Azimio la Arusha: Kuzaliwa upya?

Azimio la Arusha: Kuzaliwa upya?

Huwa sihitaji hata kulisikia hili jina la huyo jamaa. Umasikini huu tulionao yeye ni anasehemu kubwa ya mchango wake.

Mfumuko wa bei kauleta yeye, EPA na chorus zake za DOWANS, RICHMOND, Meremeta, IPTL, Kuuza mashirika yote aliyo yaanzisha, Kagoda nk nk, vyote kafanya yeye? Wakati anaondoka madarakani dola ilikuwa chini ya jero, leo ni ngapi? Aliacha viwanda vingi na nyumba nyingi chini ya serikali, leo viko wapi? Kama ulipotoshwa na mafisadi wakati unasoma elimu ya Mungai-umepotea ndugu.
 
“Kwa kuwa serikali ya nchi inawajibika kwa wananchi, basi, endapo serikali hii itahujumu maslahi ya pamoja, itakuwa ni haki ya wananchi kuyapinga maamuzi ya serikali au kuivunja serikali hiyo na kusimika serikali mpya, serikali ambayo itawajibika kuzingatia masharti yote, kama ambavyo yatawekwa na wananchi kwa ajili ya kukuza na kuhami maslahi yao ya pamoja.”

Mbona naona kama alikuwa amewatega viongozi woooote watakaofuatia baada yake?
Hivi tukijifanya kwamba Azimio la Arusha Bado lipo, na ndio linalotuongoza, hali itakuwaje Jamani?
Nadhani DR SLAA naye alirefer hapa (Kumbuka mahojiano yake na MM)

Hii kitu iko kwenye karibia katiba zote ulimwenguni. Na hata kama isingekuwepo, huu ukweli bado ungetamalaki.

Nguvu ya watawala inatokana na watawaliwa. Hii ni kweli iwe ni utawala wa kifalme, kikomunisti, kibepari, kiimla, kijeshi, kikoloni haijalishi. Zamani za kale watawala walijaribu kuleta dhana ya nguvu inatokana na jeshi, na wakaenda mpaka kuwatenga wanajeshi na wananchi ili wasiingiliane - wakawaweka kwenye makambi na kuwatungia sheria zao pekee (martial laws). Haikusaidia. Mfano mzuri kabisa ni Wafaransa wallivyomuondoa madarakani Mfalme Louis
 
Kumbuka Waziri Mkuu hayati Sokoine!! Alikuwa tofauti na Dr. Slaa? Dr. Slaa na Mwl. Nyerere wangeiva pamoja. Wote waadilifu.
wewe unafikiri ingekuwa wakati wa mzee kifimbo watu kama slaa wangepona, nyie mchezeeni kikwete tu. wewe unadhani kuna mtu mwingine angeweza kutamka haya maneno zaidi ya yeye nyerere?
 
J.nyerere alisema "ILI NCHI IENDELEE INAHITAJI VITU VI NNE, 1. ARDHI 2. WATU 3. SIASA SAFI 4. UONGOZI BORA. TZ HATUNA UONGOZI BORA NA WATU MAKINI
 
Risasi za moto zimejaa tele vituo vya Polisi, na Askari wetu wamepewa Haki ya Kuua Raia wakati wowote...
Cha Muhimu tuanze kutoa elimu ya Uraia kwa Askari wetu, kila mwana-JF ambaye ana ndugu au Jirani ambaye ni Askari ampe Darasa juu ya Umuhimu wa Raia kudai haki zao kwa njia ya maandamano. Kisha tuwaeleze juu ya Umuhimu wa wao kulinda Raia badala ya kuwafyatulia risasi kwa kufuata maagizo ya wakubwa,, Kisha tuendelee........
nakushauri uache uropokaji maana ukubwa sio umri tu bali na busara zinahitajika, imagine wewe ni askari "kwanza ulishawahi kushuhudia varangati la wakurya wakiwa na rungu?" bunduki yako cha mtoto ukizembea ukapewa moja ya nguvu tunakupa jina jipya. so askari wa tz tuseme wamekua machizi ukiwambia ua wanaua? no! kuna vitu hebu tuchunguzeni kabla ya kuaanza matusi
 
