Athuman Maige, Mbunge wa Tabora Kaskazini aomba serikali ifanye utafiti mahususi kuhusu lugha ya kufundishia nchini Tanzania

Mzee unaweza kubishana na Mzalendo Richard Mabala ?😁

Mkuu ni kweli ni vizuri mtoto kupewa elimu kwa lugha anayoielewa lakini uko mbele inamuwia vigumu kufikia malengo yake.
Nia kama unamtesa tu mtoto aisee, huko chuo ni tabu viumbe hwajui ngeli kabisa tabu zaid ni kwenye interview huko ndo purukushani.

Kama taifa linapenda ngeli basi tuanzie chini kabisa.

Kutomfundisha mtoto kingereza ni kumnyima haki ya kuchota maarifa vitabuni, vitabu vingi vya maarifa vimeandikwa kwa kingereza.
Motivational speakers wanatumia hiyo loophole kutafsiri na kupiga pesa.
 
Atafanya biashara na nani?
 
Wanaotaka kiswahili iwe lugha ya kufundishia toka shule ya msingi hadi chuo kikuu watoto wao wanasomesha kwenye shule zinazofundisha kwa lugha ya kiingereza.
Hawa watu ukiwasikiliza unaweza kusema wana nia njema lakini ukweli ni kwamba ndani ya mioyo yao si wenye dhamira njema hasa kwa watoto wa masikini, lengo lao kubwa ni kutaka familia zao ziendelee kutawala na kugawana vyeo huku watoto wa masikini wakiendelea kuwa watwana na vijakazi wao na kuendelea kuwaita yale majina ya kuwabeza kama "watu wetu"/"watu wangu", "wapiga kura wangu" nk.
Kama kweli serikali imedhamiria kufundisha kwa lugha ya kiswahili basi watoe kwanza lile sharti la kutaka wanaoomba baadhi ya ajira kama sio zote kwamba waombaji wajue kuzungumza na kuandika kwa ufasaha lugha ya kiingereza pia mawasiliano yote ya barua, email na njia nyingine za maandishi yafanyike kwa lugha ya kiswahili na miswada yote ipelekwe bungeni kwa lugha ya kiswahili vinginevyo hao wabunge na serikali wote ni wanafiki.
 
Mbunge wa Tabora Kaskazini, Mh. Athuman Maige ameitaka serikali kufanya utafiti wa kina kuhusu lugha ya kufundishia nchini Tanzania. Mbunge huyo amesema "Ziko tafiti zaidi ya 40 zimefanyika na zote zinasema lugha inayofaa kufundishia Tanzania ni Kiswahili, naomba serikali ifanye tena utafiti mahususi kwa ajili ya lugha ya kufundishia kwa Tanzania,"

Aidha Mh. Maige ameongeza kwa kusema "Duniani kote hakuna nchi iliyoendelea kwa kutumia lugha ya watu wengine, Uingereza wanatumia kiingereza, Wachina kichina, lakini Tanzania tunatumia lugha ya kufundishia ni Kiingereza, watoto wanasoma Kiswahili darasa la kwanza hadi la 7,"

Kauli hii inakuja baada ya mjadala mkali unaoendelea kuhusu ipi ni lugha sahihi ya kufundishia nchini Tanzania ambapo baadhi ya wadau wakitaka jitihada zaidi iwekwe kwenye kuwafundisha watoto kiingereza huku wengine wakitaka lugha ya kufundishia ibadilishwe na kuwa kiswahili kwa ngazi zote kuanzia Shule za awali mpaka chuo kikuu huku lugha ya kiingereza ikifundishwa kama somo.
Tatizo hawa watu hawaelewi mambo ya msingi yanayotakiwa kuangaliwa kabla hujasema utumie lugha ipi kufundishia.

Watasema tu kuwa Waingereza wanatumia Kiingereza, Wajapan wanatumia Kijapan, Wachina wanatumia Kichina, hawaendi zaidi ya hapo.

Hawajiulizi kwa nini Wamarekani wanatumia Kiingereza wakato siyo Waingereza, Waswizi wanatumia Kifaransa wakati siyo Wafaransa, Wakanada wanatumia Kiingereza wakati siyo Waingereza, Brazil wanatumia Kireno wakati siyo Wareno, etc.

