Atheists tulionekana wa ajabu sana!

Mwana Ukoo

Mwana Ukoo

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2016
Messages
238
Points
500
Mwana Ukoo

Mwana Ukoo

JF-Expert Member
Joined Nov 21, 2016
238 500
Wakuu salama, Kwanza kabisa nianze kwa kusema Elimu pekee ndio itakayomkomboa Mwanadamu katika sayari hii, Uwezo wa kutatua changamoto upo ndani yake mwenyewe, Hakuna Msaada wowote utakaotokea anga za juu kuja kusaidia hapa Dunia Hivyo Binadamu ni Mungu tosha kabisa ni Maarifa na yanazidi kupanuka na kukiweka Huru kiumbe Hichi.

Miaka kadhaa nyuma Baadhi ya sisi atheists humu tulionekana watu wa ajabu kwa imani Yetu kuwa Hakuna Mungu, Mkuu Kiranga ana thread moja imefikisha almost 3K Comments za Believers wakimshambuliwa kwa matusi nae akiwajibu kwa hoja.

Taswira ya JamiiForums sasa iko tofauti kabisa Watu kiukweli wametoka kwenye vifungo na kwa sasa wengi ni Free thinker ata kama Anaamini katika Mungu ila yuko tayari kusikiliza sera za wasio amini na kuchambua kidogo.

Tuliwahi ongea apa kwamba Mungu huyu tunaemsoma makanisani au Misikitini Hawezi kuwepo hata kwa bahati mbaya mana sifa tunazomjaza hayuko nazo hata punje. Nakaribisha mijadala zaidi.

Cc Free ideas Doyi Kiranga nusuhela @Areta ludovick Kifyatu
 
Emmanuel J. Buyamba

Emmanuel J. Buyamba

Verified Member
Joined
May 24, 2013
Messages
1,016
Points
1,500
Emmanuel J. Buyamba

Emmanuel J. Buyamba

Verified Member
Joined May 24, 2013
1,016 1,500
Ahaaa haaa haaa
Swali halijibiwi kwa swali.
Kwa sababu ya uelewa wako mfinyu ndiyo maana unasema swali haliwezi kujibiwa kwa swali,kitu ambacho si kweli.

Unaijua Socratic method ni kitu gani?

Au hujui kuwa hata manabii wenu sehemu nyingi tu walipoulizwa maswali nao walijibu kwa maswali!.

Mfano Yesu (wengine wanamuita nabii Issa bin Maryam) alipoulizwa hayo mamlaka ameyatoa wapi,unakumbuka alijibuje?

Si alijibu kuwa nami ntawauliza swali,mamlaka ya Yohana mbatizaji yalitoka kwa Mungu ama kwa wanadamu?

Jamaa waliposema hatujui nae Yesu akasema nami sitawaambieni yalikotoka.

Kwa hiyo manabii wenu walikuwa wapumbavu kujibu swali kwa swali siyo?

Sasa kwa trend yako hiyohiyo uliyomshauri mtoa mada nami nakujibu hivi,badala ya kuwaacha watu waeñdelee kuamini uzushi na uongo wa uwepo wa Mungu hebu jikite kwanza hapa kuelezea huyo Mungu alikotoka!.
 
Emmanuel J. Buyamba

Emmanuel J. Buyamba

Verified Member
Joined
May 24, 2013
Messages
1,016
Points
1,500
Emmanuel J. Buyamba

Emmanuel J. Buyamba

Verified Member
Joined May 24, 2013
1,016 1,500
Tatizo mtu katoka huko kwao bush kaja mjini kasoma kidgo kadegree kapata elimu....anajiita atheist...acha roho mtakatifu asikie wivu,maana hujitambui,hujui upendo wa MUNGU kwako
Hata wakati Benjamin Franklin anafanya ugunduzi wa kifaa cha kuzuia radi wapo watu wenye fikira finyu walianza kumjadili yeye badala ya hoja zake.

Wapo waliomwambia katoka bush huko atawezaje kupambana na radi?

Na mbumbumbu kabisa wakasema aache tu kufanya ugunduzi huo maana kwanza radi inapopiga na kuua watu pamoja na kuharibu mali duniani inaonesha ukuu na utukufu wa Mungu.

Hakujali mijadala ile na akasonga mbele na kutuletea Lighting conductor, kifaa kilichopunguza ajali za radi kwa kiasi kikubwa.

Mfano mwingine ni Mwl Nyerere wakati anapigania uhuru wa nchi.

Wapo watu badala ya kujadili hoja za kwa nini anadai uhuru, walijikita kumshambulia yeye kwa maneno binafsi.

Kwamba kwanza katoka kijijini Butiama na bukta hadi jijini,kasomeshwa na haohao wakoloni,leo anajiona mjanja kwa kuwapinga?

