Huo ndio ukweli. Kuna watu wanazunguka sana kutafuta mchawi wa kinachoendelea hapa Tanzania. Kwa sasa kuna chuki za kisiasa na uhasama uliopitiliza na kuhatarisha umoja wa Kitaifa.
Awamu ya Tano haiwezi kuepuka lawama hizo kwa hoja mbalimbali.
Tukumbuke tu kwamba kwa kiasi hiki cha miaka kama 25 baada ya kuja vyama vingi Tanzania, Utamaduni wetu uliathiriwa kwa kiasi fulani na ushabiki wa kivyama na kutengeneza ushindani wa sera na kufanya chaguzi kupata viongozi mbadala. Hapa paliongezeka kionjo kwenye utamaduni wa Watanzania na kuongeza siasa za kuvumiliana kama sehemu yautamaduni wetu.
Siasa ni sehemu ya Utamaduni wa watanzania lakini ikiendeshwa kwa kufuatwa kanuni zake japo watawala waliopita nao walikuwa na madhaifu yao. Madhaifu hayo yalikuwa ni kama mchezo wa kisiasa na kamwe haikufika mahali kukajengeka chuki kiasi hiki.
Awamu ya tano imevunja utamaduni wa kisiasa uliojengwa wa kuvumiliana na kushindana kwa hoja leo tunaona siasa ya Dola dhidi ya vyama vya siasa.
Vyama vya siasa vimeporwa uhuru wa kufanya siasa za kishindani kwa kuzuiwa kufanya mikutano na maandamano.
Viongozi wa upinzani wananyanyasika kupata haki zao za kisiasa kutoka vyombo vya dola kama Polisi na kuingiliwa shughuli zao kinyume na taratibu na utamaduni wa kisiasa.
Chama tawala kinanufaika na Udola kwa viongozi wake kutumia mwavuli wa Kiserikali kujiimarisha huku wakiacha dhambi hiyo ikiitafuna Taifa.
Huwezi kuamini kwamba Rais na Mwenyekiti wa CCM anafanya kampeni kweupe kabla ya muda kufika kwenye mikutano yake tena na kupigiwa kampeni na wakina Harmonize si msajili wa vyama vya siasa wala Mutungi anayejali. Katika hali hiyo lazima chuki ijengeke.
ATHARI
Wanasiasa wa upinzani, wanahabari, wanaharakati na taasisi za kiraia wote ni wanajamii na wana wafuasi wao, kinachowapata makundi hayo kinaipata jamii vile vile.
Huu mgawanyiko uliopo na kuombeana mabaya NI ZAO LA CHUKI HIYO. Na awamu hii ya tano inahusika.
Makundi mbali mbali yameshaeleza hatari iliyopo na kubezwa na hakuna hatua zinazochukuliwa hadi sasa si viongozi wa serikali si msajili wala viongozi wa dini.
Jamii inazidi kugawanyika, kuombeana mabaya na kuongezeka visasi baina ya watanzania.
NINI KIFANYIKE?
Tunarudia tena kufanywe mjadala wa Kitaifa na kuwakutanisha wanasiasa wote kwa Maslahi ya Tanzania. Tuanzie hapo.
Katiba mpya ipewe kipaumbele ili kutenganisha siasa na Udola, na kuweka taratibu zetu vizuri ili kuendana na mahitaji ya vyama vingi, uchumi wetu, maadili na haki.
Kwenye hili la chuki na kupotea umoja wa kitaifa awamu ya tano haiwezi kukwepa lawama na ndio ina wajibu wa kuurejesha.
Kwa hisani ya mtu wa Tanzania.
Kishada.