Habari za leo Wanajamvi,
Kwa kipindi kirefu Watanzania tulikuwa na shauku ya kupata Rais mwenye uwezo wa kufanya maamuzi magumu katika utendaji wake. Maamuzi ambayo yangelinufaisha Taifa huku pengine yakizua malalamiko kwa baadhi ya watu au lawama kwa baadhi ya ndugu na marafiki wa kiongozi huyo.
Kuna wakati Mh. Edward Lowassa akichangia Bungeni, huku akipigiwa makofi na Wabunge wengi, alipata kusema (nanukuu): “Tatizo la nchi hii mnazungumza mambo, mnazungumza hakuna utekelezaji. Tunazunguza lakini discipline ya Malaysia na hapa ni tofauti. Hapa kuna Uswahili mwingi wa kukaa bila kutekeleza mambo, mnaamua hamtekelezi. Inatakiwa chombo kinachoweza kufanya maamuzi magumu na yakawa maamuzi magumu yanayotekelezeka kweli kweli. Mkishakubaliana mambo yafanyike. Haiwezekani katika nchi kila mtu akawa analalamika, kiongozi analalamika, mwananchi analalamika” (mwisho wa kunukuu). Kutokana na hali ilivyokuwa, ya kutotekeleza makubaliano mara kwa mara EL pia alidai kuwa “Ni bora kufanya maamuzi na kulaumiwa kuliko kutofanya kabisa”. Aidha katika mchango wake huo EL aligusia maeneo mbalimbali yaliyohitaji maamuzi magumu kama vile foleni Jijini Dar, Reli ya Kati, na mengineyo.
Nilikubaliana na hoja za EL kwa asilimia 100%. Ni ukweli usiopingika kuwa miradi mingi ilizinduliwa na kuwekewa mawe ya msingi kwa mbwembwe nyingi iwe na viongozi wa serikali, viongozi wa mbio za Mwenge na wengineo, lakini miradi hiyo haijatekelezwa hadi leo. Bungeni kulijaa maazimio yenye matumaini lakini yote hayo hayakutekelezwa. Miradi mingi imeozea kwenye madimbwi ya “Tupo kwenye upembuzi yakinifu (feasibility study)” na “Tupo kwenye mchakato (process)”. Ilikuwa ukisikia madimbwi hayo mawili unajua tu hakuna kitu kinachoendelea, na yalishamiri sana hasa kisiasa katika kuzipotezea mantiki hoja zenye mlengo wa kuhoji maendeleo yake. Ni upembuzi yakinifu au mchakato ambao ulikuwa huwezi kuona mtu au kitu chochote katika eneo la mradi (site) kwa miaka mingi. Kwa kweli hayo madimbwi yalichosha watu wengi sana.
Mwaka 2015 ulifanyika uchaguzi mkuu na kumpata Rais John Magufuli. Ni Rais aliyependwa na watu wengi sana, waliompa kura na wale ambao hawakumpa kura pia. Nasema hivyo kwa sababu watu wengi walikiri kuwa Rais Magufuli ana uwezo mkubwa lakini wasingempa kura kwa sababu chama alichopeperusha bendera yake hawakukipenda. Lakini yeye JPM aliwahakikishia watu kuwa baada ya kuchaguliwa angeweza kufanya “Total system overhaul”; hali iliyopelekea watu wengi pia kumwamini na kumchagua kuwa Rais wa awamu ya tano. Ni Rais aliyebeba matumaini ya wengi, na aina ya Rais aliyekuwa ni ndoto ya watu wengi akiwemo EL (rejea quotation ya EL hapo juu).
Baada ya Rais JPM kuapishwa wote tuliona bidii zake. Kuna wengine walisema zilikuwa ni nguvu za soda lakini tunaona huu ni mwaka wa pili yupo at constant speed. Ni Rais mwenye uwezo wa kufanya maamuzi magumu na sisi sote tunaoona ni vema na haki (it’s right and just) kuongea ukweli tunampongeza.
Katika utawala wake tumeona kuwa madimbwi ya “mchakato” na “upembuzi yakinifu” yamekuwa ya kiutendaji zaidi na si ya kuua miradi/mipango. Tumeshuhudia mawe ya msingi yakiwekwa au maagizo yakitolewa; mapema tunaowaona watu katika maeneo ya miradi au kazi nyinginezo. Kwa mfano tumeona siku moja baada ya Rais kuliagiza Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kujenga ukuta kuuzunguka mgodi wa madini ya Tanzanite huko Mererani, watu wameonekana katika eneo la mradi wakifanya upembuzi yakinifu kwa hatua za utekelezaji. Kwa kweli ni suala la kupongezwa kwani kila aina ya uzembe au ubadhirifu kwa baadhi ya Viongozi au watendaji hauna nafasi kwake.
