Mimi nimeelewa vema pingamizi lako. Unadai kwamba, Mungu mwenye uwezo na nguvu, maarifa na ujuzi kwanini aumbe dunia yenye matatizo?
Mwanzoni nilikujibu kwanza ujielimishe juu ya dunia, ulimwengu, mwanadamu na matatizo ni nini? Nilikuomba kwamba jifunze na uelewe kwanza vitu hivyo kama kweli wewe ni mtu makini na unafikira za kutaka kujifunza.
Pili, nikakuomba ujifunze na uelewe juu ya Mungu ni nini na nini? Nakaendelea kusema, kwamba, jifunze na kuelewa kwanini Mungu alimwumba mwanadamu na alimwumbaje?
Kando na hapo, nikakuomba ujielimishe kuhusu ubongo wa mwanadamu unavyofanya kazi. Hapa kimsingi nilizungumza juu ya kutumia hisia kupima na kuelewa mambo.
Lakini pia, nikasema kwamba iko nafasi kubwa sana hauna ushahidi wa kisayansi ambao wewe unadai unathibitisha malalamiko yako juu ya kutokuwepo Mungu, lakini umezingatia hoja za watu engine ambazo hujaweza kuzifanyia utafiti kujua ukweli wa madai hayo.
Kwa mantiki hiyo, hija yako haitazami eneo lingine ispokuwa kwamba Mungu mwenye nguvu na uwezo wote na huruma na upendo alishindwaje kuumba ulimwengu usio na matatizo na badala yake ni kinyume chake? Hoja yako siyo kwa sababu inaelekea pekee Mungu na jinsi mambo unavyoyaona, lakini kwasababu unaelewa vibaya Mungu ni nani na nini.
Naweza kukujibu kwa kukuomba utafakati mfano huu: maji ni muunganiko wa elementi ya haidrojeni na oksijeni. Hivyo ndivyo ilivyo katika sayansi, lakini jambo hilo ukimweleza mtu asiyefahamu hawezi kukuelewa na atakuwa na maswali mengi.
Lakini kama wewe humwoni Mungu kama ambavyo mafundisho ya dini sahihi yanavyofundisha, basi wewe unamwona nani? Na kwanini unamwona huyo? Lakini pia kwa mwelekeo huo unaouchukua, maana yake unayaona matatizo ndiyo yenye nguvu, uwezo, maarifa na ujuzi kamili na kwa maana hiyo, matatizo ni zaidi ya mwanafamu.