Augustine Lyatonga Mrema: Mpiganaji! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Augustine Lyatonga Mrema: Mpiganaji!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rev. Kishoka, Sep 13, 2009.

 1. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #1
  Sep 13, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Wakati naendelea kulumbana na FMES na Mzee Mwanakijiji kuhusu wajibu wa Wapiganaji, Vita ya Wapiganaji na ni nani anafaidika na Upiganaji, jina moja linakuja mukichwa na dhamira inaniambia kuwa hukukweli alikuwa ni mpiganaji.

  Mrema pamoja na udhaifu wake wa kuchemka kwa nguvu ya soda, kuwa na elimu duni na kufanya mambo kwa pupa, Kitendo chake cha kutoka CCM ni kwa kuwa aliweka Utaifa na Utanzania mbele na si maslahi yake binafsi au ya chama.

  Naomba mwenye kumbukumbu nzuri, atukumbushe ni kwa nini Mrema aliamua kuasi ndani ya Baraza la Mawaziri na hata kuamua kuachana na CCM na kuingia upinzani?

  Nakumbuka tetesi ni kuwa alikataa kukubaliana na uamuzi wa Baraza la Mawaziri (collectively responsibility) kufumbia macho wizi wa fedha BOT ama kupitia mfuko wa EPA au CIS na aligangamaa kuwa ataanzisha uchunguzi na kupeleleza kilichotokea. Alipoambiwa alifumbie macho, akaghadhibika na kukataa kukaa upande mmoja na Baraza la Mawaziri na Serikali na hivyo kuasi na kulazimika kujivua/kuvuliwa uwaziri na mwishowe kujitoa CCM.

  Mrema hakujali maslahi yake au kitakachotokea kwake baada ya kuondoka CCM (life after action), ingawa aliingiwa na pupa ya kutaka apewe uenyekiti wa CHADEMA na alipokataliwa, ndipo akaungana na Wana Usalama wenzake kina Mabere Marandu kule NCCR.

  Ninachotaka kujengea hoja ni kitendo chake cha kukataa kukubali kufumbia macho uhalifu na uhujumu na kutii amri ya kuwajibika kwa jumla kuruhusu Uhujumu.

  Je ni Watanzania wangapi na Wapiganaji wangapi ambao leo hii wako tayari kupoteza nafasi zaoza kazi na maslahi wakiwa katika mfumo wa Kiutawala na Kisiasa kwa kusimamia haki, utu na uwajibikaji ili kulinda maslahi ya Watanzania na Taifa?
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Sep 13, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Ametajwa mara nyingi kuwa ni pandikizi la ccm upinzani na kuwa atarudi tu ccm. Miaka imepita na majaribu mengi amepitia lakini hajapiga magoti kwa ccm. Kati ya wapiganaji wote huyu ndiye shujaa wangu. Natumaini historia itamhukumu vyema na kwa haki.
   
 3. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #3
  Sep 13, 2009
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,007
  Trophy Points: 280
  nadhani Mrema alishindwa kujua kama hao wakina Marando hawakuwa wapinzani wa kweli na hili lilitokana na IQ ndogo ya mkuu, lakini ki ukweli anabaki kuwa Mpinzani wa kweli na kweli alikuwa kwa sababu ya Wananchi, uhamizi alioufanya Mrema, sidhani pamoja na kelele zao zote kama kweli Mwakyembe, Sitta, Selelii na wapigananji wengine wote kama wataweza kwenda upinzani
  Mrema alienda upinzani akiwa anakubalika na chama chote na alikuwa na cheo ambacho hata kikatiba hakipo (Naibu Waziri Mkuu),
  lakini hao wengine wataingia upinzani kwa sababu ya kutengwa na kunyimwa madaraka (ubunge) ndani ya CCM
   
 4. I

  Interested Observer JF-Expert Member

  #4
  Sep 13, 2009
  Joined: Mar 27, 2006
  Messages: 1,402
  Likes Received: 434
  Trophy Points: 180
  "hili lilitokana na IQ ndogo ya mkuu" Umenichosha kabisa, sasa hapo IQ inatoka wapi; mwenye IQ kubwa anaweza kutabiri ya mbeleni? Some comments!!!!!!
   
 5. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #5
  Sep 13, 2009
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Mkuu umenikumbusha ile story ya SHUJAA na JASIRI. Tupo pamoja mkuu.
   
 6. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #6
  Sep 13, 2009
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  i think he/she meant kuwapima, sio foresight in its literal sense
   
 7. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #7
  Sep 13, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Mimi ni mwumini wa Mrema mpaka leo na naamini alisaidia sana kujengaupinzani wa nguvu. Wapinzani wengi wa sasa, hasa upande wa wananchama ni wale ambao Mrema aliwavuta akiwa NCCR. Kwasas wanahama kutoka chama kimoja kwenda kingine.

