Nimekuwa nikiangalia na kushangaa kwa muda mrefu, avatar na majina tunayoyachagua yanatokana na nini hasa? unakuta mtu kaweka avatar ya jicho moja au kichwa nazi, mara avatar ina pengo, huwa najiuliza hivi leo Mungu anasema kuanzia leo uwe kama avatar yako sijui utafanya nini.
Watapona walioweka avatar za warembo, sijui itakuwaje aliyeweka avatar ya kike na yeye ni mwanaume.
Hebu tufunguke ilikuwaje ukachagua avatar na jina hilo.
Binafsi nilichagua jina la JEKI likiwa na maana nakuja katika JF kuwapiga jeki wasiojiweza kama vile jeki inavyomsaidia mtu aliyeharibikiwa na gari lake, avatar nayo ikawa jeki yenyewe.
Wewe je?