Yule Mzee alikuwa na vision ya mbali sana. Hotuba zake nyingi ukizisikiliza bado ziko relevant hata leo hii miaka 26 tangu angàtuke madarakani. Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi...AMEN

Hakuwa na vision! Hakuna vision kwenye hii statement bali ni ukweli wa hali ya uongozi! Nyerere amesoma tu jamani. Hata wewe ukisoma utaweza kutoa maneno kama haya. Kwa mfano mtu aliyesoma kuhusu Russian Revolution atajua tu juu ya maradhi ya serikali iliyojizidishia nguvu. Kama kweli alikuwa na vision kwa nini hakuruhusu vyama vingi toka zamani? Sasa ivi tunakula mazao ya Nyerere, penda usipende!!
 
Nabii hakosekani kutambulika isipokua nyumbani kwake.

Nyerere ndi kiongozi pekee ambaye mpaka sasa hivi ameitendea nchi hii mambo makubwa.
1.Elimu ilikua bure kuanzia shule za msingi hadi chuo kikuu.Alitaka watz wasome ili waje kuikomboa nchi hii.Kama baba yako na babu yako walikataa shule kwa ajili ya kwenda kuoa hayo ni matatizo yao.Afya nayo ilikua bure.Unaenda hospitali unachukua dawa hadi za akiba mpaka zilikua wengine zina expire nyumbani.

2.aliweza kujenga nyumba nyingi za watumishi wa umma ili kurahisisha utendaji wao wa kazi,kuwa motivate na kuwa punguzia ukali wa maisha.

3.hakuwa mbinafsi..Angetaka angefanya kama kina Mobut

4.Alijenga viwanda kwa lengo la kuongeza uzalishaji,na ndio maana currency yetu ilikua strong.

5.Alijenga umoja wa Kitaifa .ndio maana unaweza kuishi popote nchi bila tatizo.

6.Alikua ni mtu mwenye hekima ya hali ya juu,ndio maana hata deposit yetu ya madini aliiacha ili ije kusaidia na wengine pale wote tutakapokua tumekwenda shule ,tufanye maamuzi sahihi.

7.Alikua na msimamo,kwa lile alilotaka kulisimamia.

9.alikua ni mtu alie ipenda nchi hii kwa moyo.

10.Alijitahidi kufanya kazi kwa moyo wake wote.

11.Alijitahidi kujenga miundo mbinu mbalimbali--Barabara za wakati ule kuna baadhi ya mikoa hadi leo bado zipo,lakini za sikuhizi zinadumu muda gani?Hospitali,vyuo.

Hizo ni miongoni mwa sifa chache tu zinazonifanye nione kuwa mtu huyu alikua muaminifu.

Mimi ninachowaomba wana JF tuangalie kwa pamoja,miaka aliyokaa mwalimu kiuongozi na hiii tuliyonayo sasa ipi kazi kubwa imefanyika?Ni vitu gani vpya tumefanya?Hospitali na vyuo ni zilezile,watu wa extend tu...
Mwalimu alitumia fedha kidogo output ikawa kubwa,na hiyo ndio ingefanya tufike mbali,lakini saa hizi pesa nyingi zinatumika,maendeleo kidogo.

kwa hiyo wale wanaomsema mwalimu vibaya nafikiri wana matatizo.
Tatizo linalo tutafuna sisi ni maadili,kwa kila tunalolifanya.Umasikini wako wewe uangalie,kama hautokani na 1.kukimbia shule,2.Uvivu 3.Kutokujituma kwa lile unalolifanya(seriousness) sasa yote hayo tulitaka mwalimu atufanyie?

Mambo yote hapo juu mwalimu alitupa bure,leo hii tunayalipia!sasa hilo ni kosa la mwalimu?

Naomba nisiwachoshelakini mtu huyu ni wakukumbukwa daima.kwa wale ambao baba zao aliwapiga kibuti wakamchukia ni bahati mbaya kwao lakini mwl ni kiongozi bora kutokea.sasa tunaelekea kumpata kiongozi mbovu kupata kutokea.
 
Sababu za kumlaani nyerere:
(1) nyerere alisema kama angekuwa na uwezo angevizamisha visiwa vya zanzibar kwenye bahari ya hindi.

(2) nyerere alisaidia kupinduliwa dola yetu ya zanzibar halaf akalazimisha muungano hewa. Kumbuka kauli ya karume kuwa muungano ni kama koti likikubana unalivua.

