Augustine Lyatonga Mrema: Mpiganaji!

This mada iz too past oriented, ila mrema anajua afanyacho. Juz kati nilienda bush. Kule kampeni zimechemka si kitoto, na mwakani anachukua ubunge. Bara2 kaipiga greda kitu ambacho mh. Kimaro hakuwahi kufikiria

Huu ndio uongozi mnaouenzi? Kupewa badala ya kuonyeshwa na kuongozwa ili mjitegemee! Kweli wananchi wote hapo mnashindwa kweli kupiga greda barabara mpaka mfadhili awafanyie? Mnataka kiongozi au mfadhili?

Kwa mtaji huu, ufisadi kweli utaisha nchini?

Amandla.......
 
Interested Observer,

..Waziri Mkuu ni msimamizi wa shughuli za kila siku za serikali, pamoja na 'kiranja mkuu' wa baraza la mawaziri.

..kama unataka kupima utendaji wa Mawaziri Wakuu, basi unapaswa kuangalia achievements za serikali walizoziongoza pamoja, na ufanisi wa mawaziri waliowasimamia.

..nadhani Waziri Mkuu Sinde Warioba aliteuliwa wakati nchi ikiwa ktk matatizo makubwa sana ya kiuchumi na ukata wa kifedha. wakati anaondoka kulikuwa na tofauti kubwa sana kulinganisha na wakati anateuliwa.

..Sinde Warioba hakuwa mtu wa kujitangaza-tangaza na ndiyo maana Watanzania leo hii hawa-appreciate rekodi yake ya utumishi.

..kwa upande wangu Sokoine alikuwa Waziri Mkuu mzuri ktk kipindi chake cha kwanza, na siyo kile cha pili. katika kipindi cha kwanza hali ya uchumi ilikuwa nzuri, pia aliweza kutuvusha ktk kipindi kigumu cha vita vya Kagera. katika awamu yake ya pili, mpaka alipofikwa na mauti, ilikuwa ni crisis management tuu.
 
Jmushi1:

Sikatahi kama kuna moral obligations. Lakini kusubiri kupata Kiongozi mwenye Moral obligations ni sawa na kucheza bahati nasibu. And the chances are you won't get one.

Kwa mfano ukichukua Buzwagi, EPA, Richmond ni vitu ambavyo vingeweza kufanyika kwa ufanisi zaidi bila kujali moral obligations za wahusika iwapo tu taratibu za kutangaza tenda, account na procurements zingekuwa transparent.

Vilevile ukumbuke masuala ya moral obligations ni personal level. Masuala ya personal level hayarithishwi kwa vizazi vinavyokuja. Na kama yanarithishwa basi watanzania wengi wangerith moral values za mwalimu Nyerere na nchi yetu ingekuwa mswanu.

Wengine mashuleni tulifundishwa siasa kuanzia darasa la tatu mpaka Chuo. Tulikwenda majeshi lakini tuyatendao hayafanani na mafunzo yetu.

Hivyo short cut ni kuchungana tu. Kwa mfano rais akiteua mtu kuwa waziri, basi bunge limpigie kura. Ardhi inayokuwa alocated kwa investment kama uchimbaji wa madini au mbuga zipitishwe na bunge.

Vitu hivi sio rocket sayansi na moral obligation iwe extra credit.

Mkuu moral obligations kuwa possible ni only if there is accountability...Na the accounts of accountability also differs,mwalimu prefered kuwahamishia wizara nyingine watendaji wabovu,alikuwa akihamishia matatizo kutoka hapa kwenda kule na kamwe si ku eliminate matatizo hayo ama to trully hold them accountable...Ikawa kama culture yetu watanzania.Na ndio maana nikatoa mfano wa China...Nilimaanisha kuwa ili ku enforce moral obligations ni lazima kuwe na accountability inayoendana na seriouseness ya matter yenyewe kutegemeana na priorities zetu kama Taifa....Ufisadi ni uhujumu wa maisha na uhai wa mtanzania na kwa hivyo penalty zake ni budi ziendane na consequences zake ama impact zake kwenye jamii.....Utaweka taratibu zote utaremba sijui nani afanye nini,if there isnt accountability bado udanganyika utaendelea kuwa sifa kubwa na jina stahiki.
 
