Azam tv huu sasa ni utapeli

Cyo siri hata Mimi Azam imenibore sana,15,000/= nilikuwa angalau napata channel za movie (action) na mpira (local league) lakini hivi sasa nimelipia 18,000/= naangalia mpira tu channel zote za movie wamepeleka 22,000/= .Nilitegemea Azam ndiyo itakuwa kimbilio letu sisi wa kipato cha chini lakini sivyo,natamani hata kuvunja dish lao,mchina na TBC wangekuwa vizuri na star times yao ningeludi huko.
Tajiri hajawahi kua rafiki na Mnyonge tangu dunia iumbwe.
 
Nililipia King'amuzi cha Azam tarehe 19/8/2017 kwa kifurushi cha 15000 kwa stakabadhi 10854272 , Tarehe 29/8/2017 nilitaka kujua ninasalio LA pesa kiasi gani katika Account yangu . Ikawa ni na balance ya 6000 na nilipouliza kama ninaweza ku-TopUp ilikupata kifurushi jibu Likawa ni NDIYO Hivyo tarehe 29/8/2017nililipa 10,000/ambayo ikichanganywa na 6000/ ya awali nikawa nimelipia miezi 2 , Ajab Azam hawataki kutambua mwezi was pili japo kuwa pesa wamechukua kwa stakabadhi no 11082595 na ya 29/8/2017 na 10854272 ya 19/8/2017 Lakini KABLA YA MUDA MATANGAZO KWANGU YALIKATWA TAREHE 19/10/2017 KINYUME NA PESA MLIOCHUKUA AZAM TV NINI MAANA YA JAMBO HILI
 
Pole mkuu..sio fair walivyokufanyia lakini...Wapigie simu au nenda ofisini kwao ukawaelezee tatizo lako
 
Tukihama watashusha tu, ujinga wao hawatapata wa kumfanyia, hali ilivyongumu unapandisha gharama hovyohovyo unategemea nn? Afu hivi tcra hawaangalii mambo haya, inakuaje vingamzi vinajipandishia tu gharama vitakavyo, kwa nn isiwepo bei elekezi?
 
Sijui kwa nini waliwaondoa TV 1 kwenye king'amuzi chao?
Walitangaza kuwa makataba na Tv1, ulikwisha na Tv1 walitaka dau zaidi, azam walikataa hilo dau zaidi, kumbuka kuwa biashara ni kushindana, kwese ya Zimbabwe wanahisa kubwa kwenye Tv1, kumbuka kuwa KWESE Wanaouza visimbuzi vyao, kwa hiyo ndiyo mambo ya biashara hayo.
 
Kwa mtanzania ambaye unahitaji kununua Dish kwaajili ya kuangalia vipindi vya TV nakushauri usije kununua hii kitu inaitwa AZAM TV usije ukaingia kwenye Majuto ni Mjukuu maana hawa jamaa ni wezi tu kwanza Channel zao hazina vipindi vya maana zaidi ya Highlight za VPL yaani ni bora kama unataka kuangalia mpira uende vibanda umiza halafu bei zao yaani niza kitapeli tapeli tu kuanzia Dish zao huku kwetu ni 160000 wakati Dish zingine ni kuanzia 80000 kushuka chini njoo kwenye vifurushi AZAM wanaanza na 15000 wakati wengine kuondoa DSTV wao wanaanza na 8000 ukiwa na AZAM wewe utakuwa mtu wa kujutia tu usishangae baada ya wk2 utaambiwa kulipia kila channel mmoja kwa 3000 inamaana kuwa kuanzia AZAM ONE,AZAM TWO,SINEMA ZETU,AZAM SPORT HD,AZAM SPORTS 2 Utalipia 15000 ukisema uongeze ITV,EATV, nk itakubidi ulipie zaidi ya 30000 per mwezi kwanza kama ntapata mteja nauza hili DISH kwa bei ya kutupwa
Niachie Dish nihangaike nalo mkuu.
 
Nakuunga mkono mleta uzi, mie nimewahama. Njoo TING kuna mambo mazuri huku. Waliondoa Tv1 nikajua wanatuletea channel nyingine ya kutuonyesha EPL badala yake walidharai wateja wao na kutuongezea gharama tu
 
Walitangaza kuwa makataba na Tv1, ulikwisha na Tv1 walitaka dau zaidi, azam walikataa hilo dau zaidi, kumbuka kuwa biashara ni kushindana, kwese ya Zimbabwe wanahisa kubwa kwenye Tv1, kumbuka kuwa KWESE Wanaouza visimbuzi vyao, kwa hiyo ndiyo mambo ya biashara hayo.
Kwese siyo ya zimbabwe mkuu,Kwese kwao ni South Africa na Zimbabwe ni alipozaliwa Mmiliki japo kwa sasa anaishi Uingereza.
 
Mi nimteja wa hichi kinga'muzi lakin hivi karibun kumekuwa na kupanda kwa gharama zisizo endana na huduma wameongeza sh 3,000 kwa kifurushi cha chini kabisa kilichokuwa 15,000 na sasa ni 18,000 na kama utalipa 15,000 hutapata chanel za michezo...wameongeza chanel moja ya kichezo azam sport2 ambayo nilikuwa nina matumain tutaona hata miachuano ya UEFA au europa hata ligi zingina kama germany au italy lakin hiyo chanel ndio hamna kitu hata highlits za EPL hamna wanaonesha ligi yetu ya ndondo tu...lingine ni kuweka gharama za kulipia clouds plus ili kuona fiesta kwanza chanel yenyewe ina scratch halafu hiyo fiesta ina uzito gani kiasi cha kulipiwa 3,000 nagopa kesho watasema tulipie 2,000 kuona taarifa ya habari..!!.ujanja ujana mwingi chanel nyingi mnazifungia zinapatikana for free kwenye ma dish ya satelite ya makubwa.!
Piga chini ving'amuzi funga kebo mkuu. Hao wengi no matapeli tu kaka
 
fe0a8b0d25fc428990960401882bdf49.jpg
Nipo huku
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom