Awamu ya Zanzibar kutuletea mgombea urais

Kasema nani kuwa kuna zama?
Kama ndivyo nami mbara nisiye na chama ntaenda kugombea Zanzibari ati!? Unashangaa nini!?
 
Tunataka mzalendo wa kweli na sio hao wanaotokana na CCM chama koloni.

Nyerere aliacha kazi yake nzuri ndani ya serikali ya kikoloni na baadae akajiuzulu uwaziri mkuu chini ya serikali halali aliyoapa kuitetea na kuwajibika kwake na hatimaye akawa mpigania uhuru.
Nyerere angekua kama hao wana CCM wa leo angebakia kuisifia serikali ya mkoloni aliyokua anaitumikia na kuwaaminisha watu kuwa waafrika wafuate tu sheria za mkoloni na wasifanye fujo ili wawe salama.

Hii nchi chini ya CCM hata kama atatoka Zanzibar bado tutabaki na utawala wa mkoloni mweusi.

Bila CCM kupunguzwa nguvu au kushindwa na kukaa pembeni hakuna mabadiliko ya kifikra ambayao ni mabadiliko ya msingi.

CDM walitaka mabadilikp ya kifikra ,CCM wakaja na mabadiliko ya vitu kwa kutumia watu wale wale.
Mfano chini ya CCM watanzania wanaaminishwa kuwa Mwenge unaleta maendeleo.
Chini ya utawala wa CCM wapinzani sio watu sawa na wale wa CCM, ni watu wasiokua na haki yoyote ile mbele ya viongozi kama maRC na MaDC na hata hawana hadhi ya kukosoa au kutoa ushauri.
Ndio maana haifai kabisa kuipa tena CCM madaraka ili nchi yetu iwe na dira ya kitaifa na kujenga taifa lenye haki sawa ambapo mpinzani akipigwa Risasi iwe sawa na yule wa CCM na pasiwe na kubaguliwa mbele ya kuchukua hatua.
Chini ya CCM Mbunge anakamatwa na kuwekwa ndani kama kibaka kwa amri ya DC kwa mambo ya kisiasa kwenye jimbo alilochaguliwa kwa kura. Ina maana heshima ya mbunge inapatikana pale tu atakapolamba viatu vya DC au RC hata pale anaposimamia ukweli wa kidemokrasia.?

Ni aibu kama bado kuna mtu anawaza tena kupata kiongozi mwingine kutoaka kwa wakaoloni wetu wa leo ,CCM.
Hatutaki mabarabara yanaoondoa utu wetu na heshima yetu.
Kila binadamu aliyewekwa na Mungu hapa Tanzania awe ni kichaa au mzima anapaswa kulinda kwa kodi ya wananchi na sio fadhila za watawala.
Tunataka tufikie huko ili maendeleo yaje kwa haki na usawa na sio kwa manufaa ya watawala ya kujipatia kura.
 
Kama ni Hussein Mwinyi hata mimi nakuunga mkono. Mimi simfahamu binafsi lakini nina rafiki yangu wa karibu ambaye anamfahamu huyo bwana vizuri sana, alikuwa anaongelea mambo mazuri sana kuhusu yeye. Nakumbuka hayo maongezi yalikuwa takribani miaka miwili iliyopita na mimi bila kusita nikamwambia rafiki yangu huyu anaweza akawa rais sikumoja. Rafiki yangu anasema Dk. Mwinyi alikuja hapa Uingereza kusomea shahada ya udakitari lakini kwasababu masomo yake ya awali aliyafanyia Uturuki Waingereza wakawa na shaka na kiwango chake cha elimu wakamwambia arudie level ileile ambayo alikwisha isoma Uturuki kwa kiwango cha hapa Uingereza lakini baadae wakamwacha aendelee na level ya juu kwasababu kila kitu kilikuwa rahisi kwake. Lakini si elimu tu, pia nasikia ni mtu wa busara. Halafu nilivyokuja likizo Tanzania mwaka 2015 nilikuwa naongea na mdogo wangu mambo ya siasa ikaja tena habari ya Dk. Mwinyi. Mdogo wangu akaniambia pale Muhimbili alikuwa ni mchapakazi kweli mpaka baadhi ya madaktari wenzake walikuwa wanamchukia, baadhi yao walikuwa ni wavivu (kama tulivyo Watanzania!). Sasa wakimuona anafanya kazi sana wanasema eti anajifanya anajua. Nasikia alikuwa akimaliza kazi pale Muhimbili haondoki mpaka afanye 'handover' kwa daktari anayefuata wakati daktari mwingine angeondoka na kuacha wagonjwa akawahi kukata kiu kwenye baa.

