Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 15,321
- 24,192
- Thread starter
- #21
Hayo unayotoa ni mawazo tegemezi ya mtu anayeshindwa kufikiri nje ya box.Mwekezaji alikuwa sio mtu wa kuaminika, ana makado-kando mengi sana tokea alivyokuwa Mwanza. Hata kupata huo miradi aliupata kimagumashi maana hajawahi kuendesha miradi kama huo popote pale duniani. Kwa tatizo lilikuwa kwenye upangaji wa nauli ambapo yeye alitaka iwe juu zaidi, serikali ilimkatalia kupandisha nauli. Akaona apunguze mabasi kwa kusingizia mabovu ili asitumie gharama kubwa kwenye uendeshaji na yeye apate mgao unaomtosha, kitu ambacho ni kinyume na dhana ya miradi huo. Matokeo yake, uhaba wa mabasi uliongezeka, abiria kujazana kwenye mabasi na mwisho watu kuyasusa kurudi kutumia magari yao.
Lakini tokea 2015, awamu ya tano imejaribu kutafuta wawekezaji wanaoelewa maswala ya usafirishaji mijini, lakini kila mwekezaji anayekuja anakutana na Madudu ya uzembe, anakimbia. Ili kupata mwekezaji mwenye nia, lazima serikali wasafishe wahuni wote waliokuwa kwenye miradi huo na kurudisha shirika kwenye hadhi ya kubinafshwa.
Ati mtu hajawahi kuendesha mradi kama huo duniani!
My foot!
Nyie bongolala mmejiaminisha kuwa hamuwezi kitu mpaka mzungu awatie boost.
Mtaamka lini?
Mtimanyongo wenu unaua ari ya uwekezaji wa Watanzania.
Mfanyabiashara akiwekeza kigezo lazima kiwe faida na gharama za uendeshaji.
Walioajiriwa huwa hawajui hii fact.