august 1,mwisho wa vipanya (hiace)!!!

Mtaalam

JF-Expert Member
Oct 1, 2007
1,371
250
as tulivyosikia wajimini kuanzia siku hiyo ya ijumaa ya august 1 hamna ruhusa kwa vipanya kutoa huduma jijini kwa ajili ya kupunguza msongamano wa magari jijini,

je is it the right njia mbadala kupunguza msongamano huo??
wil it solve the problem?
and what about shida ya usafiri wa wananchi maana hata sasa vikiwepo tu bado kuna watu mida ya kazi hukaa vituoni mpaka miguu yataka ingia tumboni je vipanya vikipungua itakuaje??!do we have enough mabasi ya zaidi ya abiria 25???

na wale woote wanaomiliki vipanya wafanye navyo nini?or in other words vipanya vyoooote vilivyoko jijini viende wapi na kufanya kazi gani?
 

as tulivyosikia wajimini
kuanzia siku hiyo ya ijumaa ya august 1 hamna ruhusa kwa vipanya kutoa huduma jijini kwa ajili ya kupunguza msongamano wa magari jijini...

Wengine hatujasikia. Naomba chanzo cha habari tafadhali!
 
ehh we uko dunia ya wapi??!!m sure haupo bongo cz if ur there n hujui wakati sie wa huku madongo kuinama twajua......

anyways nipe muda kidogo na refer tena source yangu ya nfo na nitaiweka soon
 
MAMLAKA ya Udhibiti wa Uthibitiwa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini nchini (Sumatra) imesema kuwa kuanzia Agosti Mosi, mwaka huu mabasi ndogo yanayobeba abiri chini ya 25, maarufu kama 'vipanya', hayataruhusiwa kutoa huduma jijini Dar es salaam.

Kwa mujibu wa Sumatra, mabasi yanayota usafiri jijini Dar es Salaam (daladala), yatakayoruhusiwa ni yale yanabeba abiria zaidi ya 25 ili kupungunguza msongamano wa magari jijini.

Sambamba na hatua hiyo, Sumatra imeagiza kuwa mabasi yatayasajiliwa kutoa huduma hizo lazima yawe mapya au yaliyotumika si zaidi ya miaka mitano tangu yalipotengezwa, kwa lengo la kulinda usalama wa wasafiri na kupunguza ajali.

Katika kuboresha na kudhibiti usafiri jijini, mamlaka hiyo pia imesema daldala zitakazopewa leseini, wamailikiwa wake watalazimika kuunda kampuni ambazo ndizo zitajulikana kisheria kuwa ndizo zinazotoa huduma hiyo jijini badala ya kila mtu kuwa na basi lake kama ilivyo sasa.

Licha ya agizo hilo kutokuwa jipya, tunaipongeza Sumatra kwa kuweka tarehe maalumu ya kuanza kuteleza ilichokuwa ikisema kwa zaidi ya mwaka mmoja uliopita, kama kweli wamedhamira kufanya hivyo na kuhakikisha kuwa walichopanga kinatekelezwa.

Lego la kuhibiti msongamano wa magari jijini ni hatua muhimu katika jijini la Dar es Salaam kwa sasa, kutokana na kuongezeka kwa magari katika barabara nyembamba zilizojengwa miaka mingi iliyopita.

Ni dhahiri kwamba, kuwepo kwa vipanya jijini, licha ya kuawasidia wananchi, vimekuwa vikisabisha msongamano wa magari usio wa lazima kutokana na wingi, pamoja na mchezo mbaya wa madereva kutumia njia za mkato kuyapita magari mengine (kuchomekea).

Si hivyo tu, hatua ya kuwataka wamailiki wa daladala kuungana na kuunda kamapuni za usafirishaji, inasaidai kudhibiti vitendo vya ukiukwaji wa sheria za barabarani na utovu wa nidhamu unaofanywa na baadhi ya madereva na makondakta wa daladala dhidi ya wasafiri na hasa wanafunzi.

Kuna baada madereva ambao wanasababisha ajali kwa makusudi, kutokana na tabia zao za kuchomekea na wengine kuwanyanyasa na kuwadhalilisha abiria, kisha hukimbia namabasi yao.

Hivyo tunaamini kuwa mabasi hayo yakisajailiwa chini ya kampuni vitendo hivyo, vitakuwa rahisi na usafiri utapatikana kwa urahisi na hadhi inayotakiwa, kama ilivyo katika nyingi duniani.

Tunaamini kuwa kama usafiri wa daladala utaimarishwa na kufikia viwango bora, watu wengi na hata wanaomiliki magari madogo watalazimika kutumia usafiri huo, ili kupunguza msongamano zaidi jijini, kwa sababu mazingira hayo yanaweza kuwezesha kuwepo kwa mabasi makubwa yaendayo kasi.

Hata hivyo tunaishauri Sumatra ihakikishe kwamba hatua hiyo inaanza kufanya kazi kukiwa na mabasi ya kutosha, ili sije ikasababisha kero kubwa kwa wananchi na wanaafunzi wanaokwenda kazini na shukeni.

