Azam tv huu sasa ni utapeli

Azam tv huu sasa ni utapeli

Half Genious

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2017
Posts
491
Reaction score
786
Mi nimteja wa hichi kinga'muzi lakin hivi karibun kumekuwa na kupanda kwa gharama zisizo endana na huduma wameongeza sh 3,000 kwa kifurushi cha chini kabisa kilichokuwa 15,000 na sasa ni 18,000 na kama utalipa 15,000 hutapata chanel za michezo...wameongeza chanel moja ya kichezo azam sport2 ambayo nilikuwa nina matumain tutaona hata miachuano ya UEFA au europa hata ligi zingina kama germany au italy lakin hiyo chanel ndio hamna kitu hata highlits za EPL hamna wanaonesha ligi yetu ya ndondo tu...lingine ni kuweka gharama za kulipia clouds plus ili kuona fiesta kwanza chanel yenyewe ina scratch halafu hiyo fiesta ina uzito gani kiasi cha kulipiwa 3,000 nagopa kesho watasema tulipie 2,000 kuona taarifa ya habari..!!.ujanja ujana mwingi chanel nyingi mnazifungia zinapatikana for free kwenye ma dish ya satelite ya makubwa.!
 
Cyo siri hata Mimi Azam imenibore sana,15,000/= nilikuwa angalau napata channel za movie (action) na mpira (local league) lakini hivi sasa nimelipia 18,000/= naangalia mpira tu channel zote za movie wamepeleka 22,000/= .Nilitegemea Azam ndiyo itakuwa kimbilio letu sisi wa kipato cha chini lakini sivyo,natamani hata kuvunja dish lao,mchina na TBC wangekuwa vizuri na star times yao ningeludi huko.
 
Kwakweli hii ni njia mpya ya kuchukua pesa za watu. Tunakoelekea Dstv watakuwa na nafuu kuliko Azam TV,ni suala la muda tu. Wameanza kuingiza udalali wa kulipia channel 1,zitafuata na nyingine au kulipia vipindi
 
AZAM kwakweli sasa wanakera mimi niko mkoani nimelipia hiyo 15000 lakini hakuna chaneli yeyote waliyoongeza,nikaongeza sh3000 kama matangazo yao yanavyosema lakini hakuna channeli waliyonifungulia,nika bonyeza *150*50*5# na kubadili kama wanavyotangaza wakanitumia sms kuwa nimefanikiwa kubadili kifurushi lakni kwenye tv yangu bado vilevile.kwakweli wanajeuri sasa.
 
Azam wanabid wajiangalie sana udalali wa kulipa chanel moja moja ambazo hazina jipya inakera zaid
 
Kwa mtanzania ambaye unahitaji kununua Dish kwaajili ya kuangalia vipindi vya TV nakushauri usije kununua hii kitu inaitwa AZAM TV usije ukaingia kwenye Majuto ni Mjukuu maana hawa jamaa ni wezi tu kwanza Channel zao hazina vipindi vya maana zaidi ya Highlight za VPL yaani ni bora kama unataka kuangalia mpira uende vibanda umiza halafu bei zao yaani niza kitapeli tapeli tu kuanzia Dish zao huku kwetu ni 160000 wakati Dish zingine ni kuanzia 80000 kushuka chini njoo kwenye vifurushi AZAM wanaanza na 15000 wakati wengine kuondoa DSTV wao wanaanza na 8000 ukiwa na AZAM wewe utakuwa mtu wa kujutia tu usishangae baada ya wk2 utaambiwa kulipia kila channel mmoja kwa 3000 inamaana kuwa kuanzia AZAM ONE,AZAM TWO,SINEMA ZETU,AZAM SPORT HD,AZAM SPORTS 2 Utalipia 15000 ukisema uongeze ITV,EATV, nk itakubidi ulipie zaidi ya 30000 per mwezi kwanza kama ntapata mteja nauza hili DISH kwa bei ya kutupwa
 
Mimi nakula channel zao zote bure sijui wamenifanya barozi bila kujua maana naelekea mwez wa tano now silipii
 
Kwa mtanzania ambaye unahitaji kununua Dish kwaajili ya kuangalia vipindi vya TV nakushauri usije kununua hii kitu inaitwa AZAM TV usije ukaingia kwenye Majuto ni Mjukuu maana hawa jamaa ni wezi tu kwanza Channel zao hazina vipindi vya maana zaidi ya Highlight za VPL yaani ni bora kama unataka kuangalia mpira uende vibanda umiza halafu bei zao yaani niza kitapeli tapeli tu kuanzia Dish zao huku kwetu ni 160000 wakati Dish zingine ni kuanzia 80000 kushuka chini njoo kwenye vifurushi AZAM wanaanza na 15000 wakati wengine kuondoa DSTV wao wanaanza na 8000 ukiwa na AZAM wewe utakuwa mtu wa kujutia tu usishangae baada ya wk2 utaambiwa kulipia kila channel mmoja kwa 3000 inamaana kuwa kuanzia AZAM ONE,AZAM TWO,SINEMA ZETU,AZAM SPORT HD,AZAM SPORTS 2 Utalipia 15000 ukisema uongeze ITV,EATV, nk itakubidi ulipie zaidi ya 30000 per mwezi kwanza kama ntapata mteja nauza hili DISH kwa bei ya kutupwa
Dstv,Azam tv na startimes
Waliobaki wanasuasua tu.
 
Marketing wao hana akili yeye lifikiria Fiesta kila mtu atataka kuangalia kwanza kuangalia vipindi vya Clouds ni kuumiza macho tu vipindi kama njingle haieleweki ni vipindi au tangazo upuuzi mtupu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom