Watu8
Platinum Member
- Feb 19, 2010
- 77,240
- 111,261
Ni mmoja wa ma-legendary wachache sana kwenye tasnia ya utangazaji east Africa.
Hili nafahamu mkuu...
Lakini pia watu yawapasa wajue kuwa pamoja na umahiri wa Charles usio na shaka kuja Azam ni muendelezo tu wa yeye kusaka malisho mazuri...
Watu wanavyoshadadia utadhani kilichofanyika ni usajili wa klabu ya mpira kumleta mchezaji star wa dunia...
Hapa hakuna hata mmoja mwenye uhakika kati ya Charles na Azam nani alikuwa wa kwanza kumuomba mwenzake...
Kama suala ni uzalendo huenda anayepaswa kupongezwa hapa ni Charles kwa kukacha ajira yake ya BBC na kuamua kuja kuijenga Azam na hatimaye tasnia ya habari ya Tanzania...