Ni Serikali na CCM ambayo Watanzania wamehitaji kwa miaka Mingi.

Robert S Gulenga

JF-Expert Member
Jan 3, 2013
2,161
1,493
Wapinzani wana piga kelele na kuandamana, kwa hakina Watanzania walio wengi hawawaelewi.

1. Kwa miaka mingi Vyama vya Upinzani vimeomba Uhuru wa kufanya siasa ikiwa ni pamoja na kuandamana, Serikali hii ya Samia Suluhu Hasan imewapa wanachohitaji.

2. Watu walihitaji uhuru wa kutoa maoni, kwa sasa unaweza kutoa maoni tu usivunje Sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

3. Watanzania walihitaji kuona Maendeleo na sio takwimu kwenye makaratasi, ni Awamu hii unaweza kuona Mradi mikubwa ikifanya kazi kama JNHPP, SGR, Shule za Sayansi mpya kila mkoa, Hospitali mpya, vituo vya Afya vipya kila kata, Zahanati kila kata,

4. Ni awamu hii tunaona ugatuzi wa Madaraka, Awamu hii ndio unaona Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Wakurugenzi kila siku wako Vijijini kusikiliza kero za Watanzania. HONGERA SAAANA MH. MCHENGERWA WAZIRI OR TAMISEMI kwa Kurudisha madaraka kwa Wananchi.

5. Watanzania wanataka huduma, na huduma wanazipata.

6. Yawezekana Siasa zimekuwa sehemu ya Maisha ya watu, ndio maana hata mambo yakiwa yanaenda sawa instead ya kuungana kama Taifa watatafuta jambo waweze kuandamana lakini ni Serikali hii imewaita mezani vyama rafiki wakakimbia mezani.

7. Mtalindwa kila siku barabarani.

Mwenyezi Mungu mbariki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

Mwenyezi Mungu ibariki Tanzania.
 
Back
Top Bottom