Augustino Mrema: Behind the Scene | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Augustino Mrema: Behind the Scene

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Idimi, Apr 24, 2012.

 1. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #1
  Apr 24, 2012
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,222
  Likes Received: 2,086
  Trophy Points: 280
  Mnyonge Mnyongeni, lakini haki yake mpeni.
  Katika kikao cha saba cha bunge lilohitimishwa jana, kamati yake ya Hesabu za serikali a mitaa ilitoa ripoti moja nzuri sana juu ya ubadhirifu mkubwa ulioonekana katika serikali za mitaa. Kamati yake, tofauti na kamati nyingine za bunge, ilithubutu kutaja kwa majina na mahali walipo wahusika wa ubadhirifu wa mali za halmashauri na kutoa mapendekezo mazuri sana ya hatua za kuchukua dhidi ya wahalifu hao na namna ya kuzuia wizi huo kwa siku zijazo. Mheshimiwa huyu aliongea kwa uchungu sana namna anavyoumizwa na wizi huu, huku huduma za kijamii zikizorota kwa kukosa pesa.

  Behind the Scene (vibwagizo)

  • Mrema ni mtu pekee ambaye amewahi kupewa cheo kisichotambulika katika katiba ya nchi (Naibu waziri Mkuu), enzi za mzee Ruksa. Enzi hizo pia alikuwa ni waziri wa mambo ya ndani na utendaji wake ulijulikana sana.
  • Ni mtu pekee ambaye amekuwa mbunge katika majimbo mawili tofauti. Alikuwa mbunge wa Jimbo la Temeke mkoani Dar Es Salaam mnamo mwaka 1996 baada ya mahakama kutengua ubunge wa Ally Kihiyo, ambaye alighushi elimu yake katika wasifu wake, na kwa sasa Mrema ni mbunge wa jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro
  • Ni mtu pekee ambaye amekuwa mwenyekiti wa vyama viwili tofauti vya kisiasa kwa nyakati fofauti na amegombea uraisi kupitia vyama hivi viwili tofauti. Alikuwa Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi Mnamo mwaka 1995 enzi hizo Mabere Marando akiwa katibu mkuu na aligombea ubunge mwaka huo. Alihama NCCR na kuhamia TLP ambako alimpindua Leo Lwekamwa na kumtimua Thomas Ngawaiya aliyemkuta hapo, na amegombea uraisi mara mbili kwa tiketi ya chama hiki.
  • Ni mmoja wa wabunge waliokunywa 'Kikombe' cha Babu Ambilikile Mwasapile wa Loliondo

  Mwenye vibwagizo zaidi aongezee
  Nawasilisha
   
 2. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #2
  Apr 24, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,328
  Likes Received: 1,793
  Trophy Points: 280
  Na ndiyo mtu pekee aliyepata degree kwa njia ya fax baada ya kutunukiwa na chuo fulani cha marekani, na kuzunguka mji mzima akiwa amejivarisha joho la kugraduate ili agombee uraisi.
   
 3. L

  LAT JF-Expert Member

  #3
  Apr 24, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  amewahi kuwa mbunge wa moshi vijijini, Temeke na sasa Vunjo ..... na amewahi kujiuzulu katika nyadhifa yake katika dhana ya uwajibikaji

  ingawa kwa sasa uwezo wake upo katika stage ya "standstill"
   
 4. gango2

  gango2 JF-Expert Member

  #4
  Apr 24, 2012
  Joined: Aug 31, 2011
  Messages: 1,237
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  loading......!
   
 5. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #5
  Apr 24, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Ni waziri pekee aliyeamua kuweka rehani uwazi wake kwa kukiuka kanuni ya collective responsibility huku akijua wazi kitakachofuata....
   
 6. M

  Makupa JF-Expert Member

  #6
  Apr 24, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  hii thread kaanzisha mwenyewe mzee wa kiraracha pole sana mzee
   
 7. Bhbm

  Bhbm JF-Expert Member

  #7
  Apr 24, 2012
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 716
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Nendeni mkajifunze kiswahili upya jamani lol, hamua=amua, hacha=acha, hogopa=ogopa.......mko wengi na mnakera sana.
   
 8. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #8
  Apr 24, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Wachaga hawajui kiswahili hebu acha kuwasakama shemeji zangu!
   
 9. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #9
  Apr 24, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Mrema ndo waziri pekee aliyetishia kutandika wanaume viboko na kupunguza women abuse! Yule mkuu wa wilaya aliyeiga akacharaza waalimu sijui alihamishiwa wilaya gani?
   
 10. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #10
  Apr 24, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,105
  Likes Received: 6,579
  Trophy Points: 280
  mwalimu mwenyewe hajui kiswahili mwanafunzi atajua kweli
  nashukuru umemfundisha hapa hapa jf.

   
 11. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #11
  Apr 24, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,105
  Likes Received: 6,579
  Trophy Points: 280
  Ni mtu pekee aliyeweka mapipa ya lami kule kilema akiwa na lengo la kujenga barabara
  japo hakufanikiwa baada ya serikali kumtimua unaibu waziri, hivyo mshiko ukawa kidogo.
   
 12. M

  Makupa JF-Expert Member

  #12
  Apr 24, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  mkuu mamdenyi inaelekea tumetoka sehemu moja, mbonyi mbee
   
 13. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #13
  Apr 24, 2012
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  LAT hapo kwenye red sikumbuki alipatakujiuzulu wadhifa gani.

  Kwenye blue umepiga chini ya mkanda kabisa na maumivu yake huwa makali sana.
   
 14. Jotojiwe

  Jotojiwe JF-Expert Member

  #14
  Apr 24, 2012
  Joined: Mar 24, 2012
  Messages: 325
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 45
  Mrema ndiyo JOGOO PEKEE LINALO WIKA TANZANIA
   
 15. K

  Kimbito nyama Senior Member

  #15
  Apr 24, 2012
  Joined: Apr 10, 2012
  Messages: 157
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Chama chake ni chama pekee kinachotumia Jogoo kama alama ya Bendera yao. Na ni Mwaenyekiti pekee wa chama aliyeacha kumpigia kampeni mgombea wake wa urais 2010 na kumpigia ****** ili magamba yasimsumbue.
   
 16. Gwankaja Gwakilingo

  Gwankaja Gwakilingo JF-Expert Member

  #16
  Apr 24, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 1,963
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Ni mbunge pekee wa upinzani aliepanda jukwaa la ccm na kuomba kura mbele ya mpinzani wake na akapata kura pamoja na mtaji wa tsh laki tano
   
 17. M

  Makupa JF-Expert Member

  #17
  Apr 24, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  ni mbunge pekee alieomba kura kwa wananchi kwa kuomba wampe kura za huruma kutokana na afya yake
   
 18. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #18
  Apr 24, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,744
  Likes Received: 1,457
  Trophy Points: 280
  Really no comment. Ni nini maudhui ya uzi huu?
   
 19. S

  SJUMAA26 JF-Expert Member

  #19
  Apr 24, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 611
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mhaya huyo, msamehe maana hata akiwa Prof. ataendelea kuvurunda hivyo hivyo!
   
 20. L

  LAT JF-Expert Member

  #20
  Apr 24, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  mkuu
  Augastine Mrema aliwahi kuwa afisa usalama katika wizaraya mambo ya ndani wakati huo Mzee Ali Hasan Mwinyi alikuwa waziri wa mambo ya ndani .... miaka ya 1980's kulitokea mauaji ya watu waliosadikika ni wachawi huko mwanza/shinyanga na Mwinyi kama waziri na Mrema walijiuzulu kupisha uchunguzi na uwajibikaji
   
Loading...