Atorokea Kenya na hela ya mchango wa harusi yake

Atorokea Kenya na hela ya mchango wa harusi yake

Habari wadau,

Bwana harusi mmoja hapa mtaani kwetu kaacha bumbuwazi baada ya kutoroka na fedha za harusi yake takribani milioni 26..

Kuna madai kwamba deal hili lilichongwa mapema yeye na mkewe mtarajiwa ambao waliamua kutotumia michango yao kufanya sherehe na badala yake wakaamua kutimkia nchini Kenya kufanya biznez..

Wanakamati wanamsaka na RB.
Hivi polisi wanaweza kutoa RB kwa issue kama hii? michango si ni hiari? Pili hiyo kamati ni vilaza, why hawakutunza hizo pesa? hawakuwa na mhasibu?
 
Niende Kenya kufanya nini...nchi kubwa hii,ningeingia porini huko naenda kulima.. baada ya miaka mi 5 najitokeza nawarudishia hiyo millioni 26 yao.

Ngoja huko Kenya akafilisike sijui atarudi vipi
 
Safi sana maana zingeishia watu kupiga pombe halafu mkapewa zawadi ya milioni
 
Hawa maharusi ni mashujaa katita jamii. Tehee tehee ..watu walishanunua misuti na kushona Vitenge, Kama nawaona walivyojaa jazba mpaka kuchukua RB. Hapo Unakuta hao wanakamati waliochukua hiyo RB humo humo kuna mtu wa mapambo...kuna mtu wa chakula na vinywaji. Wote walikuwa tayari kupiga dili.
 
Nijuavyo bwana harusi mtarajiwa hakao na michango ya harusi bali suala hilo linakuwa mikononi mwa kamati ya harusi ambayo mweka hazina pia hawezi kuwa bwana harusi mtarajiwa.
 
Kwani hizo pesa walikabidhiwa wao maharusi? Mana najua kamati ndiyo zinakaa na hela kwa ajili ya kufanikisha hilo swala.....au mweka hazina alikuwa bwana harusi.?
Harusi yangu kulikuwa na mweka hazina, lakini alikuwa anaweka kwenye akaunt yangu ya benki. Ilikuwa kupimana imani kwelikweli, lakini nashukuru mpaka siku ya kuvunja kamati waliniachia 4.1m. Hata hivyo nilikuwa nshaitumia kama 2m
 
Waweke kumbukumbu za wachangiaji vizuri baada ya miaka 5 warudi na kuwarudishia michango yao na kuwaomba msamaha.
 
Harusi yangu kulikuwa na mweka hazina, lakini alikuwa anaweka kwenye akaunt yangu ya benki. Ilikuwa kupimana imani kwelikweli, lakini nashukuru mpaka siku ya kuvunja kamati waliniachia 4.1m. Hata hivyo nilikuwa nshaitumia kama 2m
Okay lakini uaminifu ni jambo jema kuna leo na kesho unawezaje kuwarudia hao uliowafanyia uhuni na kuomba msaada wao incase ukihuihitaji tena.
 
Back
Top Bottom