili na lile la Arusha.

Niliposoma bandiko la Kichuguu, wazo la kwanza lililoniingia akilini lilikuwa ni kwamba labda huyo Mzee Msekwa angepewa nafasi ya kuyatolea maelezo yake tafsiri, ni kwa vipi yeye haoni kusigana kati ya haya maazimio mawili; na pengine bado kuna umhimu wa kumwomba aelezee maoni yake kuhusu jambo hili.
Lakini baada ya kusoma Azimio la Zanzibar, mtizamo wangu ni kuwa matatizo yetu waTanzania ni yale yale. Maazimio yote mawili Arusha na Zanzibar utekelezaji wake ni tofauti kabisa na manuio halisi yaliyotarajiwa.
Labda ninukuu tu kwa mfano:"Chama cha Mapinduzi hakimkatai tajiri aliyepata utajiri wake kwa njia ya halali na kulipa kodi ya serikali analipa. Anayekataliwa na CCM ni yule aliyepata utajiri kwa wizi, kwa rushwa, dhuluma na kwa njia nyingine za haramu."Tunavyojua na kuona mwelekeo ulivyo sasa hivi katika chama hiki, haya ni maneno yasiyoleta maana sana.

Bado ninaiamini misingi ya Azimio la Arusha katika nyakati hizi mpya. Ni misingi ya haki na njia zilizo bora za waTanzania kujiletea maendeleo. Sijaona 'contradiction' mhimu kati ya haya maazimio mawili - Arusha na Zanzibar; ila wapindishaji wa mambo kwa manufaa ya kibinafsi ndio wanaopotosha maana nzima za maazimio haya.

Udhaifu wetu mkubwa ni utekelezaji. Tumekuwa mahodari sana wa kupanga, lakini dhaifu wakubwa kutekeleza.
 
JokaKuu,

Unajua mjomba lazima tuitazame shilingi moja kwa kile kilichohojiwa na sio kutafuta mapungufu ya Azimio la Arusha. hata hivyo ukitazama Azimio la Zanzibar hakuna hata sehemu moja iliyoleta tija ktk mapungufu yote uliyoyataja hapo juu na leo ni miaka mingapi?

Tunakaribia na pengine kuzidi umri wa Azimio la Arusha kisha nchi yetu imezidi kuwa maskini kuliko ilivyokuwa miaka hiyo. Mwinyi mwenyewe kasema mshahara wake wa 2,200 mwaka 1987 uliweza kumtosha na hata aliweza kununua gari la shilingi 13,000 kutokana na akiba alokuwa nayo, na nakumbuka graduate yeyote toka chuo kikuu aliweza pata kazi moja kwa moja kwa mshahara wa kuanzia shilingi 2,020. Nimefanya kazi wizara ya habari makao makuu kwa hiyo nachosema nina hakika nacho.

kwa hiyo tutazame kilichobadilika toka Azimio la Arusha kwenda hili Azimio jipya na faida zake. Nachokiona mimi ni kuwa Azimio la zanzibar lililenga viongozi wetu na mabadiliko yote yametokea ktk nafasi za viongozi, wananchi wametumiwa tu kutunga tungo inayokubalika.

Hilo swala la kujenga nyumba hakuna aliyesema ilikuwa hairuhusiwi kwani wapo viongozi kibao waliojenga nyumba yao wakati wa Nyerere isipokuwa tatizo lilikuwa kupangisha nyumba hiyo.

Hili la Nyerere kukopa na sijui kuiuza ni hadithi tumeisikia muda mrefu sana na sidhani kama ina jambo lolote linalohusiana na hujuma inayotendeka leo kutokana na Azimio la Arusha... ndio maana huwa nawapinga watu wanaosema wakati wa Nyerere biashara hazikuruhusiwa hali mimi nimewahi kuwa na biashara za kusafirisha ndege Ulaya, Nimepeleka kamba na kaa Harare, Majongoo China yaani nilikuwa najishughulisha pamoja na kwamba fedha ya kigeni ilikuwa haitoki.

Maswala ya huduma mjomba labda wewe unaishi marekani lakini hapa canada, nchi za Nordic na zingine zote ambazo leo zipo juu kwa maisha bora zinatoa huduma za elimu na Afya buree!.. fedha zinatoka wapi?.. ni kodi yakoat least wakati ule tulifahamu kodizetu zilikwenda wapi kuliko leo wizara hazina kazi ya ujenzi wa taifa lakini bado matumizi yake ni makubwa sana.

A politician leo hii anatengeneza fedha kuliko daktari ama msomi yeyote yule... Siasa ni ajira kubwa kuliko zote nchini chini ya Azimio la Zanzibar na uzalishaji wake ni Zero.
 
