Augustino Mrema: Behind the Scene

mrema akiwa naibu waziri mkuu ... alianzisha utaratibu wa kuwaadhibu wanaochelewa kazini kwa watumishi wa uma ... utaratibu huu ulikuwa kwamba ukufika kazini baada ya saa mbili asubuhi unakuta kiti chako cha offisini kimeondolewa

pia aliwahi kuanzisha utaratibu wa kutoa siku saba za kujieleza kwa watumishi waliokuwa na makosa
 
Nadhani wengi hamufahamu vizuri ni mtu mbinafsi sana anayependwa kusifiwa kwa miaka ya nyuma alipata sifa sana na watu walikuwa hawafahamu sasa nenda vunjo wanajuta .kwa sasa amalize nngwe yake kwa kura za huruma alizopata.
 
Mnyonge Mnyongeni, lakini haki yake mpeni.
Katika kikao cha saba cha bunge lilohitimishwa jana, kamati yake ya Hesabu za serikali a mitaa ilitoa ripoti moja nzuri sana juu ya ubadhirifu mkubwa ulioonekana katika serikali za mitaa. Kamati yake, tofauti na kamati nyingine za bunge, ilithubutu kutaja kwa majina na mahali walipo wahusika wa ubadhirifu wa mali za halmashauri na kutoa mapendekezo mazuri sana ya hatua za kuchukua dhidi ya wahalifu hao na namna ya kuzuia wizi huo kwa siku zijazo. Mheshimiwa huyu aliongea kwa uchungu sana namna anavyoumizwa na wizi huu, huku huduma za kijamii zikizorota kwa kukosa pesa.

Behind the Scene (vibwagizo)

  • Mrema ni mtu pekee ambaye amewahi kupewa cheo kisichotambulika katika katiba ya nchi (Naibu waziri Mkuu), enzi za mzee Ruksa. Enzi hizo pia alikuwa ni waziri wa mambo ya ndani na utendaji wake ulijulikana sana.
  • Ni mtu pekee ambaye amekuwa mbunge katika majimbo mawili tofauti. Alikuwa mbunge wa Jimbo la Temeke mkoani Dar Es Salaam mnamo mwaka 1996 baada ya mahakama kutengua ubunge wa Ally Kihiyo, ambaye alighushi elimu yake katika wasifu wake, na kwa sasa Mrema ni mbunge wa jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro
  • Ni mtu pekee ambaye amekuwa mwenyekiti wa vyama viwili tofauti vya kisiasa kwa nyakati fofauti na amegombea uraisi kupitia vyama hivi viwili tofauti. Alikuwa Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi Mnamo mwaka 1995 enzi hizo Mabere Marando akiwa katibu mkuu na aligombea ubunge mwaka huo. Alihama NCCR na kuhamia TLP ambako alimpindua Leo Lwekamwa na kumtimua Thomas Ngawaiya aliyemkuta hapo, na amegombea uraisi mara mbili kwa tiketi ya chama hiki.
  • Ni mmoja wa wabunge waliokunywa 'Kikombe' cha Babu Ambilikile Mwasapile wa Loliondo

Mwenye vibwagizo zaidi aongezee
Nawasilisha

Hiyo sio yeye pekee.
Chambili ameongoza tarime miaka 14,sasa hivi ni mbunge wa jimbo moja huko Manyara.
 
Ndiye mwana ccm wa kwanza kuupinga ufisadi waziwazi,neno vigogo baada ya kukamata gold jnia,pia fisadi chavda
 
Mmesahau aliwahi kukamata pembe za nduvu uwanja wa ndege baada ya kuzuia atc isiruke na kumbe mzigo ulikuwa wa sitti mwinyi na msuya.baada ya kubainika mzee ruksa akakimbilia kwa mwalimu kutaka ushauri maana mkewe kashikwa pabaya.Mwl alimshauri mzee ruksa kumpromote kwa unaibu waziri mkuu ili akae kimya.akakubali.hiyo ilikuwa rushwa ya cheo.
 


  • ni mtu pekee aliyejichimbia chumbani mwake na kuibuka sebuleni kaishavaa digree na anataka tumtambue kuwa ni msomi
  • ni mtu pekee aliyepewa phd ya barabarani ingawa ni pumba kisomi
 
amewahi kuwa mbunge wa moshi vijijini, Temeke na sasa Vunjo ..... na amewahi kujiuzulu katika nyadhifa yake katika dhana ya uwajibikaji
ingawa kwa sasa uwezo wake upo katika stage ya "standstill"
Hii naikumbuka sana. Teh teh teh. Hiyo situation ya stand still huenda ikamgharimu ubunge mwaka 2015

hii thread kaanzisha mwenyewe mzee wa kiraracha pole sana mzee
Hapana. Mimi mwanzisha thread si wa Kiraracha, mie ni mpiga kura kutoka jimbo la Mhe. Profesa Maji Marefu

Mrema ndo waziri pekee aliyetishia kutandika wanaume viboko na kupunguza women abuse! Yule mkuu wa wilaya aliyeiga akacharaza waalimu sijui alihamishiwa wilaya gani?
Yule Albert Mnali hakuhamishwa, alikaushwa kabisa kibarua (uteuzi wake ulitenguliwa), kwa sasa ni raia wa kawaida tu.
Ni mtu pekee aliyeweka mapipa ya lami kule kilema akiwa na lengo la kujenga barabara
japo hakufanikiwa baada ya serikali kumtimua unaibu waziri, hivyo mshiko ukawa kidogo.
Hahahahhhh. Matumizi mabaya ya madaraka hayo

Chama chake ni chama pekee kinachotumia Jogoo kama alama ya Bendera yao. Na ni Mwaenyekiti pekee wa chama aliyeacha kumpigia kampeni mgombea wake wa urais 2010 na kumpigia ****** ili magamba yasimsumbue.
Hiki kioja nakikumbuka sana. Si yeye peke yake aliyefanya kituko hicho, yule jamaa wa PPT Maendeleo bwana Kuga Peter Mziray naye alifanya hivyo kule kwao Same.

Really no comment. Ni nini maudhui ya uzi huu?
Kwa nini unachangia kitu usichojua maudhui yake? Ushakunywa chai?

ni kiongozi pekee nchini aliyekuwa na uwezo wa kuwaamuru majambazi wasalimishe silaha zao na walifanya hivyo.
Hii na yenyewe ni ya kipekee

Kuna watu ni wagumu sana wa kuelewa. Wanataka kila kinachoandikwa humu basi kiwe kinaongelea only the future and present. Sijui kwa nini?
Tell them sir
Hao ni watoto waliozaliwa mwaka 1997 kuja juu, ambao hawajui legends wa nchi hii
 
Kama angekuwa na nafasi ya Pinda kwa sasa, angewapa SIKU SABA wale MAWAZIRI mafisadi wajiuzuru.
 
Huyu ni mzee wa siku saba! Watuhumiwa wote aliwataka wakutane naye kijijini kwake badala ya ofisini!
 
ni historia ya jimbo la kirua hawana wakati wakukupa uondoze mara mbili....
hata Mmrema anafahamu ili.....
changamoto kwa viongozi wajao...lazima ufanye kitu kionekane kabla na baada yakutaka ubunge kwa jimbo hili la VUNJO....ndiyo upewe ubungen
Nadhani wengi hamufahamu vizuri ni mtu mbinafsi sana anayependwa kusifiwa kwa miaka ya nyuma alipata sifa sana na watu walikuwa hawafahamu sasa nenda vunjo wanajuta .kwa sasa amalize nngwe yake kwa kura za huruma alizopata.
 
Back
Top Bottom