AZAM TV Mmepoteza haki ya kuonyesha Bundesliga?

Shakir

JF-Expert Member
Jul 31, 2012
1,602
1,819
Kwema Wakuu?

Leo tarehe 27/01/2024 kulikua na mechi kadhaa za ligi ya Ujerumani maarufu kama Bundesliga.

Sasa AZAM TV ambao hua wanaonyeshaga live hizi mechi leo hawajaonyesha hata mechi moja. Hakukua na maelezo yoyote yale kabla kuhusu kutoonyesha mechi hizi.

Kama mtu amelipia package fulani akijua hizi mechi zipo zinaonyeshwa na mwishowe asionyeshwe basi ni kumkosea mteja huyu na Serikali kupitia mamlaka husika wanapaswa kuchukua hatua.

Ni Wizi kumchaji mtu kitu ambacho hakipati. Ingekua mechi moja imekosekana sawa, lakini kukosekana mechi zote za leo sio sawa hili kupita kimya kimya.

Screenshot_20240127-221055.jpg
 
Back
Top Bottom