Atm za kuweka pesa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Atm za kuweka pesa

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Ami, Jul 19, 2010.

 1. Ami

  Ami JF-Expert Member

  #1
  Jul 19, 2010
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 1,858
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Leo nilikuwa kwenye foleni katika benki ya NBC,ilikuwa ni ndefu kweli kweli.Wakati niko kama watu 10 mbele yangu kufika kwa teller dada mmoja akajihisi vibaya mbele yangu.Ikabidi amuegemee mvulana wa kidato kama cha 4 hivi mbele yake.Yule mvulana akauliza vipi yule dada akasema nahisi kizungu zungu,hata hivyo yule mvulana alihisi pengine kapata na akanyamaza,hakuona haja ya kutoa tahadhari.Mara yule dada puuu!.
  Ikawa kizaa zaa mule ndani.Watu wa nbc wakaja kuokota pesa zake na sisi tukashauri wanawake wenzake wambebe kumrudisha nyuma nje ya foleni.Kabla yake kijana mwengine alikwishahisi kama hivyo na kurudi nyuma huku akiweka jiwe nafasi yake.Ilipotokea hivyo yeye akiwa ndiye wa mbele sasa akalaumu kwanini hawa jamaa hawaweki viti au mabenchi humu.Nikajisemea moyoni juzi si tulikuwa tukizungumzia suala hili hili!.
  Kwa upande mwengine nikajiuliza hizi mashine za kuwekea pesa ATM hapa kwetu ziko wapi na wapi?.Kwa sababu watu wengi sasa wameona umuhimu wa kutumia huduma za benki kwa usalama wa mali zao badala ya kutembea nazo mifukoni.Hivyo uwekaji nao inabidi uwe rahisi kiasi kwamba hakuna ulazima wa foleni ndefu katika mabenki.
   
 2. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #2
  Jul 19, 2010
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,071
  Likes Received: 4,006
  Trophy Points: 280
  yaani Tz kila kitu karaha hata fedha zako mwenyewe! Ila mashine za kuweka fedha kaka itakuwa ngumu kwa hali hii ya wahusika wa wizara ya fedha kupenda 10% katika uchapishaji wa fedha! Kama unakumbuka kipindi cha Mramba kuna hela zilichapwa na kabla ya hapo maelezo yalikuwa kemkem ati hela zitakuwa si rahisi kughushi mara ohoo kipofu ataweza tambua sijui nini sijui kile sijui hiki! zilipotoka Lahaula hata miezi miwili haikuchukua choka mbovu zimechakaa!
   
 3. RRONDO

  RRONDO JF-Expert Member

  #3
  Jul 19, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 25,856
  Likes Received: 20,892
  Trophy Points: 280
  mkuu....atm za kuweka hela ziko aina nyingi,nyingine wakati wa kuweka inatoa bahasha ambayo unajaza details zako na kiasi cha fedha then unaweka hela zako ndani ya bahasha kisha unatumbukiza bahasha kwenye mashine.huko ndani[bank] mtu anafanya process yote ya confirmation,tatizo la hii ni kuwa kama bank haina watu waaminifu kama wabongo wateja watadhulumiwa kwa kuambiwa waliweka hela pungufu au bandia.....mimi nishawahi kuweka hela kupitia hii mashine nikasahau sifuri moja yaani badala ya 300 nikaweka 30,bank walinipigia simu kuniuliza uliweka kiasi gani nikawaambia amount wakaniambia nilipokosea wakasort,sasa pata picha kosa hilo umefanya CRDB/NMB etc....
   
 4. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #4
  Jul 19, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  mashine za kuwekea pesa nchi za nje ndo hizo hizo atm za kuchukulia pesa........pia huduma nyengine kama kubadili pesa kuwa za kigeni, ku transfer money into an account in a different bank, kulipa bills kwenye account

  na kila kitu kinafanyika automatic.......

  Tanzania pia kunatakiwa hizo mashine za automatic, sio akae mtu ndani kupokea kibahasha. kwa kuanzia wanaweza kufanya mashine zilizoko sasa zikaweza pia kupokea pesa
   
 5. RRONDO

  RRONDO JF-Expert Member

  #5
  Jul 19, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 25,856
  Likes Received: 20,892
  Trophy Points: 280
  hakuna mtu anakaa kupokea bahasha yako.....hata hio atm kuna mtu huwa anaijaza hela,the same person ndio anachukua hela ulizodeposit na kupeleka kunakohusika.....
   
