Aweso aingiza mitambo Dar, aelekeza visima vya dharura kuchimbwa

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
666
835
Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso Leo tarehe amefika ofisi za RUWASA sehemu ya uchimbaji visima na ujenzi wa mabwawa (DDCA) na kutoa maelekezo mahususi kwa Taasisi hiyo kwa kushirikiana na Bonde la Wami/Ruvu kuainisha maeneo yenye uwezekano wa kupata maji chini ya ardhi na visima vya dharura vichimbwe haraka katika kupunguza changamoto ya Maji.

Mhe Aweso ameagiza Visima vilivyochimbwa miaka ya nyuma 197 vifukuliwe na kukaguliwa/kuboreshwa viweze kutumika kwa kipindi hiki.

Aweso ameitaka DAWASA kuvikarabati Visima vya dharula vilivyochimbwa miaka ya nyuma pamoja na visima vitakavyochimbwa na DDCA baada ya kuanishwa na Wami/Ruvu kuviunganisha kwenye mfumo wa Usambazaji wa Maji wa Dar es salaam kwa ajili ya kuongeza kiasi cha Maji.

Mhe. Waziri Juma Aweso amekagua na kuagiza Mashine mpya za kuchimbia Visima kuanza kutumika kwa dharura hata wakati ratiba ya uzinduzi rasmi nchi mzima na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiendelea kupangwa.

Waziri Aweso ameelekeza matumizi ya dharura ya Mitambo mipya na ile iliokuwepo na kuzitaka Taasisi za Wizara ya maji kufanya kazi kwa ushirikiano kuleta suluhusho la haraka la upatikanaji wa Maji Kwa wakazi wa Dar es salaam.

Awali Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa alitembelea visima vikubwa vya maji mengi Kigamboni na kuruhusu rasmi maji lita milioni 70 kuongeza hali ya uzalishaji Maji maeneo ya katikati ya Jiji la Dar es Salaam na Kigamboni.

 
Aweso amefeli.

No research no right to say.

Hayo maji huko chini ameyaona wapi? Visima vimekauka.

He's there for his benefits
 
ulikuwa wapi Mh Waziri kusubiri ukame ndio uanze kuzima moto? kuna vitu vinachekesha sana.

Hatuna plans kwenye kutatua matatizo yetu baadala yake tunakimbikimbia tu kila tupatapo shida.
 
Hamkuwahi kuwa serious kuwekeza kwenye sekta ya maji, acheni mbwembwe......ndo maana nchi hii mifugo inakunywa maji pamoja na binadamu na watu kule vijijini bado wanakunywa maji ya kwenye madimbwi ambayo yana rangi ya tope.
 
visima vikubwa vya maji mengi Kigamboni na kuruhusu rasmi maji lita milioni 70 kuongeza hali ya uzalishaji Maji maeneo ya katikati ya Jiji la Dar es Salaam na Kigamboni.

13.01.2022
Mradi wa Maji Kigamboni utakamilika Aprili 2022, na tunategemea kuanza kazi ya ulazaji wa mabomba ya usambazaji maji kwa wananchi mapema wiki ijayo" Mhandisi Cyprian Luhemeja, Afisa Mtendaji Mkuu -DAWASA



MSUMBA ON JANUARY 15, 2022
Ujenzi wa tanki lenye ujazo wa lita milioni 15 Mradi wa DAWASA Kigamboni, Dar es Salaam Tanzania



Na Fredy Mshiu - DAWASA

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imesema, mradi wa maji Kigamboni wenye lengo la kutatua changamoto ya maji kwa wananchi utakamilika Aprili mwaka huu.

Haya yamesemwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Cpyrian Luhemeja alipotembelea na kukagua mradi huo katika siku ya tatu ya ziara yake ya kukagua maendeleo ya miradi ya majisafi na usafi wa mazingira.

"Tulikubaliana na mkandarasi kukamilisha ujenzi wa tanki lenye ujazo wa lita milioni 15 ifikapo mwishoni mwa Januari 2022, na maendeleo yake sio mabaya na mwisho wa Januari tunategemea kukamilisha," amesema Mhandisi Luhemeja.