EL alizungumzia suala la foleni Jijini Dar. Mbali na miradi miwili mikubwa ya Ubungo Interchange na Flyovers pale TAZARA ambayo inaendelea kwa kasi baada ya kuzinduliwa na Rais JPM, pia kulikuwa na Mradi wa Magari yaendayo kasi maarufu kama “Mabasi ya Mwendokasi” - UDART. Kwa wakazi wa Dar mtakubaliana na mimi kwamba barabara za mradi huu kwa jinsi zilivyosasa zilikamilika muda mrefu sana, kukawa na ahadi zisizotekelezeka za uzinduzi wa huduma ya Mwendokasi. Tarehe zilikuwa zikibadilishwa kila kukicha hadi ikafikia hatua ya kuruhusu barabara hizo kutumiwa na magari mengine. Viongozi walikuwa na kigugumizi cha kuzindua huduma hiyo. Mapema baada ya Rais JPM kuingia madarakani akaamuru huduma hiyo ianze na kama kuna maboresho yafanyike huduma ikiendelea kutolewa. Cha ajabu hadi leo hakuna jipya kwenye mradi huo lililoongezwa na watu wanaendelea kufurahia huduma hiyo. Pengine Rais asingeamuru huduma hiyo kuanza, tungekuwa bado tunapewa tarehe za uzinduzi.
Kwa upande wa usafiri wa Treni ili kuokoa barabara zetu kama EL alivyosema Bungeni, tumeona mikataba ya ujenzi wa reli kwa kiwango cha “standard gauge” ikisainiwa, na michakato ya utekelezaji wa miradi hiyo ikionekana wazi katika maeneo ambapo miradi hiyo inajengwa. Na sasa mikataba ya Dar-Moro, na Moro-Makutopora imekwisha sainiwa na utekelezaji wake umeanza. Aidha katika kuziokoa barabara zetu mradi mkubwa wa bomba la mafuta toka Hoima, Uganda hadi Tanga, Tanzania umekwisha zinduliwa na utekelezaji umeanza. Kwa kifupi ni kuwa kuna miradi mingi sana ambayo inatekelezwa kwa spidi ya mwanga kiasi kwamba haitawezekana kuiorodhesha yote hapa; ikiwa ni pamoja na juhudi kubwa za kulinda rasilimali zetu kwa manufaa ya vizazi vyetu na vijavyo. Rais JPM hataki tena Tanzania kuwa “shamba la bibi” kwenye rasilimali zetu au kichwa cha mwendawazimu katika miradi mbalimbali.
Watanzania wote tunatamani Rais atufikishe Kanaani, nchi yenye maziwa na asali. Ni kweli kuwa ana jukumu la kutuongoza tufike huko. Lakini na sisi tuna wajibu zetu za kuzitimiza. Tunapaswa kushirikiana naye kwa nguvu zetu, na akili zetu zote ili kuhakikisha kuwa mipango inayowekwa na serikali inafanikiwa kwa kiasi kikubwa. Asipatikane mtu wa kusema “Je, si afadhali kwetu turudi Misri?”. Mtu wa aina hiyo tumkatae kwani atatuchelewesha katika kupiga hatua kubwa (au kusogea mbele) kimaendeleo. Kuna viwanda vinahitaji malighafi toka mashambani, basi wakulima limeni sana. Wawekezaji wa ndani wekezeni sana. Wafanyakazi katika sekta zote za umma na binafsi fanyeni kazi kwa bidii sana. Wafanyabiashara fanyeni biashara kwa bidii sana na kulipa kodi stahiki kwa hiari. Kila mmoja wetu afanye kitu kitakachosogeza maendeleo ya nchi mbele chini ya mazingira wezeshi yanayotengenezwa na serikali ya awamu ya tano.
Tukishindwa kufanya maendeleo makubwa chini ya Rais mwenye uwezo wa kufanya maamuzi magumu, kuna uwezekano wa kurudi nyuma au kutosogea mbele kabisa kwa muda mrefu kama awamu ya sita itakuwa na Rais mwoga katika kufanya maamuzi magumu. Tuitumie fursa hii kujiendeleza binafsi na kuiendeleza nchi yetu.
Benmpo