(3) azimio la arusha la nyerere lilikuja kutaifisha mali za waislam tanganyika na zanziba. Kumbuka karume aliposema kuwa, azimio la arusha mwisho chumbe.

(4) nyerere alivunja jumuiya za kiislam tanganyika na east africa. Kumbuka kuvunjika kwa (EAMWS)-East african muslim walfare society. Sambamba na kuanzisha BAKWATA.

(5) nyerere aliwadhalilisha wazee wa kitanganyika ktk bomoa bomoa yake ya vijiji vya ujamaa.

(6) nyerere amewanyima watanganyika elimu hadi leo hii watanganyika hawana elimu na hivyo basi wamekosa akili wamekaa kama kondoo waliopotea.

(7) nyerere ndie alie simika mfumo kristo tanzania

(8) nyerere aliwatia njaa watanganyika na kuwalisha sembe njano bovu, sambamba na road blocks kila mkoa zinazozuia vyakula kuja dsm.
Huyo ndie laanatullah nyerere ambae kwa maaskofu ni mtakatifu.

(9).... Zinaendelea...
 
(1) Alitumia neno angevisukumia mbali sio kuzamisha na hiyo haikutokana na chuki bali ilikuwa ni suala la usalama zaidi.

(2)Hili sina ushahidi nalo lakini maandiko mengi yanaeleza waliohusika ni wazanzibar wenyewe chini ya Karume kwa kumtumia Okello na Muungano sidhan kama ulilazimishwa maana hakuna jeshi ambalo lilienda Zanzibar na kumkamata Karume aje DSM kusaini hati za muungano.

(3)Dhamira ya azimio la Arusha ilikuwa ni kukata mirija ya wanyonyaji, halikuundwa kwa kuwalenga waislam peke yao hivyo kama walikuwa wanyonyaji hapakuwa na jinsi.

(4)Lakini BAKWATA iliendelea kuwa ya waislam na ipo hadi leo na waislam wapo nchini na kuna wengine wanamheshimu sana Mwalimu hata alipoachia madaraka alimwachia mwislam aongoze nchi hiyo ni kuonyesha hakuwa na uadui na uislam pamoja na waislam wenyewe.

(5)Ukisikia serikali kuchukua maamuzi magumu ndo kama hivyo, lengo lake lilikuwa ni zuri labda utekelezaji ulifanywa kwa haraka, hata hivyo wananchi kuishi kwenye vijiji kulikuwa na faida kuliko kuishi mbalimbali mashambani, lengo lilikuwa ni kuwapatia huduma za jamii kwa urahisi, watu wakiwa vijijini ni rahisi kuwa na shule, ni rahisi kuchimba visima vya maji hata kutengeneza barabara ambayo itapitiwa na watu wengi na kusafirisha mizigo mingi ni rahisi, kuwajengea zahanati ni rahisi.

(6)Pamoja na chuki yote uliyonayo dhidi yake kuhusu elimu ungempa credit, toka aondoke madarakani hao unaowapenda wamejenga chuo gani kiwe kikuu, cha ualimu, cha tiba zaidi ya hiki cha Dodoma.

Pamoja na kwamba hapakuwa na vyanzo vingi vya mapato, watu walisoma bure.

(7)Kama alisimika mfumo kristo ilikuwaje akataifisha shule za wakiristo ili watu wote wasome waislam, wakristo na wasiokuwa wa dini hizo mbili, Bado madaraka alimwachia mwislam na katika kipindi chake sidhan kama kuna msikiti hata mmoja ulivunjwa ili kujenga kanisa, na sidhan kama kuna waislam walibatizwa kwa nguvu.

(8)Mkuu, kama nchi haikuwa na chakula ilikuwaje tena chakula kilikuwa kinatoka mikoani, labda kuna kitu sijaelewa, Mimi ninachojua ni kwamba nchi haikuwa na njaa na mahindi ya njano yalikuwa yanatoka nje, hata mtu kuwaletea chakula wakati hamna chakula ni kosa jamani.

Tayari kulikuwa na njaa na ni kazi ya serikali kuwalinda wananchi wake na ulinzi ni pamoja na hatari itokanayo na majanga kama njaa.
 
