Maudhui nzuri kama hii
Baada ya mda kidogo bila kuingiza neno humu jukwaani. Leo nimerudi kidogo.
Mleta mada unaushauri upi wa zanzibar kurudi kwa warabu? si ndio wakoloni wao. Najua hili swali litawaumiza wale wapenda wazungu...
Oke, turudi kwenye mada, swali lengine dogo tu, nini maana ya colony?
Nimesoma humu kwa wachangiaji wengi, duu aise kiukweli nimehuzunika sana, kwa watu wanaotetea ujinga kama huu.
Moja ya uchambuzi wao ni hii si walijenga nchi, walipanga miji, na walitujengea kiwanda hiki na kile na na...
Sasa, hivyo vyoote walivyovijenga vilikua na sababu zake, kwanzia treni na sehemu walizokua wameweka kambi, mfano sehemu kama tanga, lushoto, dar na kadha....
Moja ya sababu ni kuharakisha kwa usafirishaji wa mahitaji waliyokuwa wanayahitaji enzi hizo, mahitaji ya raw material mfano wa hizo kahawa, cotoni, na kadha.... walizokua wanazizalisha bure au kwa kiasi kidogo cha pesa kwa kuwatumia wenyeji kuwafanyiza kazi hizo. Hawakuwa katu, na imani ya kuwasaidia wenyeji.
Na sehemu nyingi walizokuwa wamezijenga ni zile sehemu walizokuwa wanazihitaji. Na kuongeza kidogo, vitu walivyotoa ni kidogo ukifananisha na vitu walivyovichukua.
Nyongeza nyingine, moja ya kitu wazungu hawapendi kuona ni nchi nyingine ya kimaskini au ya kiafrika inaendelea, wengi humu kwenye jukwaa hawajui kwamba hiyo hoja ya wakimbizi kwenda ulaya haina mshiko kivipi ?
Kama libya enzi za marehemu Muammar, ilikuwa ni nchi iliyoshamiri maendeleo ya kila namna, lakini hao hao wazungu ndio walikua mlango wa mbele kumpiga kwa kuwa hawakuwa wanampenda, daah kumbe walikuwa hawajui kuwa wanaufungua mlango uliokuwa umefungwa na marehemu Gadafi. Na kiasi kikubwa cha watu wanaokimbilia ulaya kupitia libya si walibya bali ni ndugu zetu kutoka naijeria, ethiopia na kadha.... Walibya ni wasimamizi tu wa kuhakikisha ndugu zetu wanapanda boti salama kwenda huko kwenye democrasia na maendeleo ili na wao waonje ladha ya matunda ya democrasia ya wazungu. Kwa hili ningeshauri serikali pendwa ya Tanzania kama ikiwakamata ndugu zetu kutoka ethiopia wakikimbilia SA badala ya kuwafunga na kupata hasara za matumizi, ingewasafirisha mpaka libya ili wapande boti waende kula matunda ya democrasia saafi. Ili na sisi wajukuu wetu wakikuwa wakubwa wakienda ulaya wajihisi kama wako nyumbani.
Koloni lolote lilikuwa linachukua mali kwa nguvu, tena mali yote, bila mkataba.
Wasalam.