Huwezi kuamka tu, na kusema naanza kutumia lugha fulani.

Nguvu ya lugha hutegemea nguvu ya uchumi, teknolojia na sayansi.

Tanzania, hata leo hii, tuamue kuwa kuanzia Primary mpaka University, kitumike Kiswahili, wengi wenye uelewa watahangaika kuwapeleka hata mataifa jirani ili watoto wakasome kwa Kiingereza.

Mchina, kwa sasa, anazidi kuongeza vyuo vinavyotoa degree kwa Kiingereza, na pia kuna shule nyingi na vyuo, wanazidi kufungua vya kufundisha lugha ya Kiingereza, unadhani ni kwa sababu gani?

Nchi ikiwa na uchumi imara, teknolojia ya juu na Sayansi, watu wa lugha nyingine, watahangaika kuifahamu lugha yako ili kuzipata fursa zinazopatikana kwako, fursa za uchumi, teknolojia, biashara na sayansi. Nchi ikiwa hohe hahe, ni wachache sana watakaojishughulisha kuifahamu lugha yako. Ukiwatengenezea mazingira wananchi wako wang'ang'anie kutumia hiyo lugha yako katika kupata maarifa, unazidi kuwaua.

Unaweza kuhangaika kutafsiri vitabu vya Kiingereza kwenda Kiswahili ili uwafundishe watu wako kwa Kiswahili lakini ujue kuwa vitabu vya kufundishia ni sehemu ndogo sana ya rejea ya maarifa. Kama hujui Kiingereza, Kifaransa na Spanish, utayakosa maarifa mengi maana makala mbalimbali, rejea, histotia, ugunduzi, vyote vipo katika lugha hizo.

US na Canada, zilikuwa nchi za Wahindu wekundu ambao lugha yao haikuwa Kiingereza. Lugha yao ilipotea kutokana na wahamiaji matajiri toka nchi za Ulaya, ambao wengi wao walikuwa wanaongea Kiingereza. Mpaka leo Kiingereza ndiyo lugha ya Taifa la Marekani na Canada.

Tukitaka lugha itusaidie kupiga hatua kwenye maandeleo katika nyanja nyingi, masomo yote yafundishwe kwa Kiingereza, na Kiswahili kifundishwe tu kama lugha ya mawasiliano yetu ya kila siku. Siyo kitu cha ajabu. Hata hapo kale, wakati wa Masiha Yesu Kristo, huko Uyahudi, Kiebrania (hebrew) kilitumika kama lugha ya mawasiliano ya kawaida kwa Wayahudi, na Kigiriki kilitumika kama Lugha ya wasomi (wengine waliita lugha ya kitaalam). Mpaka leo, Kigiriki kina maneno na alama nyingi, hasa kwenye Sayansi na dini. Mfano herufi ya alfa, omega, etcetera (etc), exampli gratia (e.g.)
 
Watoto wa matajiri na wanasiasa wote wanasoma shule za kiingereza, shule za kiswahili ni kwa watoto wa masikini. Kwa ufupi lugha ya kiswahili ni kwa ajili ya maskini na kiingereza kwa ajili ya matajiri.
Kule Afrika Kusini, wakati wa ubaguzi wa rangi, watoto wa makaburu walikuwa wanafundishwa kwa Kiingereza, wa Waafrika walikuwa wakifundishwa kwa Kiafrikana.

Wale makaburu walijua kuwa usipojua Kiingereza, nafasi yako ya kupata fursa za maendeleo itakuwa duni sana.
 
Kiswahili sio lugha yetu ya asili umeletwa na waarabu karne ya 7 hadi 14, 60% kiarabu, wakati kuna kisukuma kigogo nk hizo ndo lugha za asili
Kwahiyo Tanzania inatambulika kimataifa kua lugha yao ya mawasiliano ni kigogo na kisukuma si ndio??

Usikaze ubongo ndgu hapa naongelea Tanzania kitaifa kiujumla lakini pia kimataifa usilete huo ukabila hapa.

Naposema lugha asili ya watanzania wote tuitikie kiswahili sio kigogo na kisukuma. Ukienda nchi za watu utajitambulisha ni mtanzania unaeongea kiswahili au ni mgogo unaeongea kigogo??
 
Tatizo hawa watu hawaelewi mambo ya msingi yanayotakiwa kuangaliwa kabla hujasema utumie lugha ipi kufundishia.

