Jethro:
Kuna vitu vingine vinatakiwa kwenye moyo na sio lazima kuandikwa kwenye vitabu.
Wahehe walipokuwa wanapigana na wajerumani hawakujua kusoma wala kuandika. Hawakuwa na Azimio lolote la Arusha, lakini they knew what they were fighting for. You can't put a good fight, if you are unmotivated.
Lekanjobe Kubinika,
Mkuu Azimio la Arusha haliwezi kurudishwa kama Azimio la Arusha.. hii ndio taabu ya kuwaelezea watu wanaofuata cook book..Tunachosema sisi ni mawazo ya mwongozo yaliyomo ndani ya Azimio hilo yarudishwe ili kuondoa hilo la pili, la kwanza haliwezekani kwani Azimio sii Mungu aliyeweza kumrudishia Yesu uhai..
Tukiweza kurudisha miiko na maadili ya viongozi basi bila shaka litakuwa fagio la chuma.
Waberoya,
Mkuu wangu unaposema Wahehe hawakuwa na Azimio wakati hawakusoma mlitegemea kitu gani tofauti? Hivi ktk fikra zenu Wahehe wangeweza vipi kuandika Azimio lao wakati hawakuwa na elimu hiyo..Jamani msianze kuchekesha hapa.
Wahehe walikuwa na Azimio lao na sii lazima liandikwe mahala popote, kama vile sheria, ama hata Costitution walikuwa navyo pasipo maandishi na walifahamu utawala bora, haki za binadamu na amani pasipo UN..
Sasa mkinambia leo tuache kuandika sheria zetu, kwa sababu huoni umuhimu ikiwa Wahehe hawakuwa na maandishi hayo nitakueleweni..
Wakuu zangu, hakuna ubishi hapa ni kueleweshana tu..Sisi tunacholilia Azimio la Arusha ni kutokana na ufedhuli unaotokana na kutokuwepo mwongozo. Yesu alikuja na hata kuandikwa Biblia (mwongozo) ni kutokana na utovu wetu binadamu ktk ibada ya kumwabudu Mungu.. haijalishi kabisa kwamba wakati wa Yesu hawakuwa na Biblia ama ukimwambia mtu asome Biblia basi tunarudi karne ya tatu. na zaiodi ya hapo hakuna mtu anayetaka kujipima imani yake na Yesu, Moses wala Muhammad isipokuwa tunachokitazama hapa ni watu waliokuwa na mwongozo, leo hii Tanzania hatuna mwongozo, ni Taifa linalokwenda kwa kudra za Mungu kama tunavyosubiri mvua za masika. Sheria zinatungwa kufuata upepo na jua..
Mkuu wangu sisi tutaweza vipi kurudisha Azimio ikiwa watu muhimu kama nyie mnapinga pasipo sababu kama tulivyo wadanganyika. Nimekuwa maisha yangu yote sijawahi kuona Wadanganyika wote wakakubaliana kwa jambo lolote, hata kuandama kwa mwezi ni mashauri!
Vijana wengi wa Tanzania wamepitia kwenye shule za kukaa chini, na kwa miaka zaidi ya 20 sasa haijafanya watanzania wavumbua madawati na vitu vingine vya kuwasaidia.
Zakumi,
Hakuna innovation yoyote ikiwa kitu hicho Hakihitajiiki..Kiuchumi ktk udogo wa mahitaji wanasema kama hakuna demand hakuna Supply hivyo Production inakatwa na innovation haihitajiki...Kwa nchi hizo zilizoendelea wanasema - west of time and money!
Neccessity is the mother of invention mkuu wangu hakuna hadithi nyingine na wamesema hao hao walioendelea.
Mkandara:
Here you might argue that necessities stimulated the innovation of alternative and efficient tools, lakini ukiangalia matatizo ya nchi kama Tanzania, idadi ya watu na resources zinazowazunguka, ungetegemea watanzania kufanya ugunduzi. Mpaka sasa uvumbuzi wowote haujatokea na bila kutumia misaada ya watu wengine, watu wengi wako tayari kurudi katika maisha yao ya zamani.
Nimesahau kuna mpakistan mmoja huwa ananitania, ikiwa leo first world countries wataweka ndege za bure aiport DSM na kusema wanaotaka kwenda Ulaya wapande ndege bure, for sure (wewe shahidi) kuwa watanzania watataka hata kusimama kwenye ndege ili waende ughaibuni!
Ikiwa una taifa la watu wasio na uzalendo, wanaowaza kujiendeleza kibinafsi, kwenda na kupotelea nje ya nchi, Ikiwa una taifa la watu waliochoka na nchi yao wenyewe! WAKIO TAYARI KUIBA MAFUTA YA TANESCO ili watu wakose umeme1
Taifa hili lina hitaji kwanza MOYO WA KIZALENDO, WATU WAPANDIKIZWE MOYO WA KIZALENDO, MOYO WA KULIPENDA TAIFA, ROHO NA MOYO WA KIZALENDO UKIINGIA, BASI TUTAWAZA NA KUTEKELEZA MAAZIMIO, HII NDIO ASSIGNMENT KUBWA ZA VIONGOZI WETU KULIKO CHOCHOTE KILE, taifa lisilo na wazalendo limekufa!
please let us be honesty, hilo azimio ili kureinforce maazimio lazima sheria zinatumika, thats why Laws na utekelezaji wake are far better than maazimio katika nchi kama yetu.
Mbaya zaidi wezi na mafisadi wa nchi hii ni WAZEE WALIOKARIRI AZIMIO LA ARUSHA NA KANUNI ZA TANU!
Waberoya:
Nilitaka kuanzisha thread ya kuuliza Spirit ya Taifa la Tanzania. Labda Companero na Mkandarea watanisaidia.
Ukiwa hapa Marekani na kutokana na jinsi ya nchi ilivyoundwa, watu wanakuwa na confidence ya kufanya vitu hata ambavyo haviwezekani. Ukiwauliza, watasema hiyo ni spirit yao.
Kwa mfano: Bill Gates, vijana wa facebook, Napster etc, walipopata ideas za kutengeneza pesa, walikuwa tayari kuachia shule na ku-implement ideas zao. Ukiwauliza watakwambia hiyo ni spirit ya taifa lao.
Zakumi,
Mkuu wangu tunabishana kitu gani ikiwa mwenyewe umeshasema, necessities stimulated the innovation of alternative and efficient tools.
Hili sii swala la kubishana ila ndio imani nilokuwa nayo..Ebu fikiria vitu vinavyotengenezwa na chuma kama vingeweza tengenezwa na MAWE...Sidhani!
Hatuna Spirit. Roho ya nchi au jamii yeyote, alinena Mwalimu Nyerere kwenye Hotuba yake ya Kwanza kwa Bunge la Jamhuri ya Tanganyika mnamo 1962, ni utamaduni wake. Sasa sisi hatuna utamaduni/roho na wewe ni miongoni mwa watu mnaoona kuwa kujenga utamaduni wetu hakuna maana ila mkialikwa kwenye Thanksgiving huko US mnaenda kula minyama ya Bata Mzinga kumbe hamjui wenzenu ndio wanajenga hivyo hiyo Spirit inayowafanya wawe Wavumbuzi! Azimio la Arusha lilijaribu kujenga Roho ya Taifa ila kama yule Kikaragosi wa Sinema ya Wizard of Oz mkalitupilia mbali huko Zanzibar ili mle kwa uroho wa kifisadi rasilimali zetu bila kuwa na Roho ya Kizalendo!
Kwa kukufahamisha zaidi kuhusiana na Necessities, ni sawa na sisi bninadamu tunavyokuwa, na dunia nayo inakuwa... Mtoto anapozaliwa huhitaji maziwa tu, na jinsi anavyokua ndivyo mahitaji ya chakula kingine yanavyopanda hivyo necessty ndio ina stimulate uvumbuzi wa vyakula vigumu na nyenye nutrition..mavazi vile vile..
Na usije changanya uwezo wa mtu au binadamu na innovation hata kidogo, nakumbuka utotoni mwangu sikuvaa viatu kabisa hadi nikiwa mkubwa wa darsa la saba na wala haikuwa noma, kifupi kwa waafrika wengi wetu (maskini) viatu havikuwa neccessity pamoja na kwamba tayari vilikwisha vumbuliwa.
Lakini nimekuja gundua kwamba baada ya wao kuvumbua viatu sijui karne ya ngapi hakuna tena uvumbuzi wa kitu kingine zaidi ya viatu ikiwa kweli properity inaleta invention... Na kama itatokea sijui lini, basi ujue kuna mahitaji ya vazi hilo!