Atheists tulionekana wa ajabu sana!

Atheists tulionekana wa ajabu sana!

mmmmhhhh
sipo kwaajiri ya kubishana au changanya hili na lile ninavyoweza kusema kuna iman nyingi duniani hapa na kila MTU anaamin anapo amin kwamfano watu wengi mashuri kama MZEE mzima Albert Einstein na wengineo wengi walikuwa ni watu wasio amin uwepo wa MUNGU ngoja nikwambie mleta huu Uzi AMIN UNACHO AMIN.
Ila asiamini kila kitu ambacho wengine anaamini pia
 
Mimi hata grup langu la chuo wananiona wa ajabu hasa pale ninapo wapinga live kuhusu huyo mungu.
Lkn kwasasa naona kuna baadhi wamebadilika na kuwa open mind.

Mwanzon unaonekana km jiti lililokosa adabu, lihuni lkn kadri unavyowatemea facts wakaanza kunielewaa.

Sasa tunaheshimiana na wengi kwasasa hawajishughulishi na mambo ya imani km zaman
Kwa kuwa ni wafuasi wako si ndiyo?
 
Dini zetu hazijaweka wazi vitu vingi sana kwa believers wake.
Hii inapelekea kuwepo kwa madukuduku mengi.
Hata sasa baadhi ya conspiracy theories nyingi against the existence of God zinaaza kuleta mantiki ijapokuwa wengi tunakaza ubongo kimtindo.....
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 
Wakuu salama, Kwanza kabisa nianze kwa kusema Elimu pekee ndio itakayomkomboa Mwanadamu katika sayari hii, Uwezo wa kutatua changamoto upo ndani yake mwenyewe, Hakuna Msaada wowote utakaotokea anga za juu kuja kusaidia hapa Dunia Hivyo Binadamu ni Mungu tosha kabisa ni Maarifa na yanazidi kupanuka na kukiweka Huru kiumbe Hichi.

Miaka kadhaa nyuma Baadhi ya sisi atheists humu tulionekana watu wa ajabu kwa imani Yetu kuwa Hakuna Mungu, Mkuu Kiranga ana thread moja imefikisha almost 3K Comments za Believers wakimshambuliwa kwa matusi nae akiwajibu kwa hoja.

Taswira ya JamiiForums sasa iko tofauti kabisa Watu kiukweli wametoka kwenye vifungo na kwa sasa wengi ni Free thinker ata kama Anaamini katika Mungu ila yuko tayari kusikiliza sera za wasio amini na kuchambua kidogo.

Tuliwahi ongea apa kwamba Mungu huyu tunaemsoma makanisani au Misikitini Hawezi kuwepo hata kwa bahati mbaya mana sifa tunazomjaza hayuko nazo hata punje. Nakaribisha mijadala zaidi.

Cc Free ideas Doyi Kiranga nusuhela @Areta ludovick Kifyatu
Siku si nyingi utajua kuwa Mungu yupo/
 
Hahahaaa!!,
Wanadamu hupotea katika njia panda za fikra Zao.

Nmefurahishwa na jinsi unavyojieleza na kutaja wafuasi wa Mrengo wako. Kitu pekee ninachoweza kukwambia ni kuwa kila Swali litajibiwa. Ikiwa utataka majibu.

Ukiujua ukweli utakuweka huru, Nao ukweli ni nini basi?

Ukweli ni kumjua asiyekuwepo kwa mambo yaliyopo. Kumtafuta kwa bidii zote kwa akili aliyokupa. Ukweli hauji kwa kumpinga Asiyekuwepo katika njia panda ya Fikra za nyama.

Basi Nakusihi,, angalia sana katika siku zako, siku za mapito zako. usije ukajipoteza kwa yaliyopo machoni pako nawe ukakosa yasiyokuwepo katika macho yako na Akili yako ambayo katika hayo ndio asili ya roho yako.
Naomba unijibu
1. Kwanini utumie nguvu kumtafuta baba yako ?
2. Kwanini ameweka mazingira magumu ya sisi kumtafuta kama
Magonjwa
Shida
Njaa
Umasikini n.k
 
Atheist wanafeli hapo.... Mungu Hayupo, halafu anasema Binaadamu ni Mungu Tosha. Binaadamu hayupo
Neno 'MUNGU' Sio shida....Hili Ni kapu linaloweza kubeba maana yoyote ile
Hata Mimi naweza Sema "Mimi ni Mungu wa Maisha yangu" Au "Nyota ya Alpha centaury" ndie iliyotuumba
Hakuna shida as long as ni Imani yako tu na unaamini hivo
Shida inakuja unapoonza kubeba mabango na Maspika ukiwahubiria Watu kuwa Imani yako ndio sahihi na nyingine zote hazifai....Kuwa tafsiri yako ya neno Mungu ndo sahihi na wengine wote wanapotosha
Na kuanza kutoa povu na kuwashangaa hata kuwalaani Watu tofauti na imani yako
Hapo Sasa wenye hekima zao,watakuweka kati na kukuomba uthibitishe kuwa Mungu unayeamini yupo kweli na kafanya hayo yote unayohubiri
Kuna Sahani Elfu za chuma na zote zinafanana,Vipi wewe utake tuamini kuwa Sahani yako ndo Bora zaidi bila kututhibitishia ubora wake?
Kuna Miungu zaidi ya Elfu kutoka dini tofauti tofauti,Vipi wewe utake tuamini Mungu wako ndio wa kweli kuliko wengine hao 999?
Thibitisha kuwa Mungu wako Yupo? au funga Domo kwenye mada nzito Kama hizi
 
Back
Top Bottom