AZAM TV na Bodi ya Ligi mnatuibia pesa watazamaji wa ligi kupitia king’amuzi chenu

Complicator

JF-Expert Member
Aug 23, 2013
2,198
3,566
Naandika kwa masikitiko makubwa sana baada ya kugundua kwamba miezi miwili sasa imepita bila kuwa na mwendekezo mzuri wa kuonyesha mechi za ligi kuu ya nbc,ndani ya mwezi unaangalia game mbili au tatu halafu unatakiwa kulipia tena.

Kwa mfano weekend hii iliyoisha kulikua na shida gani mpaka kusiwe na mechi za ligi? Hakuna timu iliyokuwa na mashindano ya kimataifa, weekend imeisha.

Napata mashaka ratiba inapangwa kimkakati ili kuwanufaisha hawa Azam.
 
Shida ipo CAF,,kuna ratiba ya mashindano ya CHAN,, lakini haijapangwa mpaka leo.
 
Azam media ndiye anayepanga ratiba nzima ya Ligi kuu na bodi ya ligi ni kivuli hawana wanachopanga na hata wao hawapendi hili suala la wikiendi kutokuchezwa kwa ligi kuu.
 
Nadhani Bodi ya Ligi na TFF wanahusika moja kwa moja na huu ubabaishaji, ukilinganisha na hao Azam Media.
 
Ukiangalia fixtures mfano timu inacheza tarehe 04.10.2023 then inakuja kucheza Tena trh 22.10.2023 na inacheza game 3 ndani ya siku 6 Sasa huo Kama sio upumbavu ni Nini? Kwanini wakae wiki 3 bila kucheza then uje kumjazia mamichezo mengi ndani ya mda mfupi? Mpira wa bongo ili ukuwe Kuna mijitu inabidi itoke kwenye mpira
 
Back
Top Bottom