  Ndio, alikuwa na mpungufu yake kama mtu mwingine yeyote lakini kweli jamaa alikuwa mpiganaji na mtu ambaye utekelezaji wa jambo lolote alilokuwa analisimamia ulikuwa unapewa kipau mbele.

  Najua wasomi wengi ambao wao wenyewe ni zero kwenye utekelezaji walimpiga vita lakini ukweli utabaki pale pale kwamba Mrema alikuwa waziri mtekelezaji kuliko waziri mwingine yeyote kwenye serikali ya rais Mwinyi.

  Watu wamejaribu kusema Mrema alikuwa na pesa nyingi au alichuma pesa nyingi akiwa waziri lakini maisha yake ya shida baada ya kuondoka CCM yanaonyesha wazi jamaa hakuiba. Pia pamoja na maisha yake ya shida na kuumwa kwingi bado Mrema amekataa kurudi CCM na kuamua kuendelea na harakati zake hata kama zitaishia kumpeleka kaburini mapema.

  Kosa kubwa alilofanya Mrema na wafuasi wake lilikuwa lile la kuamini kwamba angeishinda CCM kwa nguvu ya NCCR peke yake. Alishindwa kuunganisha upinzani pamoja na pia alishindwa kuwavuta baadhi ya viongozi wa CCM hasa kundi la mtandao ambalo lilikuwa limechukizwa na kuangushwa kwa JK. Huenda hili ndilo kosa ambalo linarudiwa tena na CHADEMA mwaka huu.

  Naamini angemvuta JK au Lowassa ili wagombee urais na yeye kuwa tayari kuwa PM, wangelikuwa na nafasi kubwa sana ya kushinda.
   
 8. M

  Magezi JF-Expert Member

  #8
  Sep 13, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Mrema kwa sasa anastahili angalau apate ubunge ili apumzike kwa sababu kama ni mateso, CCM walimtesa vya kutosha. Lakini kwa kiapo chake yeye bado ni CCM damu kwa sababu sijaona akirudisha kadi ya kijani.
   
 9. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #9
  Sep 13, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Ndio maana nasema Vita dhidi ya ufisadi siyo ya CCM walidandia gari kwa mbele, Lakini Makamba yupo Sahihi sana kwa ajili hawa Makamba dhidi ya ufisadi
   
 10. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #10
  Sep 13, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Ndio maana nasema Vita dhidi ya ufisadi siyo ya CCM walidandia gari kwa mbele, Lakini Makamba yupo Sahihi sana kwa ajili hawa Makamba dhidi ya ufisadi
   
 11. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #11
  Sep 13, 2009
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Mkuu Rev. Kishoka
  Mheshimiwa Mrema hakungoja kuambiwa arejeshe kadi kama ilivyokuwa kwa Mheshimiwa Sitta.Mrema bado anaendelea kuwa shujaa wa kupampambana na ufisadi na aliyetanguliza maslahi ya taifa mbele badala ya maslahi ya chama au maslahi binafsi kama ilivyokuwa kwa mheshimiwa Sitta.

  Nawashangaa baadhi ya wanasiasa wa kambi ya upinzani wanao kuja na hoja eti Mrema ni pandikizi.Mrema aliisumbua sana CCM na usalama wa taifa tatizo ni yeye kukubali kujiunga na lile kundi la wanausalama NCCR Mageuzi ya akina Marando.
   
 12. S

  Subira Senior Member

  #12
  Sep 13, 2009
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 162
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  yaani mimi nauthamini mchango wake kwa nchi hii sana na pia he is a leader of his sort ambae tungependa kuwa nae mwenye uwezo wa kuamua jambo na kulitolea ufumbuzi linapojiri we need strong leaders jamani . waafrica wanatakiwa kutishwa tishwa. na ni mpambanaji sana bwana.
   
 13. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #13
  Sep 13, 2009
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Lakini ktk uchaguzi wa Tarime na Biharamulo, CHADEMA walisema Mrema ni pandikizi la ccm.

  Hapa ktk maono yangu kati ya Mrema na CHADEMA mmoja lazima atakuwa pandikizi sasa ni nani? Mrema ama CHADEMA
   
 14. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #14
  Sep 13, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Ugomvi kati ya Mrema na CHADEMA ni kutokana na kitendo cha Mrema alipofuatwa kujiunga CHADEMA, alitoa sharti moja kuwa lazima apewe Uenyekiti wa Taifa CHADEMA. Mtei alimwambia Mrema akitaka kuwa kiongozi wa CHADEMA, sharti aanzie kwenye ngazi za mtaa, kijiji, tarafa, wilaya, mkoa na ndipo aje Taifa, na si kurukia Usukani tuu.

