KINGSLEE
JF-Expert Member
- Aug 30, 2013
- 842
- 1,064
Kwanza niwe muwazI ninawakubali sana hawa jamaa Channel zao nyingi ni HD compared na vingamuzi vingine ukitoa Dstv.
Ishu ipo hivii:-
Azam TV wametangaza punguzo la bei kwenye vifurushi vyake ambavyo ni Azam Lite kutoka 10,000 hadi 8,000, Azam Pure kutoka 18,000 hadi 13,000 na Azam Plus kutoka 23,000 hadi 20,000.
Mabadiliko hayo yanaambatana na mabadiliko ya channel katika kila kifurushi.
Kifurushi cha Azam Lite kilichokuwa Tsh 10,000 na kupunguzwa hadi Tsh 8,000 kitakuwa hakina channel za Azam one na Azam two, ina maana ili uzipate hizi, utalipa 13,000 (Azam Pure), huku Azam Lite utapata Sinema Zetu! Hapa ni sawa na kupandisha gharama kwa Tsh 3,000.
Kifurushi cha Azam Pure kimeshushwa kutoka 18,000 hadi 13,000, hiki ni kifurushi kilichokuwa na Azam Sports na Azam Sports HD zinazoonyesha Soka ikiwemo VPL. Sasa channel hizi zitahamia Azam Plus iliyotoka 23,000 hadi 20,000. Kwa kuwa walipaji wa hiki kifurushi ni wapenzi wa michezo hasa mpira, ina maana wameongezewa gharama kutoka 18,000, hadi 20,000.
Hapa idara ya masoko na mauzo itakuwa inaamini Watanzania ni wajinga kiasi hiki? Kwa nini wasiseme ukweli kwamba wameongeza gharama badala ya kudanganya kwamba wamepunguza?