Imekuwa sasa ni mazoea ya watu katika kada mbalimbali kuzungumzia kuwa ni heri azimio la Arusha lirudishwe na wengi wakibeza azimio la zanzibar kuwa lilileta ufisadi wengi wamekuwa wakitaka sana azimio hilo lirudishwe wakiamini kuwa ndilo suluhisho la matatizo yanayoendelea hapa nchini lla hasha hii si sawa kabisa kwakuwa sasa tuko katika kipindi tofauti sana na wakati ule kiuchumi,kisiasa na kiutamaduni kuna mabadiliko mengi yametokea yanayopelekea ugumu wa utekelezaji wa azimio la Arusha kwakuwa hakuna tena ujamaa hapa nchini sasa tuko katika uchumi wa kibepari unaomilikiwa na wachache.

Unafiki uliopo ni huu hakuna mtanzania atakayekuwa tayari kuachia mali zake zimilikiwe na wote hebu wewe hapo niambie una kijumba chako ulichojenga na umepangisha je uko tayari nyumba ichukuliwe na kumilikiwa na watu wote na kodi itumike kwa maslahi ya watu wote!!! la hasha hapana hakuna hata mmoja atakaye thubutu kukubali hili sasa huu ndo unafiki wenyewe tena wengi watabeza kuwa heee ebooo kwani tulijenga wote!!! na hapa ndipo wote wanaotetea azimio la arusha lirudi watakuwa wanafiki wakubwa kwakuwa haiwezekani mkatamani kitu mnachokibeza.

Aimio la arusha liliasisiwa na kujengwa katika misingi ya ujamaa je nani hapa nchini mjamaa kila mtu bepari sasa acheni unafiki ,,nchi yetu isonge mbele katika sera za ubepari na kuachana na fikra za azimio la arusha!
 
je ni nani alikuwa waziri mkuu wakati huo
je ni nani alikuwa ni waziri wa elimu wakati azimio la arusha
 
Kila nikikaa na kupitia azimio la arusha sijaona kosa lake karibu kila kitu ambayo tunashabikia imeandikwa mle.

Sera yetu ilikuwa ya ujamaa na kujitegemea . Nchi hii ni ya wakulima na wafanya kazi. maana neno hii ni kwamba watu wengi ni wakulima na wafanyakazi. Idadi kubwa ya watu wetu ni wakulima wakifuatiwa na wafanyakazi. Hao ndio wenye nchi.

UJAMAA: Ufafanuzi wa neno hili uko hivi uchumi wa taifa ni kwa faida ya watanzania wote. Maana yake ni kwamba kama tunajenga uchumi wetu uwafae watanzania wote. Msimamo huo ukaitwa UJAMAA. Hiyo faida ya wote ndio ikazaa neno UJAMAA. Je uchumi wa tanzania kwa sasa hivi ni kwa faida ya nani? Ebu tusaidiane hapa wajameni uchumi huu unajengwa kwa faida nani kama si ya watanzania wote?

KUJITEGEMEA Tuangalie maana ya neno kujitegemea. Hii ina maana moja tu kwamba kama kweli tunataka kuendelea
ni tujitegemee hakuna njia ya mkato ya kuendelea isipokuwa ni kwa sera ya kujitegemea tu. Huo ndio msingi wa Azimio la arusha . Je leo suala la kujitegemea bado haisitzwi? mbona kila kona watu inawauma kusikia bajeti tegemezi. Sasa kama ndio iko hivyo kwa nini tuliua AZIMIO la Arusha? wakati ilitoa miongozo mingi sana DIRA YA TAIFA, NAMNA YA KUPATA VIONGOZI, MAADILI YA VIONGOZI, MAADILI YA TAIFA, SERA YA UCHUMI NA MISINGI YA UTU.

Naomba tujadili kwa umakini wote suala hili na tutoe solution. kwa upande wangu AZIMIO la Arusha irudishwe.
 
AZIMIO la ARUSHA........... Liliruhusu JOB AVAILABILITY kwa pia kushirikisha Mashirika yanayomilikiwa na Serikali kuajiri

AZIMIO la ZANZIBAR..........Liliruhusu LABOR AVAILABILITY hence - cheap labor higher PROFIT MARGIN
 
Kosa kubwa la Azimio la Arusha ilikuwa ni kuwakatia mirija Mabepari wa Ulaya. Sasa hivi wamerudi kwa kasi tena wakisaidiwa na MAKUWADI ambao ni miongoni mwa Viongozi walioko madarakani... Fun facts; Wote waliosoma Harvad University walitekwa na kutumiwa kama Economic hit Men! Mfano mzuri ni Fisadi Andrew Chenge, Ballali, Ndullu, Rostam...wengine ni BWM, Prof Muhongo, Dr Kafumu, Nyalandu, Apson, Mboma, Mgonja et al...
 
mimi ninachotaka mkuu ni kukirudisha ili tuwe na dira kwa sababu taswira ya taifa ni mbaya sana hakuna hata moja tunaweza kujivunia mambo mazuri tuliyojaribu yameachwa na hatujui tuendako kiukweli kabisa. je unaweza kueleza sera ya taifa letu je ni taifa la ujamaa au ya ubepari. watu wengi hasa wenye nchi hawajui nchi yao inafuata sera ipi?
 
Mkuu maganjwa,

sera inayofuatwa kwa sasa ni sera ya Uchuuzi mdogo mdogo. wananchi wanaambiwa waunde vikundi ili wapewe mitaji ya kuuza karanga, bamia, kucheza ngoma nk. Viongozi nao wanashindana kuingia mikataba mingi itakayo wapatia vijicent vya kuweka Uswis...

Ni vigumu sana kuirjesha Azimio la Arusha kwa wakati huu; Sera zenye kukinzana tayari tumesha letewa na bunge letu kubariki! Njia kuu za uchumi kumilikiwa na Umma ilifutwa, njia kuu za uchumi zinamilikiwa na akina BWM et al...Tanzania imesha ridhia mikataba feki ya kibiasha za kimataifa, itakuwa vigumu sana kufuta mikataba kama ya dhahabu, uranium, gesi, almasi et al...

Kama nchi tutakachoweza kufanya ni kuweka uwazi katika mikataba na utekelezaji wa bajeti mwanzo mwisho... zaidi ya yote ni kuweka kwenye katiba kuwa adhabu ya Ufisadi ni Kifo na kitekelezwe kwa mtu yeyote hata Rais wa nchi kama walivyofanya Wachina...mwisho na kwa umuhimu: kunahaja ya kureview vipaumbele vyetu ili viwalenge walengwa ambao ni wananchi badala ya kuendelea kuwavutia wanyonyaji...

...Nina matumaini makubwa kuwa hii mikataba ya Wachina inayoingiwa sasa hivi itatusaidia sana kuwabana mataifa ya kimagharibi ambayo huwa wana homola Rasilimali zetu in the name of Jesus na kuwaacha wananchi hoi in the name of shetani...
 
Mkuu Maganjwa, sera inayofuatwa kwa sasa ni sera ya Uchuuzi mdogo mdogo. wananchi wanaambiwa waunde vikundi ili wapewe mitaji ya kuuza karanga, bamia, kucheza ngoma nk. Viongozi nao wanashindana kuingia mikataba mingi itakayo wapatia vijicent vya kuweka Uswis...
Ni vigumu sana kuirjesha Azimio la Arusha kwa wakati huu; Sera zenye kukinzana tayari tumesha letewa na bunge letu kubariki! Njia kuu za uchumi kumilikiwa na Umma ilifutwa, njia kuu za uchumi zinamilikiwa na akina BWM et al...Tanzania imesha ridhia mikataba feki ya kibiasha za kimataifa, itakuwa vigumu sana kufuta mikataba kama ya dhahabu, uranium, gesi, almasi et al...
Kama nchi tutakachoweza kufanya ni kuweka uwazi katika mikataba na utekelezaji wa bajeti mwanzo mwisho... zaidi ya yote ni kuweka kwenye katiba kuwa adhabu ya Ufisadi ni Kifo na kitekelezwe kwa mtu yeyote hata Rais wa nchi kama walivyofanya Wachina...mwisho na kwa umuhimu: kunahaja ya kureview vipaumbele vyetu ili viwalenge walengwa ambao ni wananchi badala ya kuendelea kuwavutia wanyonyaji...
...Nina matumaini makubwa kuwa hii mikataba ya Wachina inayoingiwa sasa hivi itatusaidia sana kuwabana mataifa ya kimagharibi ambayo huwa wana homola Rasilimali zetu in the name of Jesus na kuwaacha wananchi hoi in the name of shetani...