  Mrema akakataa na NCCR walipoona kuna mtu mashuhuri kama huyu na ndio walikuwa wakijiweka sawa baada ya mgawanyiko wa Wapinzani, wakakimbilia kumpa Uenyekiti Mrema.

  Ni kutokana na mfumo wa Kikomunisti wa vyama kuona kuwa Mwenyekiti wa Chama ndio mwenye mamlaka ya mwisho na vyama hivi kujiendesha kwa kumpa Mwenyekiti mamlaka makubwa (mfumo wa Ki-CCM), ndio maana kila mtu anaamini kuwa ni lazima awe Mwenyekiti wa Chama kwa kuwa uanasogea karibu na nafasi ya kugombea Urais na kuwa Rais.

  Hii ilitokana na marekebosho ya Katiba ya CCM ya kofia mbili, wakati Nyerere alipoamua kuacha Uenyekiti 1987, kutokana na mgongano wa nguvu za Utendaji ambapo Urais na Serikali zilionekana kuwa dhaifu kwa Chama hasa kutokana na Chama kuwa na Mwenyekiti ambaye hakuwa Rais na Serikali ilikuwa ikifanyha kazi kwa ridhaa ya Chama.

  Kama Mrema angekaa chini na kuchukua mateka hasa ya viongozi kutoka CCM, basi leo hii tungekuwa tunacheza sindimba nyingine!
   
 15. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #15
  Sep 13, 2009
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 8,253
  Likes Received: 4,276
  Trophy Points: 280
  Mkuu hii haijakaa vizuri, yaani unamaanisha kwamba ukiwa mbunge ndio unakuwa umemaliza matatizo yako binafsi?

  Hii hali ndio watu wengine tunaikataa.
   
 16. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #16
  Sep 13, 2009
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,583
  Likes Received: 1,944
  Trophy Points: 280
  Rev. Unachosema ni kweli ila tatizo kubwa kwa Mrema na CHADEMA kwa maoni yangu binafsi ni Mh P. Ndesamburo, ambaye yeye na Mrema haziivi kabisa. Kumwekea masharti aliyowekewa kabla ya kujiunga na CHADEMA lazima kulikuwa na shinikizo kutoka kwa wadau wa ndani na wenye sauti wa CHADEMA na kwa wakati ule kabla hata Mrema hajajitoa CCM yeye na Ndesamburo walikuwa ni kama paka na panya...Yani sioni ni kwa kivipi Mzee Ndesamburo angekubali Mrema awe mwenyekiti,hata kama angeambiwa huyu ni masiya asingekubali.
   
 17. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #17
  Sep 13, 2009
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 8,253
  Likes Received: 4,276
  Trophy Points: 280
  Mkuu,

  Lakini Mrema si nae alikuwa mwalimu wa hawahawa wana usalama pale Mbweni au labda namchanganya!

  Hapa namaanisha kwamba makablasha mengi ambayo huyu mheshimiwa alikuwa anapata yanayohusu ufisadi kwa wakti ule si alikuwa akipewa na baadhi ya wanafunzi wake wa zamani?

  All in all Mrema alipaswa kuunda chama kipya kabisa ambacho kingekuwa na watu wasiohusiana na mfumo wa siasa uliopo jambo ambalo kwa Tanzania ya sasa ni vigumu sana kwasababu mfumo wa siasa wa Tanzania au "political establishment" umekaa vibaya kwa upinzani.
   
 18. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #18
  Sep 13, 2009
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Jamani hata mm namfikiria sana huyu mzee wa watu. Kwanza alipokuja na rushwa ya milioni 900 wakamtemgenezea wingu zito watu wakamuona kama kichaa na hana uwezo hadi na yeye akaamini kwamba kweli hana akili na anachosimamia si cha kweli. Jamani hii ni hatari sana. Lakini hebu angalieni jinsi Mrema alivyopambana na ufisadi kwa dhati.
   
 19. Kafara

  Kafara JF-Expert Member

  #19
  Sep 13, 2009
  Joined: Feb 17, 2007
  Messages: 1,392
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  hapo ndipo najiuliza je ni ubinafsi au ni nia madhubuti ya kutaka kuongoza mapambano ndio ulipelekea mrema kudai uenyekiti wa chama chochote alichojiunga baada ya kutoka ccm ?
   
 20. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #20
  Sep 13, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Ni vyote viwili Ubinafsi na nia madhubuti.

  Ni Ubinafsi (he took it personally with the actions of CCM and Mwinyi's Government) kwa kuwa alikuwa na nia ya kuwaonyesha kuwa anaweza kufanya mambo kwa ubora kuliko wao alioachanana nao, ikiwa ni kiunganishi kwa dhamira ya umadhubuti wa kuongoza mapambano.

  Vitendo vya Mrema, vinatoa sura mbili ambazo zinashabihiana mno.
   
Loading...