Mojawapo ya interviews ambazo Mwalimu alitoa miezi michache kabla ya kifo chake NI HII HAPA: Of interest, ni jibu lake kufuatia suali hili:

IB: Does the Arusha Declaration still stand up today?

MJN: I still travel around with it. I read it over and over to see what I would change. Maybe I would improve on the Kiswahili that was used but the Declaration is still valid: I would not change a thing. Tanzania had been independent for a short time before we began to see a growing gap between the haves and the have-nots in our country. A privileged group was emerging from the political leaders and bureaucrats who had been poor under colonial rule but were now beginning to use their positions in the Party and the Government to enrich themselves. This kind of development would alienate the leadership from the people. So we articulated a new national objective: we stressed that development is about all our people and not just a small and privileged minority.

The Arusha Declaration was what made Tanzania distinctly Tanzania. We stated what we stood for, we laid down a code of conduct for our leaders and we made an effort to achieve our goals. This was obvious to all, even if we made mistakes - and when one tries anything new and uncharted there are bound to be mistakes.

The Arusha Declaration and our democratic single-party system, together with our national language, Kiswahili, and a highly politicized and disciplined national army, transformed more than 126 different tribes into a cohesive and stable nation.

However, despite this achievement, they say we failed in Tanzania, that we floundered. But did we? We must say no. We can't deny everything we accomplished. There are some of my friends who we did not allow to get rich; now they are getting rich and they say `See, we are getting rich now, so you were wrong'. But what kind of answer is that?

The floundering of socialism has been global. This is what needs an explanation, not just the Tanzanian part of it. George Bernard Shaw, who was an atheist, said, `You cannot say Christianity has failed because it has never been tried.' It is the same with socialism: you cannot say it has failed because it has never been tried.

BTW: Kichuguu pole na majukumu na karibu sana.. kutokana na hili, I'm so interested to get Prof. Shivji kwani naona ni peke yake amebakia na kitabu cha Azimio la Arusha
 
Mwanamalundi,
maelezo yako ni sahihi. iko miaka tulikuwa tunazalisha kahawa kuliko Brazil. Je, wao wamefanya nini mpaka wakatuzidi?

Nakubaliana na wewe kwamba bei ya kahawa imekuwa ikiyumba. Lakini naamini kabisa kwamba bei ya processed coffee imekuwa ikipanda au iko steady kwa muda mrefu. Did we take advantage of that?

tatizo letu ni kwamba tulikuwa rigid sana ktk kuendesha uchumi wetu. tulitakiwa tuchanganye mambo kidogo--tukaribishe mitaji na watu binafsi on our own terms.

kitendo cha kuwa rigid na kuchelewa kuchukua hatua za lazima ktk kuokoa uchumi wetu ni mambo ambayo namlaumu sana Baba wa Taifa.

ukirudi kwenye mkonge vs senthetic fibres, hivi ni kitu gani kilituzuia kuzalisha mkonge na kuutumia/kuu-process Tanzania?

suala lingine ni BAJETI YETU YA ULINZI. Yuko waziri aliyelalamika kwamba bajeti yetu ya ulinzi ilikuwa kubwa mno. Alishauri kuwa tuelekeze fedha na rasilimali zetu ktk kuanzisha viwanda vingi zaidi. Ushauri huo ulimfanya waziri huyo aitwe adui wa taifa na ujamaa.

Mwana Malundi, hakuna jibu rahisi hapa. Ziko nchi ambazo rushwa imeshamiri lakini zimeendelea kuliko sisi. hilo siyo la msingi hapa. Ushauri wangu ni kwamba tujiangalie sisi wenyewe na tusitafute vijisababu vya kuhalalisha umasikini wetu na uduni wa uchumi wetu.

Nimesoma kwa makini hoja zako. Nimegundua kitu kimoja. Wote tunazugumza lugha moja.

"Mwana Malundi, hakuna jibu rahisi hapa. Ziko nchi ambazo rushwa imeshamiri lakini zimeendelea kuliko sisi. hilo siyo la msingi hapa. Ushauri wangu ni kwamba tujiangalie sisi wenyewe na tusitafute vijisababu vya kuhalalisha umasikini wetu na uduni wa uchumi wetu".

Sina pointi za kuongezea hapo Mkuu. Kama tungelikuwa ni waandishi wa vitabu, tofauti zetu zingelikuwa ni kwenye titles but not the substance. Thanks Mkuu.

 
Mwanamalundi, Mkandara,

1. Mimi napenda kuchokoza, na kupanua uwigo wa mijadala. tatizo ninaloliona humu ndani ni wachangiaji wengi kuanzisha mijadala to prove their theories.

2. Suala lingine linalotukwaza watanzania ni kupenda visingizio. kuna kipindi viongozi waligundua msemo "uhaba wa fedha za kigeni." ilikuwa kaazi kweli kweli. au walipoanza kusingizia vita vya kagera kwenye kila tatizo la uchumi.