Dk Mwinyi sio mzanzibari kama vile Salim Ahmed Salim hawa watu ni wazanzibari jina tu,hawana uhusiano wowote na zanzibar kisiasa,kimila hawaijui Zanzibar,hawa watu ni "sale out"......

Karume ndio anafaa kuwa raisi wa Tanzania kutoka Zanzibar...
 
Mtanzania yeyote mwenye sifa ana haki ya kuwa Rais wa nchi hii. Siyo lazima atoke zanzibar maana na Zanzibar ni sehemu ya Tanzania kama ilivyo CHATO, Mtwara, Nkasi n.k
TsafuRD,
Hakika Mtanzania yeyote anaweza kuwa rais wa Tanzania.
Lakini kuweka mizania katika utawala wa nchi yeyote hili ni jambo la lazima.

Ikiwa kila siku rais anatoka Tanzania Bara hii inaweza kuleta fitna baina ya
nchi mbili hizi zilizoungana.

Halikadhalika ikiwa jamii moja katika nchi inahodhi fursa zote katika nchi
hii pia ni chanzo farka.

Zanzibar haijapata kuwa kama Chato, Mtwara nk na haitakuwa.
Zanzibar ni nchi iliyoungana na Tanganyika.
 
Kama ni Hussein Mwinyi hata mimi nakuunga mkono. Mimi simfahamu binafsi lakini nina rafiki yangu wa karibu ambaye anamfahamu huyo bwana vizuri sana, alikuwa anaongelea mambo mazuri sana kuhusu yeye. Nakumbuka hayo maongezi yalikuwa takribani miaka miwili iliyopita na mimi bila kusita nikamwambia rafiki yangu huyu anaweza akawa rais sikumoja. Rafiki yangu anasema Dk. Mwinyi alikuja hapa Uingereza kusomea shahada ya udakitari lakini kwasababu masomo yake ya awali aliyafanyia Uturuki Waingereza wakawa na shaka na kiwango chake cha elimu wakamwambia arudie level ileile ambayo alikwisha isoma Uturuki kwa kiwango cha hapa Uingereza lakini baadae wakamwacha aendelee na level ya juu kwasababu kila kitu kilikuwa rahisi kwake. Lakini si elimu tu, pia nasikia ni mtu wa busara. Halafu nilivyokuja likizo Tanzania mwaka 2015 nilikuwa naongea na mdogo wangu mambo ya siasa ikaja tena habari ya Dk. Mwinyi. Mdogo wangu akaniambia pale Muhimbili alikuwa ni mchapakazi kweli mpaka baadhi ya madaktari wenzake walikuwa wanamchukia, baadhi yao walikuwa ni wavivu (kama tulivyo Watanzania!). Sasa wakimuona anafanya kazi sana wanasema eti anajifanya anajua. Nasikia alikuwa akimaliza kazi pale Muhimbili haondoki mpaka afanye 'handover' kwa daktari anayefuata wakati daktari mwingine angeondoka na kuacha wagonjwa akawahi kukata kiu kwenye baa.
Uko sawa mkuu ispokuwa mimi nimejaribu kuwasaidia kiushauri tu hawa ndugu zetu wajaribu kuamka kwa kufanya wanayoweza kwa manufaa ya nchi yao na vizazi vyao.
Naishangaa hii srikali ya tanzania wanaposema tanzania ni moja je inapotokea mtanzania wa unguja kaleta bidhaa kutoka nje ya nchi ikesha hiyo bidhaa ikipokewa unguja na ukiamua kuileta dar hapo ni mtihani mkubwa lazima utadaiwa kulipia kodi kama vile hiyo bidhaa umeagiza kutoka nje ya nchi.
Hii nini maana yake kama sio unyanyasaji wa wananchi wa upande huu?
Halafu ukiwaambia nchi ni moja kwanini mnanilipisha ushuru ndani ya nchi yangu?
ITAPENDEZA SANA
WAKIFANYA MABADILIKO[emoji196] [emoji83]
 
Kasema nani kuwa kuna zama?
Kama ndivyo nami mbara nisiye na chama ntaenda kugombea Zanzibari ati!? Unashangaa nini!?
Ulishaenda kuomba kugombea ukakataliwa?
Si unasema tanzania ni moja..
Nikupe mfano wewe kama unakaa dodoma kisha nenda mtwara kajaribu kuomba kugombea kiti mfano cha udiwani tu utapata majibu yako.
 