Mhandisi Luhemeja amempongeza mkandarasi anaetoa maji visimani kwa kukamilisha ununuzi wa pampu tatu za kusukuma maji, huku akimuagiza kuongeza kasi katika mchakato wa manunuzi ya pampu za kutoa maji visimani kupeleka kwenye tenki.

"Namuagiza mkandarasi kukamilisha manunuzi hayo mapema ifikapo mwezi wa pili mwaka huu ili kukamilisha mradi huu, endapo ifikapo mwezi wa nne mkandarasi hajamaliza mradi tutamwondoa," amesisitiza Mhandisi Luhemeja.

Katika hatua nyingine, Mhandisi Luhemeja ameeleza hatua ya pili ya mradi ni kupeleka maji Kongowe kwani ni karibu na maji yapo ya kutosha huku hatua ya tatu itahusisha kupeleka maji Mbagala ambapo yote haya yatafanyika ndani ya mwaka huu kabla ya Disemba.

Shughuli ya usambazaji wa mabomba kupitia mradi huu wa maji Kigamboni inatarajiwa kuanza Jumatatu tarehe 17 Januari mwaka huu huku Afisa Mtendaji Mkuu, Mhandisi Luhemeja akielekeza Menejimenti ya DAWASA kuhakikisha wanaendeleza mapambano kukamilisha mradi huu ndani ya muda


TOKA MAKTABA :

January 24, 2016 by Global Publishers

Matengenezo ya bomba kubwa la maji yaendelea Kawe-Tegeta​


4
Kazi ya Kuunganisha Bomba la Maji kutoka mtambo wa uzalishaji wa Ruvu Chini ukiendelea katika eneo la Wazo Tegeta.
7
Matengenezo ya Bomba hili ndiyo yaliyopelekea kuzimwa kwa mtambo wa uzalishaji maji wa Ruvu Chini ambapo kwa muda wa saa 48 huduma ya maji itakosekana katika jiji la Dar Es Salaam na Bagamoyo.
5
Afisa Mtendaji mkuu wa DAWASCO Mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumza juu ya matengemezo hayo alipotembelea katika eneo hilo kujionea shughuli zinavyoendelea.
 
13.01.2022
Mradi wa Maji Kigamboni utakamilika Aprili 2022, na tunategemea kuanza kazi ya ulazaji wa mabomba ya usambazaji maji kwa wananchi mapema wiki ijayo" Mhandisi Cyprian Luhemeja, Afisa Mtendaji Mkuu -DAWASA


02 November 2022

Mfumo wa Maji kutoka Kigamboni kwenda mjini Kati, Temeke, Buguruni DSM


Waziri Mkuu ambana mkurugenzi wa DAWASA kuhusu kukamilika kwa mradi wa maji Kigamboni jijini Dar es Salaam



Mradi wa Kigamboni kupeleka maji awamu ya kwanza maeneo ya Mjini Kati (City centre), Tuangoma, Mbagala , Keko Mkapa stadium, Temeke, Buguruni huku maeneo mengine ya Dar es Salaam yatafuatia ... baada ya mpango kazi na utafiti kukamilika ili DAWASA iweze kuwafikia kwa huduma hiyo kutoka chanzo cha maji ya visima vya Kigamboni .... waziri mkuu asisitiza maji yatoke kuanzia.....

Source : Mwananchi digital
 
2 February 2022
Dar es Salaam, Tanzania

KINONDONI KIMEUMANA: MEYA AFUTA MAANDISHI YA DAWASA - ''WAZIRI AWESO AINGILIE KATI MGOGORO HUU'...



Madiwani wa Manispaa ya Kinondoni wakiongzowa na Mstahiki Meya wa manispaa hiyo, Songoro Mnyonge wametinga katika eno la Kiwanja kinachodaiwa kuwa cha manispaa hiyo kilichopo eno la Mikocheni A Dar es Salaam na kufuta maandishi yanayodaiwa kuandikwa na Mamlaka ya Maji Dar es Salaam (DAWASA) kwa madai ya kuwa eneo hilo siyo la kwao na kumtaka Waziri wa maji, Jumaa Aweso kuingilia kati mgogoro huo ili ijulikane mmiliki halali .....

Source : Global TV online
 
Back
Top Bottom