Mara ni mchonga meno, na mengine kadha wa kadha.

Alichokifanya Nyerere ni kuwapuuza na kusonga mbele kukamilisha misheni.

Kwa hiyo watu kama nyinyi ambao kazi yenu ni kujadili watu badala ya hoja zao dawa yenu huwa ni kuwapuuza tu na kuwaacha.

Ila mimi siwaachi hivi hivi ninawaacha na homework ili kuwapunguzia muda wa kujadili watu, kama ulivyofanya kwa aliyetuletea mada hii.

Na homework hiyo kwa muda huu ni hii,kwa kuwa Mungu wenu ni muweza yote,kwa nini aliumba dunia ambayo inawezekana mtu mwenye ka degree kamoja kufika mjini na kuhoji maswali kama haya wakati alikuwa na uwezo wa kuumba dunia isiyokuwa na uwezekano wa mtu huyo kufika mjini toka bush na kuuliza hivyo?

Je,alitoa uhuru? Kama ni hivyo kwa nini atoe uhuru ambao wewe unaona ni wa mambo ya kipuuzi?

Ndiyo kusema nae ni mpuuzi kwa kuruhusu upuuzi wakati alikuwa na uwezo wa kuuzuia?

Karibu utoe majibu!.
 
eliakeem

eliakeem

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2009
Messages
8,347
Points
2,000
eliakeem

eliakeem

JF-Expert Member
Joined May 29, 2009
8,347 2,000
Kwa sababu ya uelewa wako mfinyu ndiyo maana unasema swali haliwezi kujibiwa kwa swali,kitu ambacho si kweli.

Unaijua Socratic method ni kitu gani?

Au hujui kuwa hata manabii wenu sehemu nyingi tu walipoulizwa maswali nao walijibu kwa maswali!.

Mfano Yesu (wengine wanamuita nabii Issa bin Maryam) alipoulizwa hayo mamlaka ameyatoa wapi,unakumbuka alijibuje?

Si alijibu kuwa nami ntawauliza swali,mamlaka ya Yohana mbatizaji yalitoka kwa Mungu ama kwa wanadamu?

Jamaa waliposema hatujui nae Yesu akasema nami sitawaambieni yalikotoka.

Kwa hiyo manabii wenu walikuwa wapumbavu kujibu swali kwa swali siyo?

Sasa kwa trend yako hiyohiyo uliyomshauri mtoa mada nami nakujibu hivi,badala ya kuwaacha watu waeñdelee kuamini uzushi na uongo wa uwepo wa Mungu hebu jikite kwanza hapa kuelezea huyo Mungu alikotoka!.
Wewe mwenye uelewa mkubwa nilitegemea uanze na kwa kufafanua nilicho kuuliza. Sasa badala yake unaenda kwenye ajenda nyingine.
Tafadhali, rejea kile nilichokuuliza.
 
Emmanuel J. Buyamba

Emmanuel J. Buyamba

Verified Member
Joined
May 24, 2013
Messages
1,016
Points
1,500
Emmanuel J. Buyamba

Emmanuel J. Buyamba

Verified Member
Joined May 24, 2013
1,016 1,500
Wewe mwenye uelewa mkubwa nilitegemea uanze na kwa kufafanua nilicho kuuliza. Sasa badala yake unaenda kwenye ajenda nyingine.
Tafadhali, rejea kile nilichokuuliza.
Uliuliza swali ama ulitoa ushauri wa kwamba mleta mada aache kuwaambia watu wasiamini uwepo wa Mungu na badala yake ajikite kwenye kuelezea chanzo cha Ulimwengu na vilivyomo?

Hilo ni swali ama ushauri?

Au hujui hata tofauti ya swali na ushauri!.

Vipi akisema hataki kujikita huko, yeye anakomaa huku huku?

Hata tukisema twende na akili yako,nami ntakuuliza kama Yesu na mitume wako walivyokuwa wakijibu,
umejuaje kama Ulimwengu na vilivyomo vina chanzo?

Una uthibitisho wa hilo?
 
eliakeem

eliakeem

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2009
Messages
8,347
Points
2,000
eliakeem

eliakeem

JF-Expert Member
Joined May 29, 2009
8,347 2,000
Uliuliza swali ama ulitoa ushauri wa kwamba mleta mada aache kuwaambia watu wasiamini uwepo wa Mungu na badala yake ajikite kwenye kuelezea chanzo cha Ulimwengu na vilivyomo?

Hilo ni swali ama ushauri?

Au hujui hata tofauti ya swali na ushauri!.

Vipi akisema hataki kujikita huko, yeye anakomaa huku huku?

Hata tukisema twende na akili yako,nami ntakuuliza kama Yesu na mitume wako walivyokuwa wakijibu,
umejuaje kama Ulimwengu na vilivyomo vina chanzo?