3. Mijadala mingi sana hapa Jambo Forums imehusu maadili ya viongozi. ningependa tuzame zaidi na kujiuliza mbona wenzetu Kenya wana viongozi wakabila na mafisadi kuliko wetu lakini wamepiga hatua kiuchumi kuliko sisi?

4. Kama tunasingizia vita vya Kagera, mbona Uganda na Msumbiji walipigana vita vya wenyewe kwa wenyewe lakini leo hii kama hawajatuzidi basi tuko nao sawa kimaendeleo?
 
Mwinyi alielezea vizuri kabisa nia na sababu ya kufanya mabadiriko katika azimio la arusha, Tusingeweza kuendelea na azimio la arusha katika mtindo ule, japo azimio la arusha lilihimiza kujitegemea, lakini halikuzingatia kujitegemea kwa mtu binafsi,badala yake lilijenga watu wenye kuitegemea serikali kuwapa maendeleo,kiufupi azimio liliua ubunifu wa mtu binafsi yeye mwenyewe kujiletea maendeleo.

Halafu azimio liliwabana sana viongozi kupita kiasi(sitetei ufisadi wa kileo bali naangalia hali halisi), mathalani kiongozi hakuruhusiwa kuwa na nyumba ya kupangisha,hii ilikuwa too much, sasa kama mtu unazo nyumba mbili kwa nini usipangishe nyingine?
 
LAZIMA TWENDE NA WAKATI

Lazima twende na wakati ina make a lot of sense, lakini talking solution ya yanayojiri sasa tatizo ni respect kwa rule of law, maana Liberia ambako rais wa zamani amekamatwa hawana Azimio La Arusha, ila wana sheria inayofanya kazi, mambo hayo ya maadili na maazimio ya Arsuha, yalikuwa in a way yana-underestimate sheria za jamhuri, ndio mana hatuhitaji maazimio tena wala mwenge, ila tunahitaji heshima kwa sheria za jamhuri!

Nafikiri by now mtakuwa mmesikia yaliyojiri TRA, kuanzia sasa kila mfanyakazi wa TRA anatakiwa kuorodhesha ma;li zake alizonazo, na atakuwa akiorodhesha kila mwaka maongezeko ya mali zake, atakayebainika kuwa analimbikiza mali kinyume na uwezo wake, anafukuzwa kazi na kufikishwa mahakamni, not very convincing lakini at least something!
 
LAZIMA TWENDE NA WAKATI

Lazima twende na wakati ina make a lot of sense, lakini talking solution ya yanayojiri sasa tatizo ni respect kwa rule of law, maana Liberia ambako rais wa zamani amekamatwa hawana Azimio La Arusha, ila wana sheria inayofanya kazi, mambo hayo ya maadili na maazimio ya Arsuha, yalikuwa in a way yana-underestimate sheria za jamhuri, ndio mana hatuhitaji maazimio tena wala mwenge, ila tunahitaji heshima kwa sheria za jamhuri!

Nafikiri by now mtakuwa mmesikia yaliyojiri TRA, kuanzia sasa kila mfanyakazi wa TRA anatakiwa kuorodhesha ma;li zake alizonazo, na atakuwa akiorodhesha kila mwaka maongezeko ya mali zake, atakayebainika kuwa analimbikiza mali kinyume na uwezo wake, anafukuzwa kazi na kufikishwa mahakamni, not very convincing lakini at least something!

si haba hi serikali ya kikwete inajitahidi, ila bado tuongeze speed ili walaji wote wacheuke walivyokula
 
Mpaka Kieleweke:

Asante kwa juhudi zako. Labda Lowassa anatakiwa asome hicho kipande.
 
Heshima mbele wakulu, Kama mlivyosema, tatizo sio maazimio tatizo ni sisi wenyewe especially elites. Now kuna kitu kimoja inabidi tukiweke wazi hapa. Every Human being is inherently selfish and greedy. Hatuwezi kutokomeza rushwa na ufisadi kama hizo juhudi haziendi sambamba na juhudi za kuinua kipato/maisha ya mkulima na mfanyakazi. Ni kweli watu ni mafisadi na wengine wanaendelea kujifunza. Lakini, lazima serikali iwe creative big time. Realistically, huwezi ukamlipa mtu mshahara wa laki moja na utegemee ufanisi kazini/au kutokomeza rushwa. Najua ni complicated na uwezo wa serikali si mkubwa sana. LAKINI UKISEMA TUFUNGE MIKANDA, BASI WOTE TUFUNGE HIYO MIKANDA! and we should get our priorities right-Always. Jiulize, mbunge unamlipa Laki moja na nusu kwa siku ya kikao na marupurupu mengine, member wa bodi CMA au BOT unampa laki tano kama sitting allowance ya masaa mawili, wakati daktari, mwalimu, hakimu unawapa peanut..what do you expect? Unataka waishi vipi? Sisemi kwamba lazima tulingane, haiwezekani, but we should try to appreciate and reward hardwork and productivity!

