Aweso na Serikali kiujumla wanawaonea watendaji wa Mambo ya maji, watafute root cause sio kufukuza tu

ubarinolutu

JF-Expert Member
Oct 22, 2012
1,964
3,895
Nadhani wataalamu wetu waliosomea fani ya maji na walioajiriwa katika mamlaka ya maji wanapitia wakati mgumu Sana na nadhani wanajuta kwanini walisomea taaluma hizo hasa wahandisi.

Muda uliopita nimeona Aweso ameamrisha watumishi wa maji sengerema 6 wakamatwe na wakawekwe ndani kwasababu wananchi wamekosa maji na wanaopata shida, juzi MH Rais amesema anafanya mabadiliko makubwa kwa mainjinia wa maji. Tatizo hatujiulizi kwanini wahandisi karibu wote waonekane kushindwa kazi, yaani wote hao no wazembe, Rais labda amepewa taarifa za uchonganishi kuwa wahandisi ndo tatizo na japokuwa sifahamu Wala sijui hao watu wa maji na mainjinia wao wanafanyaje kazi lakini naamini Kuna tatizo zaidi ya watu au watendaji ambao kila siku wanalaumiwa.

Lazma tatizo na chanzo Cha matatizo ya maji kijulikane kiini ni Nini , hii biashara ya kuwalaumu watendaje Aweso atafeli kabisa, na ameshafeli, alipaswa aunde timu ijue na ichunguze Nini kiini Cha matatizo haya. Hata Kama utapata mainjinia wazuri kutoka mmarekani watafeli Kama watatumia namna inavyokwenda.

Acheni kuwaonea watendaji wa maji, mnawabully mno, haiwezekani wote waonekane hawafai, Mambo yataendelea kuwa mabaya tu,
 
Kweli.
Pamoja na baadhi ya wakandarasi wanaonewa mfano kuwaondoa contractors wote wawali wa mradi mkubwa wa SAME MWANGA KOROGWE (SMK) kwa wakati mmoja.
Toka December 2020 hadi sasa hakauna kinachiendelea kuwafikishia wananchi wa Same, MWANGA na Korogwe.
Kwa tumbuatumbua hiyo kwa kila aliye simama mbele yake ni wazi wizara iko kwenye mkwamo mkubwa.
Soon anakutana na Go slow ya technocrats na hapo ndiyo mwisho.
Tunasubiri maji HEDARU toka bwawa la nyumba ya Mungu.

Sent from my LG-F800S using JamiiForums mobile app
 
Kwa sie watu ' malaymen' ambao kwa njia moja au nyingine tumebahatika kufanya kazi hizi za miradi, unakuta sio fair kulaumu uzembe wa miradi bila kuangalia kwa undani tatizo hasa linatokana na nini... manake tatizo laweza kuwa ni kwa mkandarasi mbovu( either alichaguliwa kwa upendeleo bila kukidhi vigezo), au upande wa Client kuwa na usimamizi mbovu (ukihusisha malipo kususua kwa mkandarasi na ucheleweshwaji) hivyo kuathiri utendaji wa Contractor na pia msimamizi kutokuwa na timu yenye uwezo madhubuti na makini wa kusimamia kazi yenyewe.....kwa haya mambo hayahitaji mihemko ni bora umakini kutumika, ili kutatua tatizo..
 
Nadhani wataalamu wetu waliosomea fani ya maji na walioajiriwa katika mamlaka ya maji wanapitia wakati mgumu Sana na nadhani wanajuta kwanini walisomea taaluma hizo hasa wahandisi.

Muda uliopita nimeona Aweso ameamrisha watumishi wa maji sengerema 6 wakamatwe na wakawekwe ndani kwasababu wananchi wamekosa maji na wanaopata shida, juzi MH Rais amesema anafanya mabadiliko makubwa kwa mainjinia wa maji. Tatizo hatujiulizi kwanini wahandisi karibu wote waonekane kushindwa kazi, yaani wote hao no wazembe, Rais labda amepewa taarifa za uchonganishi kuwa wahandisi ndo tatizo na japokuwa sifahamu Wala sijui hao watu wa maji na mainjinia wao wanafanyaje kazi lakini naamini Kuna tatizo zaidi ya watu au watendaji ambao kila siku wanalaumiwa.

Lazma tatizo na chanzo Cha matatizo ya maji kijulikane kiini ni Nini , hii biashara ya kuwalaumu watendaje Aweso atafeli kabisa, na ameshafeli, alipaswa aunde timu ijue na ichunguze Nini kiini Cha matatizo haya. Hata Kama utapata mainjinia wazuri kutoka mmarekani watafeli Kama watatumia namna inavyokwenda.

Acheni kuwaonea watendaji wa maji, mnawabully mno, haiwezekani wote waonekane hawafai, Mambo yataendelea kuwa mabaya tu,Ni kwe
Ni kweli uchunguzi wa kina ni lazima ufanyike ili kuleta tija inayostahili. BUT sometimes huwa kuna uzembe wa hali ya juu, kutokujali na business as usual kwa baadhi ya Network Engineers.
 
Back
Top Bottom