Una uthibitisho wa hilo?
Ahaaa haaa haaa
Wewe una uwezo wa juu SANA wa kujenga hoja.
Ngoja nitoke ndukii....
 
U

UHURU JR

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2014
Messages
6,904
Points
2,000
U

UHURU JR

JF-Expert Member
Joined Jul 24, 2014
6,904 2,000
1.Hata kama yakinifikirisha kuwa yupo aliyeyaweka, mwekaji huyo si lazima awe ni Mungu mjuzi wa yote,mwenye uwezo wote na upendo wote.

Inawezekana mwekaji huyo akawa ni mwingine tu ambae hatujamjua bado.

Kama ambavyo mwanzoni hatukujua tiba ya Malaria (quinine na nyinginezo), kutokujua tiba ile haikuwafanya watu walazimishe kuwa tiba hiyo ya Malaria lazima iwe mahindi.

Kilichofanyika ni kuweka pembeni pande zinazogoma na kujibidisha kusaka upande wenye uwezekano wa tiba.

Kitendo cha binadamu kutoa haja kubwa (uchafu) ni kuonesha system yake ni imperfection, kwa mujibu wa second law of thermodynamic s.
Muumbaji mwenye uwezo wote,ujuzi wote na upendo wote hawezi kutengeneza kitu chenye mapungufu (imperfection).

Kwa msingi huo muumbaji mwenye sifa hizi lazima awekwe pembeni kwenye kusaka jibu (we shade un required region-in maths),tunasaka upande wa asiyekuwa na sifa hizo zote at the same time.

Otherwise utupe maelezo kwa nini Mungu huyo aliumba vitu vyenye mapungufu wakati alikuwa na uwezo wa kuumba visivyo na mapungufu!.

2.Kitendo cha kumuona Mungu muumbaji (japo mimi sijataka mpaka nimuone ndiyo nijue yupo) kingesaidia kuondoa maswali ya kwamba hayupo na hivyo kutokuwa na utata.

Mfano tu kitendo cha Rais Magufuli kuonekana mara kwa mara kunasaidia sisi kujua uwepo wa Rais wetu.

Hii inatufanya tupokee kwa urahisi utenguzi na uteuzi wa mawaziri na wengineo,maana anapowaapisha tunamuona na tunakiri wazi ni maamuzi ya rais.

Hebu fikiria ingekuwaje iwapo tu baada ya kuapa tar 05/11/2015 angepotea tusimsikie hadi sasa tukawa tunaambiwa tu Rais kamteua yule na kamtengua huyu?

Hapo lazima tungejiuliza yupo kweli au nae alidondoka na ndege ya Malaysia ila tumefichwa tu?

Na kama kweli atakuwepo Ila tu anaongoza kwa rimoti toka alikojificha tangia 2015, na mwakani akaja kuomba ridhaa tena, piga picha ataambulia kura ngapi!

Mpaka hapo nadhani umeshaona faida ya kumuona "live" kiongozi wako.

Sijui nimeeleweka?
Sijakwambia lazima awe nani wala nani ,hatua ya kwanza ni kufikirishwa na hayo hayo mambo ndipo tutaweza kujadili ni nani na si nani,kwanini iwe hivi na si vile.
 
Emmanuel J. Buyamba

Emmanuel J. Buyamba

Verified Member
Joined
May 24, 2013
Messages
1,016
Points
1,500
Emmanuel J. Buyamba

Emmanuel J. Buyamba

Verified Member
Joined May 24, 2013
1,016 1,500
[/QUOTE]
Sijakwambia lazima awe nani wala nani ,hatua ya kwanza ni kufikirishwa na hayo hayo mambo ndipo tutaweza kujadili ni nani na si nani,kwanini iwe uhivi na si vile.
Huwezi ukasonga hatua ya kumtafuta ni nani,kwa nini iwe hivi na si vile wakati bado hujawa na uhakika wa kwamba kuna aliyeyafanya hayo hata kama yatakufikirisha hivyo.

Mathalani mimi pamoja na kunifikirisha still sijapata jibu la kama kuna mtengenezaji ama hayupo.

Kwangu ni ngumu kuanza kumtafuta mtengenezaji huyo kabla ya kupata jibu yupo au hayupo.

Maana hatuwezi kuwa tunafikia hitimisho la jambo kwa mafikirio tu.

Lakini iwapo wewe huwa unao huo uwezo basi tuwekee hapa hitimisho lako ña ushahidi wako and then tuanze kumsaka mhusika huyo.

Unaweza kufanya hivyo!?
 
U

UHURU JR

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2014
Messages
6,904
Points
2,000
U

UHURU JR

JF-Expert Member
Joined Jul 24, 2014
6,904 2,000
Huwezi ukasonga hatua ya kumtafuta ni nani,kwa nini iwe hivi na si vile wakati bado hujawa na uhakika wa kwamba kuna aliyeyafanya hayo hata kama yatakufikirisha hivyo.

Mathalani mimi pamoja na kunifikirisha still sijapata jibu la kama kuna mtengenezaji ama hayupo.

Kwangu ni ngumu kuanza kumtafuta mtengenezaji huyo kabla ya kupata jibu yupo au hayupo.

Maana hatuwezi kuwa tunafikia hitimisho la jambo kwa mafikirio tu.

Lakini iwapo wewe huwa unao huo uwezo basi tuwekee hapa hitimisho lako ña ushahidi wako and then tuanze kumsaka mhusika huyo.

Unaweza kufanya hivyo!?[/QUOTE]

Hebu nitajie mfano wa kitu kimoja tu kilichowahi kukufikirisha na si mbaya ukieleza sababu zinazofanya wewe kuwa hadi sasa usione uwezekano wa kuwepo mtengenezaji?
 
Emmanuel J. Buyamba

Emmanuel J. Buyamba

Verified Member
Joined
May 24, 2013
Messages
1,016
Points
1,500
Emmanuel J. Buyamba

Emmanuel J. Buyamba

Verified Member
Joined May 24, 2013
1,016 1,500
Hebu nitajie mfano wa kitu kimoja tu kilichowahi kukufikirisha na si mbaya ukieleza sababu zinazofanya wewe kuwa hadi sasa usione uwezekano wa kuwepo mtengenezaji?
[/QUOTE]
1.Naona napoteza muda wangu kujadili mambo na mtu ambae kazi yake ni kujiandikia tu ili aonekane nae kaandika.

1.Kwa hiyo wakati unaniuliza mambo haya hayanifikirishi chochote hukujua tunazungumzia mambo gani kiasi cha kunitaka muda huu nikutajie tena walau kimoja?

Ndiyo kusema hujitambui au?

2.Wapi ambapo nimekwambia kuwa sijaona uwezekano wa kuwepo mtengenezaji?

Unajua kusoma? Unajua maana ya mtu kusema kuwa pamoja na kunifikirisha lakini bado sijajua iwapo yupo au hayupo mtengenezaji huyo?

Wewe uliyefikirishwa na Ulimwengu huu na vilivyomo kwa namna vilivyo kisha ukafikia hitimisho kuwa lazima mtengenezaji yupo ndiyo taja sasa na uweke hapa sababu za hitimisho lako hilo.

Na usiishie maneno pekee,weka na ushahidi kuwa lazima vilitengenezwa.

Tukishaupima na kujua kuwa lazima yupo ndipo tunaingia hatua inayofuata ya kumjua ni nani.

Narudia tena,unaweza kufanya hivyo?
 
Narudia tena,unaweza kufanya hivyo?[/QUOTE]

Vitu vyenye kufikirisha viko vingi na mimi nimeomba unitajie kimojawapo tu ambacho kilichokufikirisha.

Ndio hujaona uwezekano huo na ndiyo maana unapinga hata madai yenye kudai hivyo,maana yake hayo mambo hayajakufanya ufikiri kuwa kutakuwa na mtengenezaji.
 
kamanyani

kamanyani

Member
Joined
Jan 2, 2015
Messages
34
Points
125
kamanyani

kamanyani

Member
Joined Jan 2, 2015
34 125
Elimu ipi unayomaanisha? Kama ni elimu ya mashuleni basi Mimi naweza kusema si kitu pekee kinachoweza kumkomboa mwanadamu kwenye sayari hii.

Unaweza ukapata elimu lakini usiwe na uelewa au "knowledge". Ama Kwa lugha nyingine educated fools

Pili kuna watu hawajapata structured basic education, they are self taught, mfano Nikola Tesla etc; na ndio wamekua wavumbuzi wa vitu vingi ambavyo vimepelekea mapinduzi ya kiteknolojia, kifikra,kisayansi na mwishoe kuleta maendeleo na mageuzi makubwa ulimwengu.

Tatu, kuna drop outs wengi Tu ambao walikuja kugundua baadae elimu wanayoipata haiwapeleki kwenye mafanikio zaidi ya kukinzana na files zao Mfano bill gates etc.

Mwisho; elimu tunayopata majority imechakuchuliwa Sana kiasi kwamba haiwezi kutusaidia kifikra mpaka kupelekea kufanya tafiti na gunduzi mpya mbalimbali ambazo zitaleta chachu au mapinduzi ya kimaendeleo kwny sector zote. They are few privileged elites receive proper education which is the hidden education which is transferred through generations to generations to few elected individual with a purpose of controlling us majority. Ndo maana hata maprofesa wetu wa engineering hawawezi kutengeneza mashine ya kukamua juice Tu, scholia mbaya other complex techs
 
Forum statistics

Threads 1,326,022
Members 509,361
Posts 32,209,190
Top