Dk Mwinyi sio mzanzibari kama vile Salim Ahmed Salim hawa watu ni wazanzibari jina tu,hawana uhusiano wowote na zanzibar kisiasa,kimila hawaijui Zanzibar,hawa watu ni "sale out"......

Karume ndio anafaa kuwa raisi wa Tanzania kutoka Zanzibar...
Kwahiyo dr. Husein tuambie kwao ni wapi
 
Kwann mtoto wa Mwinyi?

Inamaana kati yao wte hakuna mwenye uwezo isipokuwa huyo ambaye baba yake amewahi kuwa rais mwataka na mtoto pia?

Halafu haya mazoea yanataka kujenga tabia, badala ya kujenga nchi na aliyepo mnawaza atae kuja

Hivi nani aliyewaloga
Ana uzoefu mkubwa wa kufanya kazi na majeshi ya ulinzi nchini.
 
TsafuRD,
Hakika Mtanzania yeyote anaweza kuwa rais wa Tanzania.
Lakini kuweka mizania katika utawala wa nchi yeyote hili ni jambo la lazima.

Ikiwa kila siku rais anatoka Tanzania Bara hii inaweza kuleta fitna baina ya
nchi mbili hizi zilizoungana.

Halikadhalika ikiwa jamii moja katika nchi inahodhi fursa zote katika nchi
hii pia ni chanzo farka.

Zanzibar haijapata kuwa kama Chato, Mtwara nk na haitakuwa.
Zanzibar ni nchi iliyoungana na Tanganyika.

Uko sawa ila kuna baadhi wanajifanya vichwa vyao vimejaa matope kama huyu ndg uliemjibu
TsafuRD
 
TsafuRD,
Hakika Mtanzania yeyote anaweza kuwa rais wa Tanzania.
Lakini kuweka mizania katika utawala wa nchi yeyote hili ni jambo la lazima.

Ikiwa kila siku rais anatoka Tanzania Bara hii inaweza kuleta fitna baina ya
nchi mbili hizi zilizoungana.

Halikadhalika ikiwa jamii moja katika nchi inahodhi fursa zote katika nchi
hii pia ni chanzo farka.

Zanzibar haijapata kuwa kama Chato, Mtwara nk na haitakuwa.
Zanzibar ni nchi iliyoungana na Tanganyika.
jingalao
 
Zenj ni Nchi kamili, bara hatuhitaji rais toka kwao na wala wao pia hawahitaji mtu toka bara agombee urais.
 
Yaani tuongozwe na Rais kutoka nchi nyingine?

Maajabu haya
 
TsafuRD,
Hakika Mtanzania yeyote anaweza kuwa rais wa Tanzania.
Lakini kuweka mizania katika utawala wa nchi yeyote hili ni jambo la lazima.

Ikiwa kila siku rais anatoka Tanzania Bara hii inaweza kuleta fitna baina ya
nchi mbili hizi zilizoungana.

Halikadhalika ikiwa jamii moja katika nchi inahodhi fursa zote katika nchi
hii pia ni chanzo farka.

Zanzibar haijapata kuwa kama Chato, Mtwara nk na haitakuwa.
Zanzibar ni nchi iliyoungana na Tanganyika.
baadaya kuungana kila nchi ilipoteza sovereignity yake na kutengeneza nchji moja. Hivyo siyo nchi mbili tena. Ingekuwa hivyo nchi kama USA si wangekuwa wanapata shida sana kumpata Rais wa nchi? maana USA ni muunganiko wa nchi 52.
Cha msingi ni kumpata mtu sahihi wa kuiongoza nchi, siyo lazima atoke upande fulani.
 
Back
Top Bottom