Pamoja na hayo, tunaomba kuanzia sasa Sumatra na mamlaka zote zinazohusika yafanyike maandalizi ya kutosha kabla ya kuanza utekelezi wa amri hiyo kwa haki na kutoa upendeleo kwa baadhi ya wamiliki a mambasi hiyo.
 
hiyo nimecopy habari ya mwananchi gazeti la leo june 17...
waweza tafuta magazeti yafuatayo...yana hiyo habari pia
daily news ya june 17
 
nyingine hiyooo

Vipanya marufuku katikati ya jiji Agosti 1
2008-06-17 15:30:49
Na ITV Habari


Mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa nchi kavu na majini-SUMATRA umewataka wamiliki wa mabasi yanayofanya safari zake katika jiji la Dar es Salaam kuhakikisha hawaagizi magari aina ya vipanya kwani hayataruhusiwa kutoa huduma zake katikati ya jiji kuanzia tarehe moja mwezi wa nane kutokana na kuanza kwa mradi wa mabasi yaendayo kasi.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi mkuu wa SUMATRA Bw. Israel Sekirasa kwenye mkutano na wadau wa sekta ya usafiri kujadili mapendekezo ya kupanda kwa nauli za usafiri wa daladala ambapo amesema chini ya kanuni mpya.

Mapema mwenyekiti wa chama cha wamiliki wa mabasi ya daladala DARCOBOA Bwana Sabri Mabruki amesema kuwa kimsingi serikali inatakiwa kujipanga upya katika suala la kuboresha usafiri wa daladala nchini kwa kuhakikisha inawawezesha wamiliki kuagiza magari ambayo hayajapita muda wake ili kuepusha ajali.
 
Sio rahisi kama unavyofikiri, mwabula alijaribu akashindwa unafikiri SUMATRA wataweza wapi wakati hata wanaokatiza ruti hawawezi kuwadhibiti, vipanya vinamilikiwa na vigogo na hawako tayari kuvilaza chini na kuingia hasara, hakuna utekelezaji utakaofanyika.

hachilia mbali kumikiwa na vigogo wameandaa utaratibu gani wa kuingiza magari ya kuchukua nafasi ya vipanya kama wanavisimamisha, maneno matupu hapo subiri hiyo august 1 uone.
 
Asafadhali maana vilikuwa vinachafua jiji!ila sasa usafiri watu si ndio itakuwa kasheshe!Hivi jamani serikali inashindwa kununua mabasi yake kukawa na usafiri wa umma?Wizara ya miundo miundo mbinu vipi mbona hamko creative?
 
tena tetenus nje nje ila ... huu utakuwa mradi wa mnene ... wawajali wanafunzi kwanza maana wanataabika ...
 
Sasa mbona hii habari inapingana na ile ambayo imepostiwa na BMO, ya kwake inadai kwamba vipanya havitaruhusiwa kuingia city centre na hii hapa inasema kwamba ni total ban kwenye jiji la Dar, which is which? So confusing.
 
hata wenyewe hawaelewekii i think this is somethin for one of the vigogoz....lazima kuna mnene yuko behind everything!!!lets wait n see hiyo august moja ikifka!!wajimini anzeni kununua baiskeli hukooo u wont hav to think abt mafuta prices,daladala zipo au hazipo,zikiwepo nauli bei gani wala nini
 
kweli KKN,

Bali nielewavyo mimi ni kuzuiliwa kuingia city center kuepusha msongamano ingawa sina uhakika sana kuwa vipanya ndivyo husababisha. But SUMATRA wapoamua kuzuia hao panya kuingia city center ni budi wawe wamejiandaa na njia mbadala sio kuja kusababishia usumbufu kwa wana-Dar wengi wanaotumia panya.

Kudai kuwa mabasi makubwa tu ndio yaruhusiwe kuingia katikati ya jiji lazima wawe wamefanya utafiti wa kina kama hayo yatakuwepo na kukidhi haja ukizingatia city center inameza watu kibao..

Lakini mh!! hao wanene wa SUMATRA kweli na wao hawana vipanya vyao au ndio wanataka mabasi yao makubwa yafanye kazi??? Teh! teh! tehtehteh!!!!! This is bongo bwana....
 
Its a good idea, dont get me wrong kwa kuwa hata mimi si mshabiki mkubwa wa vipanya na nilikuwa nakerwa sana na uwepo wake katikati ya jiji, ila ninachohofia hapa ni kwamba huu uamuzi umefanywa kwa kukurupuka, sidhani kama kuanzi sasa hadi hiyo August mosi kutakuwa na mabasi makubwa ya kutosha kureplace hivyo vipanya, and as usual atakaeteseka na maamuzi haya ni mlalahoi.
 
Mkuu kana ka nsungu,unafahamu jiji la dar linaanzia wapi na kuishi wapi?
 
nice qn malila watuambie jijini wanamaanisha wapi hadi wapi kwanza tujue...
and je wamejiandaa kwa hayo mabasi makubwa ya kutosha kuwahudumia watu woote??maana now yenyewe tu with the vipanyaz na mabasi makubwa bado tu usafiri ni kero na shida tupu sasa minus the vipanyaz si ndo itakua balaa
 
Once again it can be proven how our leaders are reactive rather than proactive.This shows that there was no indepth analysis and planning on how best to solve the problem of public transport.

No wonder the dream of most walala hoi has become buying a car,hata kama anakaa nyumba ya kupanga! This has led also to the long car ques we have now which makes driving a car almost unbreable and with the rise of fuel prices makes it even worse.

It is not wrong to ban the vipanya unless they have a solid plan and way of introducing the best alternative to this problem.There are some defining questions that need to be answered such as do we have the infrastructure to support the alternative to the vipanya???
 
Back
Top Bottom