Wazanzibar sasa ni wakati wenu kututolea mtu wa kuendesha hili lori TANZANIA maana kila kukicha ni bara tuuu ina maana wazanzibar nyie hamna uwezo wa kutoa mtu wa kusimama kidete?
Kwa kuwasaidia tu anzeni kumuandaa mtoto wa mzee Mwinyi aje kupeperusha kwa niaba ya wazenji.
Miaka hii mitatu inatosha kujiandaa.
Mwalla,
Hii fikra ya Zanzibar kutoa rais mbona hujaiweka vyema?
Umetanguliza gari mbele na punda nyuma.
Itakuwa tabu kuvuta mzigo.
Vipi CCM Zanzibar wafikirie kutoa rais wa Jamhuri ya Muungano ilihali wana tatizo
kubwa la kushinda urais Zanzibar toka uchaguzi wa vyama vingi uanze mwka 1995?
Swali lako labda lingekuwa hivi - ''Zanzibar ifanye juhudi ya kuondoa tatizo la uchaguzi
wa rais ili waweze kutoka mgombea urais wa Jamhuri ya Tanzania,'' au mfano wa hivi.
Vinginevyo utakuwa muhali mkubwa kwa Zanzibar kutoa mgombea urais ambae hawezi
kushinda kwao.
Lakini juu haya yote umeleta jamvini mada nzuri sana ya kufikirisha.
Nasema ya kufikirisha kwani ikiwa hii fikra ipo Zanzibar haiwezi ikawa chanzo ni CUF.
Fikra kama hii itakuwa CCM Zanzibar na wao ili kufikia hatua hii watahitaji kupata kiongozi
kwanza ambae ataweza kuleta umoja wa Wazanzibari wote.
Kwa hali ya Zanzibar ilivyo kwa hivi sasa hii si kazi ndogo.