Kama kitu kisichokuwepo hakijulikani, wewe umejuaje hakijulikani?
Unajua kujua kitu hakijulikani ni kujua?
Unajua ukisema umejua kitu hakijulikani unaji contradict kwa sababu ukishajua kitu hakijulikani umeshajua hicho kitu na hakiwezi tena kuwa hakijulikani?
Unajua kitu kinaweza kutajwa kwa hadithi tu, bila kuwapo?
Unajua characters wa hadithi za kutunga kina James Bond, Willy Gamba, Kipepe, Ndumilakuwili, Lodi Lofa, Madenge, etc wanajulikana lakini hawapo kiukweli nje ya hadithi?
Sasa mtu akikwambia Mungu naye ni character wa hadithi tu kama hao, na kiukweli hayupo, utasema kwa vile Willy Gamba kaandikwa kwenye hadithi za Aristablus Elvis Musiba, utasema ni lazima yupo vile vile, kwa sababu huwezi kufikiria kitu ambacho hakipo?