Poverty does not justify corruption, lakini lets reason as common/average Tanzanian ambaye ana mahitaji kama wewe..he needs to pay medical bills, asomeshe watoto, awe na nyumba/alipe kodi..and on and on....and you pay the folk laki moja na kodi juu!..na jiulize Billions and billions zinazoibwa/maisha ya kifahari ya viongozi wetu....and on and on..kifupi we preach and fight for standards which we cannot honour ourselves.

Kwa hiyo kupigana na ufisadi ni vyema kabisa, but REALITY CHECK ndo hiyo, huwezi kuwadanganya wananchi na hizi sera za kimangimeza kila siku. Maisha ni magumu sana yet we dont get our priorities right, as a result tunapiga gwaride hapa hapa tuliposimama. Kila mtu anataka kuishi and we shoud STRIVE (as leaders and politicians) to promote/grant standards to our people which we would wish us to have. Muulize kiongozi yeyote au wewe member wa JF hapa..ukipewa laki moja inakusaidia vipi? Its a peanut. Lakini unataka mwalimu anayeishi Buguruni/Mbagala Chamazi kwenye nyumba ya kupanga, watoto sita, mke, extended family and on and on..alipwe hiyo.......Get real!

As we have always said, tunahitaji utawala wa sheria, ambapo kila raia (wakulima kwa viongozi) wako responsible kwa matendo yao. Otherwise we MIGHT WIN THE BATTLE BUT LOSE THE WAR!
 
Hata mimi sina tatizo na mzee Mwinyi.

Tatizo ni lilelile la umaskini wa kupita kiasi ambapo mtu anakusudia kutumia madaraka kujinufaisha.

Azimio la Arusha linaweza kuendelea kutumiwa kwa kuhakikisha kila rasilimali ya taifa inatumiwa kwa uadilifu na matunda yake yanagawiwa kwa kila mwananchi badala ya wale wachache.

Tukiangalia mfano wa wenzetu China wamefanikiwa.

Wao wametumia misingi ileile ya kijamaa lakini hapohapo wameruhusu mabepari kuingia nchini humo na kuleta maendeleo ya ajabu kabisa tofauti na nchi zingine ambazo ziliiga sera za mwenyekiti Mao Zedong na zimetumbukia katika umaskini wa milele.

Mapinduzi ya China ya 1949 hayakuja bure na ndio yaliyounda China ya kisasa ya leo. Yalikuwa na lengo lilelile la kuondoa wafanya biashara uchawara au "bourgeois" ambao walikuwa waliwanyonya wachina wenzao.

Nchini China kila mtu bila kujali ana madaraka alipanda basi kwenda kazini,shule na katika shughuli zingine na pia kila duka liliuza vitu kwa bei moja na kila mtu alijiona yuko sawa na mwingine.

Kwa hio kwa namna moja au ingine chama tawala kilifanyiwa mabadiliko makubwa "purification" ili kuleta "order" nzuri ya China yenye neema.

Kwa hio CCM ilitakiwa ibadilishe baadhi ya ilani zake za uchaguzi pamoja na kukubali kuifanyia mabadiliko katiba, ili kutoa nafasi zaidi kwa sheria kufanza kazi zake ipasavyo na kudhibiti UFISADI.

Vinginevo JF itakuwa inaendelea kuwa kioo cha wanachama popote pale walipo na kusaidia kufanza kazi hio.
 
Nafikiri by now mtakuwa mmesikia yaliyojiri TRA, kuanzia sasa kila mfanyakazi wa TRA anatakiwa kuorodhesha ma;li zake alizonazo, na atakuwa akiorodhesha kila mwaka maongezeko ya mali zake, atakayebainika kuwa analimbikiza mali kinyume na uwezo wake, anafukuzwa kazi na kufikishwa mahakamni, not very convincing lakini at least something!


Why TRA peke yao? Mawaziri je, Makatibu je? Hii lazima uwaguse wote wenye dhamana ya kuwatumikia Watanzania ambao wanapata mianya katika kazi zao za kujitunisha mifuko.
 
Taabu kubwa Tz ni sheria zetu tu- haziapply kwa wote equally!

Ukiiba na kupora through BoT (EPA) 30 Billion Tshs utapeta na utahonga hakimu hata mahakama kuu na utaachiwa! Ila Ole wako uibe kuku- yaani utafungwa tu- ni lazima!
 
Back
Top Bottom