 6. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #6
  Jul 19, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  mie najua atm za kupokea na kuweka pesa ni automatic hakuna mtu wa kupokea wala kuweka ...........

  labda sikukuelewa hapo kwenye maandishi ya red na blue ..............fahamisha tafadhali
   
 7. RRONDO

  RRONDO JF-Expert Member

  #7
  Jul 19, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 25,856
  Likes Received: 20,892
  Trophy Points: 280
  ok......unaingiza card yako kwenye mashine.....enter your pin number.....select deposit.....enter amount..... inatoka bahasha.unaweka hela ndani ya bahasha na kujaza few details then seal ur envelope unatumbukiza kwenye mashine.get ur receipt.off you go.done.full automatic.

  what if nimeweka tsh5000 lkn nimejaza tsh 500,000?hapa ndio MTU ANAINGIA........hio ndio ninayotumia
   
 8. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #8
  Jul 19, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  anhaaa...................hiyo nchi uliyoko imenishangaza kwa kweli huo mfumo wao


  nizijuazo mimi ziko hivi sasa

  unaingiza cash card............select deposi.........una enter amount........ panafunguka ki-draw..... unaweka hela yako, mashine inazihesabu kabla hakijajifunga hicho ki-draw, inakuambia umeweka pesa sawa na uloandika if not inakwambia ingiza zaidi au anza mwanzo kama umekosea.
  ukimaliza hapo inatoka risiti ambayo inakwambia umeweka pesa ngapi na kwenye account therefore zimekuwa pesa ngapi.
  ukipenda una update kitabu chako unaondoka

  hakuna uwezekano wa kuandika pesa nyengine na ku deposit nyengine .....................hiyo ndo niliyo iita mimi full automatic
   
 9. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #9
  Jul 19, 2010
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,711
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  mashine zipo crdb ya azikiwe na ya millenium towers kijitonyama.
  unaweka kadi yako alafu unaweka hela zako kwenye mashine, zinajihesabu na risit unachukua huyooooooooo
   
 10. RRONDO

  RRONDO JF-Expert Member

  #10
  Jul 19, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 25,856
  Likes Received: 20,892
  Trophy Points: 280
  yeah....ila hii ni notorious kwa hela chafu/mbovu.....haifai bongo ndio maana nikatolea mfano wa hii......na benki huku hakuna foleni ya kutisha hivyo ni mara chache utatumia machine....na transaction nyingi ni juu kwa juu very rare cash transaction.
   
 11. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #11
  Jul 19, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Mkuu hizo ATM za kuweka pesa kwenye bahasha zipo. hizo ni toleo la mwanzo kabla hazijakuja hizi za kutumia kadi.
  Kwa msaada zaidi nenda pale Dar bara bara ya Bibi titi, jengo linalofuata baada ya Pegiote house (ukitokea Palm beach) .
  wapo jamaa wanaitwa NCR wanadeal na ATMs, waombe uzione, watakuonyesha na watakupa maelezo mazuri sana.
   
 12. kussy

  kussy JF-Expert Member

  #12
  Jul 19, 2010
  Joined: Jun 15, 2010
  Messages: 346
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  jamani mbona crdb wanazo? kwani zinatoa bahasha zile? ingawa mara nyingi hazifanya kazi
   
 13. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #13
  Jul 19, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Lol...haya mambo ya kuiga haya!! Hivi hizi ATM zimekuja lini Tanzania? Maana naona zinaleta mushkili sana kwa watu....
   
 14. Mgombezi

  Mgombezi JF-Expert Member

  #14
  Oct 12, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 630
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  ATM za kuweka fedha zipo BACKLAYS, mimi ndiyo njia ninayoitumia kuepuka foleni na hata usiku naweza kuweka fedha zangu benki. Unaingiza kadi yako. namba ya siri, kisha chagua huduma nyingine, halafu nyingine tena, utaona option ya kuweka pesa, chagua hiyo, halafu utatakiwa kuweka fedha zako (kuna sehemu inafunguka), machine iathesabu pesa na kuthibitisha idadi ya noti na kiasi, mwisho itaprint risiti.
   
Loading...