Inawezekana nina-compliment kile unachosema au una-compliment kile nachosema.

Either way, ku-enforce moral obligations hakuji bila kuwa na system inayoeleweka, yenye sifa za kufanya kile kinachotarajiwa na kukubalika.
 
Tunaweza kuwa na system yenye sifa hizo lakini kile kinachotarajiwa na kukubalika kisifanyike,hapo ndipo umuhimu wa accountability unapojitokeza.
 
Mtu yeyote afanyaye kitu tofauti na wengine. Why can I say Sokoine was a better Prime Minister than John Malecela? My question is better if asked this way: Why Sokoine and Mrema as Prime Minister and Deputy Prime Minister respectively had impact on most [most not all]Tanzanians? My answer I have, what about your opinion?

- Hapana mkuu swali lako lingekua better ungeuliza kwa nini Ben Ndulu ni gavana better kuliko Balali, na kwa nini Balali alikimbia bila kufukuzwa nchi, au? Bwa! ha! ha!

- U-better wa Sokoine ni upi huo mkuu wa kukamata wauza sabuni za kuogea mtaani na kuwaacha mafisadi wakizidi afadhali hata Mrema kidogo, eti utamlinganisha Mrema na Sokoine? Kwani hawa mafisadi wa sasa walitokea wapi? Au unasema walizaliwa baada ya Sokoine kutangulia kwenye haki?

- Kama walikuwepo akiwa waziri mkuu aliwafanya nini hasa mkuu? Angalau Mrema, alikuwa anafukuza malaya mitaani mjini Dar! By the way kwa nini Balali alikimbia nchi bila kufukuzwa?

Respect.

FMEs!
 
Kwa maoni yangu binafsi cheo cha naibu waziri mkuu ni cheo ambacho hakiitaji kufafanuliwa kikatiba. Ni cheo kinachotumika kuonyesha seniority katika kabinet.

.

- Ukiona kiongozi yoyote duniani sio Tanzania peke yake, anakubali kupokea cheo kisichotambulika kisheria na serikali yake, basi ujue ana matatizo makubwa sana, either yeye au wanaompa,

- Tunajua kilichowagombanisha Sokoine na Mwalimu, mpaka Sokoine kujiuzulu ni pale tu alipogundua kua hakuwa na power yoyote ya ku-deal wezi wakubwa hasa mawaziri, ili kuwashika alihitaji okay ya Mwalimu, Sokoine akaona ni ujuha kuendelea na ile nafasi,

Eti was this the case na Mrema? Alijiuzulu unaibu waziri mkuu kwa sababu kama hizi za Sokoine?

Repect.

FMEs!
 
Zakumi,Rev.Kishoka,

NB:

1. ..Katiba yetu imefafanua Waziri Mkuu, Waziri, Naibu Waziri, Waziri wa Nchi. Katiba haijafafanua nafasi ya Waziri Mkuu.

2. ..TATIZO SI MREMA KUTEULIWA KUWA 'NAIBU WAZIRI MKUU.'

3. TATIZO NI MREMA KUSHANGAZWA NA KUCHUKIZWA NA MWANASHERIA MKUU ALIYEMWELEKEZA KWAMBA NAFASI HIYO HAIPO KIKATIBA NA HAITAMBULIWI KISHERIA.

.

- Mkuu pale juu ulitaka kusema haijafafanua nafasi ya naibu waziri mkuu au?

- Tanzania hatuna nafasi ya naibu waziri mkuu, sasa any suggestion ya kupewa hiyo nafasi ni ufisadi, either kwa watoaji au kwa mpokeaji, ingawa honestly the burden fall on mpokeaji, maana sidhani kama kuna utumwa wa mawazo unaozidi huu!

