0ozg Tz
JF-Expert Member
- Feb 28, 2016
- 4,159
- 11,100
Kwa jinsi hali ilivyo sasa ya kimpira hapa kwetu, hasa katika mazingira ya vibanda umiza, kwa kuangalia mashabiki wa hizi timu mbili kubwa hapa Bongo.
SIMBA
Kwa msimu huu wa 2021/22 hasa siku za hivi karibuni, mashabiki wa Simba wameanza kupungua kuhudhuria mechi za Simba, hasa hasa inapokuwa inacheza michezo ya Ligi Kuu na hata kutoa kiingilio wanakuwa wagumu.
Majibu yao ni kuwa "leo sina" au anatoa hela pungufu, wakati misimu mingine iliyopita mashabiki wa simba walikuwa wanafurika kwenye vibanda kwa idadi kubwa sana. kwa kila mechi haijalishi ni za kimataifa au za hapa nyumbani na walikuwa hawana usumbufu wa kutoa kiingilio.
YANGA
Kwa msimu huu wa 2021/22 mashabiki wa yanga wamekuwa wakitoa pesa ya kiingilio bila kuwa na usumbufu wowote.
Yanga ina mashabiki wavumilivu sana hata misimu ambayo walikuwa hawafanyi vizuri bado waliendelea kuhudhuria kwa wingi sana, ila kwa misimu ambayo Yanga walikuwa wanafanya vibaya mashabiki wake walikuwa wasumbufu kutoa kiingilio ingawaje walikuwa wanahudhuria wengi sana kwa kila mechi ambayo Yanga inacheza.
MASHABIKI WA JINSI YA "KE"
Takwimu zinaonesha Yanga wana mashabiki wengi zaidi ya mashabiki wa Simba,yaani mashabiki wa Yanga wa jinsi ya ke wapo 70% na simba 30% ya wanawake wote TZ.
LIGI ZA ULAYA
Toka Azam TV ianze kuonesha Ligi ya tz,imepelekea kupunguza mashabiki wa ligi za Ulaya.
Hii inapelekea kutumia faida tuliyoipata kwa kuonesha ligi ya TZ kulipia ving'amuzi vinavyoonesha ligi za ulaya,tunafanya hivi kutokana na kuwa sisi wamiliki ni wapenzi wa ligi hizi za ulaya lakini isingekuwa hivyo tusingekuwa tunalipia ving'amuzi vya Ulaya.
Niliwahi kuhisi labda zile bechi ambazo haziruhusu watu kuegema ndo zinasababisha watu wasipende kuangalia mechi za Ulaya maana wanakuwa wameshachoka baada ya mechi ya simba au yanga kuisha.
Niliamua kutafuta viti vya kuegama lakini bado watu walikuwa hawakai baada ya mechi ya simba na yanga kuisha.