Historia ya utawala wa awamu ya tano mwaka 2015 - 2020

Hashimu lwenje

JF-Expert Member
Oct 2, 2017
415
359
HISTORIA YA UTAWALA WA AWAMU YA TANO MWAKA 2015 MPAKA 2020

Utawala wa awamu ya tano ulianza mwaka 2015 mpaka 2020 ukiongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Katika utawala wake Rais huyo aliitwa majina mbalimbali kutokana na utendaji aliouonyesha katika kipindi chake. Wapo waliomwita mchaMungu, wapo waliomwita Rais wa wanyonge, wapo waliomwita Mwamba, wapo waliomwita Tingatinga, wapo waliomwita shujaa wa Afrika na wengine walimwita nabii aliyetumwa na Mungu.

Ingawaje katika maisha yake ya uongozi alipata upinzani mkubwa lakini Dkt. Magufuli aliishi maisha marefu sana. Dkt. Magufuli aliaga dunia tarehe 17 march 2021.

⚒️Kabla Rais Magufuli hajaingia madarakani Kama rais alikutana na vita kubwa toka kwa Viongozi wazembe katika Wizara alizowahi kuziongoza. Huko alifanyiwa mambo mengi maovu ikiwemo kunyweshwa Sumu kwa lengo la Kumuangamiza. Lakini Mungu alimvusha salama. Lakini Vita ya Mchakato wa Uchaguzi ndani ya Chama dhidi ya Mabwenyenye yenye Pesa yaliyotaka kupata madaraka kwa Gharama zozote zile haikuwa ndogo. Vita hii iliendelea hata baada ya Uteuzi ndani ya Chama. Baadae Vita hii iliendelea kupitia Vyama Upinzani ambavyo viligeuka na kuwa Watetezi wa Mabeberu,Viligeuka na kuwa Watetezi wa Wapiga Dili na Wasaliti wa Taifa la Tanzania. Vita hii ilikuwa kubwa na bila Msaada wa Mungu Rais Magufuli asingefika March 17.

⚒️Baada ya Rais Magufuli kuingia madarakani alianzisha vita na Mafisadi na wahujumu Uchumi. Vita hii iliyogusa maslahi ya Wahujumu Uchumi, Wakwepa kodi, wauza Madawa ya Kulevya, Majangili na wanyonyaji ilikuwa Moja ya Vita hatari mno. Katika Vita hii kama sio msaada wa Mungu uwezekano wa Kufa mapema kuliko Amina Chifupa ulikuwa Mkubwa mno. Lakini Mungu alisimama naye mpaka katika kipindi chote.

⚒️Ujenzi wa Miradi Mikubwa ya Kimkakati kama Mradi wa Uzalishaji Umeme wa Rufiji alipingwa na Mataifa ya Ulaya kwa madai kuwa anaharibu mazingira, aliponunua Ndege alipigwa vita kwa Serikali kufunguliwa Kesi za uongo na Kweli na Ndege kukamatwa lengo likiwa kukatisha Tamaa jitihada za kufufua Shirika la Ndege la Taifa,Baada ya kuboresha bandari ya Dar es Salaam na kusainiana na Uganda kuhusu Ujenzi wa Bomba la Mafuta vita ilikuwa kali mno na baadhi ya Nchi za Afrika. Lakin vita ya kiuchumi ilinoga zaidi baada ya Ujenzi wa Reli ya mwendo Kasi (Standard Gauge). Katika Vita zote hizi Kifo cha Magufuli kilikuwa nje nje.

⚒️Wakati wa Mlipuko wa Janga la Corona Kifo cha Rais Magufuli kilikuwa nje nje zaidi kwani alionyesha wazi kabisa kutoruhusu Wananchi wake Kufanyiwa majaribio ya Chanjo. Msimamo wa Rais Magufuli uliyachukiza Mataifa ya Kigeni ambayo yalijizatiti Kufanya Biashara ya Chanjo na Kutengeneza matrilion ya Dola. Ila Rais Magufuli alipotilia shaka kuhusu Corona, Nchi zote Duniani zilikuwa zinashtuka na kuchukua tahadhali. Aliwahi kutahadharisha kuhusu Vipimo vya Corona na Barakoa (Mask) na Kweli Nchi zote Duniani zilirudi nyuma kuhusu Vipimo hivyo. Lakini mapema hivi Karibuni alikataa kuhusu Chanjo, na Nchi nyingi Duniani zilianza kuikataa Chanjo ya Oxford AstraZeneca. Hizi zote ni vita alizokuwa akipigana.

Hivyo basi unaweza kuona Rais Magufuli ameishi maisha marefu mno kuliko vita alizokuwa akipigana kwa manufaa ya Watanzania na Afrika kwa Ujumla.

Taifa la Tanzania limepoteza Shujaa ambaye Watanzania wazalendo tunamuita "Mpigania Uhuru wa Kiuchumi" huku mataifa ya Mabeberu na wafuasi wao wakipotosha historia.

Pumzika kwa Amani Rais John Pombe Magufuli, utaendelea kuwa Nembo ya Wazalendo wachache waliowahi kuongoza Barani Africa.

Maswali ya Msingi tunayomuachia Mungu ni Kama Rais Magufuli amekufa ama "SHETANI" ametumia Mkono wake kuzima Taa ya Watanzania na wanamajumui wa Kiafrika.

By Hashimu Lwenje
March 28 2021.
 
KWANGU MIMI PEKEE YANGU NI MTU SHUJAA.

Tupa chooni vikosa vya kibiadamu.
 
Back
Top Bottom