- Hivi kweli jiulizeni one question, wewe unapompa kiongozi nafasi ambayo haina katiba kwenye jamhuri, unamuangaliaje huyu kiongozi kama Mrema anayeipokea na kufurahi kama vile ni mazuri sana hayo?

- Sasa ona mwanasheria wa serikali alivyokuja kumuabisha kwamba cheo chako hakipo kwenye katiba, huoni kwamba hii ni aibu ya mwaka kwa a man mnayesema ni good enough kuwa rais wa sasa?

Respect.

FMEs!
 
- Mchungaji sikai Marekani, na ni makosa makubwa sana ku-speculate location ya another member kwa sheria za JF, nikitaka kusema ninakoishi niache niseme mwenyewe,

- Si nilikuambia hua mnaanza wenyewe ya kunitafuta personal halafu nikijibu on the personal level hampendi, kwani Mchungaji hoja yako isingeeleweka bila ku-speculate my location?

- Ni lini umewahi kuniona niki-speculate location yako au ya member yoyote hapa mkuu? Unahitaji ku-apologize for this maana ni too low and uncalled for! I mean kwa nini siwezi kujadili hoja humu JF bila hizi lows za personal?

FMEs!

FMES

Imebidi nirudi tena na kukisema ulichodai ni ukiukwaji wa kanuni za JF.

Kama ni kuvunja Protocols za ID za watu, mbona uliamua kusema kuwa nina mahusiano na Mtu aliyekuwa BOT, je hiyo si kuvunja kanuni au kanuni za JF zinapiga vita kutaja mtu yuko wapi, bali kusema ya ndugu na familia ya mwana JF ni ruksa?

Na si mimi pekee ambaye umediriki kutoa habari binafsi ukumbini humu, Umemtuhumu Waboyerwa kuwa ni ndugu wa Jamaa wa Meremeta, je hiyo ni sawa?

So you also owe me an apology!
 
Tunaweza kuwa na system yenye sifa hizo lakini kile kinachotarajiwa na kukubalika kisifanyike,hapo ndipo umuhimu wa accountability unapojitokeza.

Jmushi1:-

Niko na wewe. Hila tusitumbukie tu kwenye mjadala wa kuku na mayai kipi ni cha kwanza.

Ndani ya thread hii, Rev. Kishoka aliuliza items nne ambazo ni mapungufu ya political system yetu.

Ukiweza kuzipata hizo nne kwa kutumia misamihati yako mwenyewe na kuzi-apply katika political system ya sasa, accountability itajitokeza.
 
Zakumi,

..umeongelea suala la kuwa na checks and balance na hilo tumekubaliana kwamba ni muhimu.

..sasa mimi nimeanza kujiuliza kama hizi checks and balance zilizopo sasa hivi, hata kama ni very weak, je tunazitumia ipasavyo.

..binafsi nadhani tutaendelea na umasikini wetu ikiwa wapiga kura wataendelea kudanganyika na viongozi wa aina ya Mrema.

..zaidi wananchi inaelekea kwamba tumeukataa 'ufisadi', wakati umasikini tunaukumbatia. kwa Tanzania kiongozi anayepiga makelele ya 'ufisadi' anakubalika zaidi kuliko kiongozi anayejishughulisha kutatua masuala kama ya elimu, afya, miundombinu, mazingira etc etc.
 
Zakumi umesema hapo mwanzo kuwa system ikawa nzuri na fisadi kuwa malaika ndio matarajio...Nikasema kama matarajio hayo yasipokuwa realised basi aacountability iwepo,jambo ambalo limekuwa tatizo sugu kwenye kuresolve matatizo yetu...Collective responsibility ndiyo ilireplace accountability wakati Mrema alipoazimu kujitoa kutoka kwenye baraza la mawaziri kama unakumbuka.
 