Bwana nimekuelewa ila uchuuzi mdogo mdogo hautupeleki popote na zaidi wala usiseme mikataba hii ya kimataifa haiwezekani kubomolewa ishu ni sera ya yetu inasemaje kwa kuwa hatuwezi kunyonwa eti kisa mikataba ya kimataifa kama ndio hivyo tutataka kuwauliza je unyonyaji wa rasilimali zetu uwe halali wao walindwe kwa sababu ya mikataba mibovu isiyo na faida kwetu. Hiyo haifai hata univeral law of human right ambazo wameziunda wao haziruhusu.

Lingine bwana Ilboru mikataba sio amri ya mungu leo duniani kote Hugo sharves anasifika kwa kuwasaidia watu wake baada kuvunja mikataba mibovu ya hao wanaojiita wa kimataifa watu wa venezuela wakapata ahueni ya maisha Ebu tujaribu kufikirisha BONGO zetu hakuna kisichowezekana chini ya jua turudi kwenye missingi ya iliyojenga nchi yetu.
 
Kama kambarage aliacha mshahara na akawa anakula zawadi anazopewa wao wanashindwa nini. Kama kinjekitile alinyongwa baada ya kugoma kumeza maneno yake wao wanaogopa nini. Kama Mkwawa alijiua kuliko kujitoa kwa wajeuriman wao wanaogopa nini. Wakati wa kuandika historia ni sasa, Je wewe ni nguruwe tukufichie lulu zetu? Wewe ni farisayo, je wewe ni Sadukayo? Je wewe ni mwalimu wa sheria. Je wewe ni mtoza ushuru? Je wewe ni wa kambarage mbatizaG. Je wewe ni petro?. Je wewe ni Yuda eskarioti. piga uwa garagaza ufalme ni wangu na ikulu ni yangu na kizazi changu. hata ikibidi wote mfe kidogo. ukitaka kuokoa nafsi yako dhidi yangu utaingamiza na ukitaka kuiangamiza nafsi yako kwa ajili yangu utaiokoa. power to u ->Fufuka au Kufa mazima
 
tuungane shime watanzania AZIMIO la arusha ndio jibu letu

Je, hayo yatoka kwako kwa dhati kabisa? Pasi na kufungwa na kushinikizwa na chochote, je ndio imani yako hiyo? Je, kwa dhati kabisa u radhi kusimamia uaminicho? Kama ndivyo, UBARIKIWE Mkuu wangu maganjwa. Huu ni wakati sasa wa wenye Fikra moja kuungana na kutenda, hata kama kuna kanafasi kadogo aje, acha tukacheze kiukamilifu maana huo ndio WAJIBU wetu kwa imani na jamii yetu! Ni wakati muafaka wa kuweka Fikra zetu katika vitendo. IMETOSHA kulalama buree! NO MORE POLITICS! Na TUSIMAME LEO. Nguvu yetu ni Umoja na Kuthubutu! TUNAWEZA. Mimi ni muumini!
Mungu wetu yu hai, tayari kutushindia vitani. Anaita sasa!
 
Last edited by a moderator:
Lirudishwe kama lilivyo KATIKA SURA NA WAKATI TULIONAO ...HAITAKUWA VIBAYA KULIITA AZIMIO JIPYA LA ARUSHA.

TUNALIPENDA! TUNALITAKA! TUNALIAMINI! Lirudi upya "Azimio Jipya la Arusha". Lakini hakuna mwingine wa kulirudisha, bali ni 'mimi'. Ni wewe ukijisemea nafsi yako! Ni SISI! Si wengine, ni waumini wake, SISI! Swala si lirudi ama lisirudi, bali TUNALIRUDISHAJE? Mimi na wewe katika umoja wetu, tukae chini tuunganishe FIKRA zetu, tutegue na kutega hesabu zetu, kulifanya tena hai. MANENO YAMETOSHA ni WAKATI wa KUTENDA SASA!
Nguvu yetu ni 'Umoja na Kuthubutu' TUNAWEZA. Mungu wetu yu tayari kutupigania. Anaita sasa!
 
Back
Top Bottom