Athuman Maige, Mbunge wa Tabora Kaskazini aomba serikali ifanye utafiti mahususi kuhusu lugha ya kufundishia nchini Tanzania

Mbunge wa Tabora Kaskazini, Mh. Athuman Maige ameitaka serikali kufanya utafiti wa kina kuhusu lugha ya kufundishia nchini Tanzania. Mbunge huyo amesema "Ziko tafiti zaidi ya 40 zimefanyika na zote zinasema lugha inayofaa kufundishia Tanzania ni Kiswahili, naomba serikali ifanye tena utafiti mahususi kwa ajili ya lugha ya kufundishia kwa Tanzania,"

Aidha Mh. Maige ameongeza kwa kusema "Duniani kote hakuna nchi iliyoendelea kwa kutumia lugha ya watu wengine, Uingereza wanatumia kiingereza, Wachina kichina, lakini Tanzania tunatumia lugha ya kufundishia ni Kiingereza, watoto wanasoma Kiswahili darasa la kwanza hadi la 7,"

Kauli hii inakuja baada ya mjadala mkali unaoendelea kuhusu ipi ni lugha sahihi ya kufundishia nchini Tanzania ambapo baadhi ya wadau wakitaka jitihada zaidi iwekwe kwenye kuwafundisha watoto kiingereza huku wengine wakitaka lugha ya kufundishia ibadilishwe na kuwa kiswahili kwa ngazi zote kuanzia Shule za awali mpaka chuo kikuu huku lugha ya kiingereza ikifundishwa kama somo.
Hawa watu wa magharibi pamoja na kukaa kwao mwikulu miaka yoote huwa hawawanufaishi watu wao zaidi ya fitina na mambo ya hovyo hovyo, yule wa mpanda yeye aliambulia uwaziri mkuu, huyu yeye kazi yake kuchongea wazalendo wenzie
 
Mbunge wa Tabora Kaskazini, Mh. Athuman Maige ameitaka serikali kufanya utafiti wa kina kuhusu lugha ya kufundishia nchini Tanzania. Mbunge huyo amesema "Ziko tafiti zaidi ya 40 zimefanyika na zote zinasema lugha inayofaa kufundishia Tanzania ni Kiswahili, naomba serikali ifanye tena utafiti mahususi kwa ajili ya lugha ya kufundishia kwa Tanzania,"

Aidha Mh. Maige ameongeza kwa kusema "Duniani kote hakuna nchi iliyoendelea kwa kutumia lugha ya watu wengine, Uingereza wanatumia kiingereza, Wachina kichina, lakini Tanzania tunatumia lugha ya kufundishia ni Kiingereza, watoto wanasoma Kiswahili darasa la kwanza hadi la 7,"

Kauli hii inakuja baada ya mjadala mkali unaoendelea kuhusu ipi ni lugha sahihi ya kufundishia nchini Tanzania ambapo baadhi ya wadau wakitaka jitihada zaidi iwekwe kwenye kuwafundisha watoto kiingereza huku wengine wakitaka lugha ya kufundishia ibadilishwe na kuwa kiswahili kwa ngazi zote kuanzia Shule za awali mpaka chuo kikuu huku lugha ya kiingereza ikifundishwa kama somo.
Africa kuna nchi inafundishia lugha yake ya asili? Kwanza africa ki asili huwa hakuna lugha moja ndani ya nchi moja, kiasili waafrica huwa tuko kwenye makundi madogo madogo mfano tanzania tuna lugha 120, south africa wana lugha lasmi 10, ethiopia kidogo wameendelea na lugha yao rasmi, lakini kihistoria ethiopia haikuwahi tawaliwa, na ustaarabu wa kihabeshi ulianza miaka maelfuniliyopita, the rest tuko taabani
 
Wanaotaka kiswahili iwe lugha ya kufundishia toka shule ya msingi hadi chuo kikuu watoto wao wanasomesha kwenye shule zinazofundisha kwa lugha ya kiingereza.
Hawa watu ukiwasikiliza unaweza kusema wana nia njema lakini ukweli ni kwamba ndani ya mioyo yao si wenye dhamira njema hasa kwa watoto wa masikini, lengo lao kubwa ni kutaka familia zao ziendelee kutawala na kugawana vyeo huku watoto wa masikini wakiendelea kuwa watwana na vijakazi wao na kuendelea kuwaita yale majina ya kuwabeza kama "watu wetu"/"watu wangu", "wapiga kura wangu" nk.
Kama kweli serikali imedhamiria kufundisha kwa lugha ya kiswahili basi watoe kwanza lile sharti la kutaka wanaoomba baadhi ya ajira kama sio zote kwamba waombaji wajue kuzungumza na kuandika kwa ufasaha lugha ya kiingereza pia mawasiliano yote ya barua, email na njia nyingine za maandishi yafanyike kwa lugha ya kiswahili na miswada yote ipelekwe bungeni kwa lugha ya kiswahili vinginevyo hao wabunge na serikali wote ni wanafiki.

Back
Top Bottom