Je kuna namna yoyote ya kumjenga, kumrudisha na hatimaye kumpata Mrema kama mgombea wa Urais mwakani?
Mzee watu mwacheni apumzike na umri ule aanze kuzunguka nchi nzima kufanya kampeni? nafikiri swali lingekua je tunao watanzania wengine wenye sifa kama za Mrema wanoweza kutuongoza?
 
Zakumi,

..umeongelea suala la kuwa na checks and balance na hilo tumekubaliana kwamba ni muhimu.

..sasa mimi nimeanza kujiuliza kama hizi checks and balance zilizopo sasa hivi, hata kama ni very weak, je tunazitumia ipasavyo.

..binafsi nadhani tutaendelea na umasikini wetu ikiwa wapiga kura wataendelea kudanganyika na viongozi wa aina ya Mrema.

..zaidi wananchi inaelekea kwamba tumeukataa 'ufisadi', wakati umasikini tunaukumbatia. kwa Tanzania kiongozi anayepiga makelele ya 'ufisadi' anakubalika zaidi kuliko kiongozi anayejishughulisha kutatua masuala kama ya elimu, afya, miundombinu, mazingira etc etc.

Jokakuu:

Wakati wa chama kimoja ni watanzania wa kawaida waliopiga kura za kuchagua wabunge. Na vipindi vya bunge wakati ule vilikuwa bora kuliko vya sasa.

Pamoja na umasikini wao wa Tanzania wanaweza kuchagua wabunge wazuri ambao watahakikisha check and balance.

Matatizo yanayokuja ni kuwa wapiga kura wanapelekewa majina ambayo yamepitishwa na vikao vya vyama vya kisiasa. Frankly speaking, kama Kikwete alivyoteuliwa na chama chake, wagombea wengi wa CCM katika ngazi za ubunge wanapitishwa hivyo.

Siku hizi mbunge wowote wa CCM akiboronga, utasikia uongozi wa umoja wa vijana katika wilaya wanakuja juu kuwa mbunge wao ni babu kubwa. Wanafanya CCM kuwa ni biashara.

Hivyo hatuwezi kuwa na check and balance wakati process za kuwachagua watu watakaosimama muundo huo zinakiukwa.

CCM na vyama vingine wanatakiwa kutafuta njia za kuhakikisha kuwa jinsi ya wanavyopatikana wagombea wao wa ngazi zote ni fair.
 
Zakumi umesema hapo mwanzo kuwa system ikawa nzuri na fisadi kuwa malaika ndio matarajio...Nikasema kama matarajio hayo yasipokuwa realised basi aacountability iwepo,jambo ambalo limekuwa tatizo sugu kwenye kuresolve matatizo yetu...Collective responsibility ndiyo ilireplace accountability wakati Mrema alipoazimu kujitoa kutoka kwenye baraza la mawaziri kama unakumbuka.

Jmush1:-

Nchi zetu zingine ni petty project za maendeleo ya World Bank, IMF na nchi zilizoendelea.

Nadhani wangetunyima misaada labda tutachapana bakora na kuweka mfumo wa kuheshimiana na kuheshimu sheria.

Sheria za nchi zinapovunjwa au kukiukwa, baraza la mawaziri halitakiwi kuchukua collective responsibility. Hivi ni vitu tunavyotakiwa kuvikataa. Lakini sometimes hata hapa JF watu wanavishabikia.
 
Je kuna namna yoyote ya kumjenga, kumrudisha na hatimaye kumpata Mrema kama mgombea wa Urais mwakani?

Mzee Mwanakijiji,

Mzee Mwanakijiji umenikumbusha mbali sana, naikumbuka ile Picha tulio piga na mzee wetu Mrema 1995, nakumbuka jinsi tulivyokuwa tukihisi kufanya mabadiriko ya kweli, Oooooo!!! my God.

Sawa siku zile nilimkubali sana Mzee yule na hata sasa ninaendelea kumkumbuka sana kwani yeye ndiye aliyechochea mageuzi hapa Tanzania.

Mwenyezi Mungu amnusuru mzee wetu Mrema kwa magonjwa yanayomuandama kila kukicha.
 
Back
Top Bottom