Watasema tu kuwa Waingereza wanatumia Kiingereza, Wajapan wanatumia Kijapan, Wachina wanatumia Kichina, hawaendi zaidi ya hapo.

Hawajiulizi kwa nini Wamarekani wanatumia Kiingereza wakato siyo Waingereza, Waswizi wanatumia Kifaransa wakati siyo Wafaransa, Wakanada wanatumia Kiingereza wakati siyo Waingereza, Brazil wanatumia Kireno wakati siyo Wareno, etc.

Huwezi kuamka tu, na kusema naanza kutumia lugha fulani.

Nguvu ya lugha hutegemea nguvu ya uchumi, teknolojia na sayansi.

Tanzania, hata leo hii, tuamue kuwa kuanzia Primary mpaka University, kitumike Kiswahili, wengi wenye uelewa watahangaika kuwapeleka hata mataifa jirani ili watoto wakasome kwa Kiingereza.

Mchina, kwa sasa, anazidi kuongeza vyuo vinavyotoa degree kwa Kiingereza, na pia kuna shule nyingi na vyuo, wanazidi kufungua vya kufundisha lugha ya Kiingereza, unadhani ni kwa sababu gani?

Nchi ikiwa na uchumi imara, teknolojia ya juu na Sayansi, watu wa lugha nyingine, watahangaika kuifahamu lugha yako ili kuzipata fursa zinazopatikana kwako, fursa za uchumi, teknolojia, biashara na sayansi. Nchi ikiwa hohe hahe, ni wachache sana watakaojishughulisha kuifahamu lugha yako. Ukiwatengenezea mazingira wananchi wako wang'ang'anie kutumia hiyo lugha yako katika kupata maarifa, unazidi kuwaua.

Unaweza kuhangaika kutafsiri vitabu vya Kiingereza kwenda Kiswahili ili uwafundishe watu wako kwa Kiswahili lakini ujue kuwa vitabu vya kufundishia ni sehemu ndogo sana ya rejea ya maarifa. Kama hujui Kiingereza, Kifaransa na Spanish, utayakosa maarifa mengi maana makala mbalimbali, rejea, histotia, ugunduzi, vyote vipo katika lugha hizo.

US na Canada, zilikuwa nchi za Wahindu wekundu ambao lugha yao haikuwa Kiingereza. Lugha yao ilipotea kutokana na wahamiaji matajiri toka nchi za Ulaya, ambao wengi wao walikuwa wanaongea Kiingereza. Mpaka leo Kiingereza ndiyo lugha ya Taifa la Marekani na Canada.

Tukitaka lugha itusaidie kupiga hatua kwenye maandeleo katika nyanja nyingi, masomo yote yafundishwe kwa Kiingereza, na Kiswahili kifundishwe tu kama lugha ya mawasiliano yetu ya kila siku. Siyo kitu cha ajabu. Hata hapo kale, wakati wa Masiha Yesu Kristo, huko Uyahudi, Kiebrania (hebrew) kilitumika kama lugha ya mawasiliano ya kawaida kwa Wayahudi, na Kigiriki kilitumika kama Lugha ya wasomi (wengine waliita lugha ya kitaalam). Mpaka leo, Kigiriki kina maneno na alama nyingi, hasa kwenye Sayansi na dini. Mfano herufi ya alfa, omega, etcetera (etc), exampli gratia (e.g.)
Mkuu naungana na wewe kabisa, ukiangalia kwa undani unaweza ukapata wasiwasi kwamba hawa "wazalendo" wanaotaka mabadiliko ya lugha ya kufundishia wana agenda zaidi iliyojificha nyuma (wengine wanatafuta consultancy za kutoa expertise katika mabadiliko ya mitaala na namna ya kufundisha na wengine wanataka kupata kazi za kutafsiri vitabu na nyaraka mbali mbali). Kuna nguvu kubwa sana inatumika na watu wachache kuonyesha kwamba lugha ya kiingereza ndio tatizo kubwa katika mfumo wa elimu yetu bila kuangalia matatizo mengine kwa kina.
 
Halafu watoto wa wachache wenye uwezo wanasoma ennglish medium pamoja na hao watunga sera wanaokitaka kiswahili
 
Back
Top Bottom