Atorokea Kenya na hela ya mchango wa harusi yake

Interest

JF-Expert Member
Apr 11, 2015
3,434
7,067
Habari wadau,

Bwana harusi mmoja hapa mtaani kwetu kaacha bumbuwazi baada ya kutoroka na fedha za harusi yake takribani milioni 26..

Kuna madai kwamba deal hili lilichongwa mapema yeye na mkewe mtarajiwa ambao waliamua kutotumia michango yao kufanya sherehe na badala yake wakaamua kutimkia nchini Kenya kufanya biznez..

Wanakamati wanamsaka na RB.
 
yani hili wazo mm ninalo kitambo sana mana bi mkubwa keshawachangiaga sana watu ss itapofika zam ya mm kuowa km sijayeya na michango sijui

ss wanakamati wanamsaka wa nn,,wamchunia tuu jamaa kashajikomboa na kamtaji hahah
 
Kwani hizo pesa walikabidhiwa wao maharusi? Mana najua kamati ndiyo zinakaa na hela kwa ajili ya kufanikisha hilo swala.....au mweka hazina alikuwa bwana harusi.?
Siku hizi bwana harusi anaweza kuchagua mtu/au yeye mwenyewe kuwa mtunza fedha.
Wamefanya jambo jema sana, sherehe zinakaribisha umasikini tu. Waende wakajijenge maisha yaende!!
 
Siku hizi bwana harusi anaweza kuchagua mtu/au yeye mwenyewe kuwa mtunza fedha.
Wamefanya jambo jema sana, sherehe zinakaribisha umasikini tu. Waende wakajijenge maisha yaende!!
Ok basi mie nilikuwa mshamba wa taratibu za zamani......

Kutorola nazo si jambo jema wangesema ukweli.......ili kuendeleza ukaribu na watu waliojitoa kwa sababu zao. Sasa unadhani kwa manunguniko ya watu hiyo biashara itafanikiwa kweli?
 
Hakuna kesi hapo. hiyo kamati wanapaswa kumpongeza bwana harusi.
 
Habari wadau,

Bwana harusi mmoja hapa mtaani kwetu kaacha bumbuwazi baada ya kutoroka na fedha za harusi yake takribani milioni 26..

Kuna madai kwamba deal hili lilichongwa mapema yeye na mkewe mtarajiwa ambao waliamua kutotumia michango yao kufanya sherehe na badala yake wakaamua kutimkia nchini Kenya kufanya biznez..

Wanakamati wanamsaka na RB.
Kwani mtunza fedha alikuwa nani??
 
Back
Top Bottom