Atheists tulionekana wa ajabu sana!

Atheists tulionekana wa ajabu sana!

Hata Baba mwenye akili
Humtahini mtt wake na kumuadhibu kwa kumnyoosha
Baba kumtahini mtoto ili kujua uelewa wa mtoto ni sahihi, kwasababu baba sio mjuzi wa yote hivyo mtihani ni njia itakayomuwezesha kujua uelewa wa mtoto wake

Pia baba hana uwezo wote wa kumfanya mtoto wake afate yale anayoyataka baba yake

Sasa allah kwanini atumie mtihani inamaana hawezi kujua jambo litalo tokea mbeleni??

Inamaana allah bila kutumia mitihani hawezi kujua jambo lolote kwa viumbe vyake??
 
Walioshika msimamo huo wengi wao wameaminishwa uongo kua mungu yupo bila kujua ukweli kwasababu ya dhana ya kuogofya na ndio maana ukihoji habari zake utawaona watu wanakuambia unakufuru, wengine wameamini kwasababu wamekosa majibu ya baadhi ya vitu
Sioni uhalisia wa hoja zako kwa sababu kuna watu wanakubali uwepo wa Mungu ila wanaishi kinyume na huyo Mungu anavyotaka na huku akiamini kabisa kuna adhabu,sasa mtu huyu utasema anaamini Mungu kwa uoga? halafu pia si kweli watu wanaamini Mungu kisa wamekosa majibu,kuna mambo mangapi maswali mangapi yameshajibika hadi sasa ila bado watu wanaamini Mungu?
 
Nilikuuliza mwili wa ndani ukoje ulinijibu vipi?
Ungeiquote hiyo sehemu halafu tukaendelea, ila sio case tuendelee tu lakini usibadilishe majibu niliokupa, mwili wa ndani ni kile kinachokufanya wewe ukawa na hisia kama njaa, upendo, imani ambayo kila mtu yupo nayo na mengine mengi tu ya kihisia
 
Your question is a non sequitur.

Nikishindwa kuthibitisha origin ya mtu hilo ndilo linathibitisha Mungu yupo?

Unaweza kuthibitisha Mungu yupo?
sasa kama huwez kuthibitisha origin ya mwanadamu..vipi nikisema ww hau exist ????/
 
Sioni uhalisia wa hoja zako kwa sababu kuna watu wanakubali uwepo wa Mungu ila wanaishi kinyume na huyo Mungu anavyotaka na huku akiamini kabisa kuna adhabu,sasa mtu huyu utasema anaamini Mungu kwa uoga? halafu pia si kweli watu wanaamini Mungu kisa wamekosa majibu,kuna mambo mangapi maswali mangapi yameshajibika hadi sasa ila bado watu wanaamini Mungu?

Kuwepo kwa watu wanaoishi kinyume hii inatosha kuwa sababu kuonesha mungu hayupo, angekuwepo kusingekua na watu wa aina hiyo

Mpaka hapo umeona namna gani ya vitu ambavyo havipo ila majina yake yapo??
 
Ungeiquote hiyo sehemu halafu tukaendelea, ila sio case tuendelee tu lakini usibadilishe majibu niliokupa, mwili wa ndani ni kile kinachokufanya wewe ukawa na hisia kama njaa, upendo, imani ambayo kila mtu yupo nayo na mengine mengi tu ya kihisia
Kwaiyo kila kitu kina sifa hizo?
 
Kuwepo kwa watu wanaoishi kinyume hii inatosha kuwa sababu kuonesha mungu hayupo, angekuwepo kusingekua na watu wa aina hiyoT
Mpaka hapo umeona namna gani ya vitu ambavyo havipo ila majina yake yapo??
Huo ni mtazamo wako ila mwengine anaona hao watu hawana hofu ya Mungu japokuwa wanakubali uwepo wake,maana suala zima la uwepo wa Mungu kwanza ni kuamini kuwa yupo halafu kufuata maamrisho na kuacha makatazo yake.

Hata hivyo hiyo sio hoja yangu,mie hoja yangu ni kutaka kujua kwanini hadi sasa kutoka karne na karne ila bado watu wana msimamo wa kuwa Mungu yupo? kipi chenye kufanya huu msimamo uendelee kudumu hadi leo? ukiangalia hii ni imani tu na hakuna mwenye kucontrol watu waamini hivyo lakini watu bado hadi leo wanaamini Mungu..
 
Kwani kila kinachoaminiwa kua kipo ni lazima kiwepo?
 
Kwani kila kinachoaminiwa kua kipo ni lazima kiwepo?
Hapana Sio lazima kiwepo vipo vingi tu tunaaminishwa na havipo hata leo wanasayansi wanaweza kutuaminisha jambo lisilo la kweli na ni kwa sababu ni wanasayansi.

Sasa mie nataka kujua ni kipi chenye kufanya watu hadi leo waseme Mungu yupo?
 
Wakuu salama, Kwanza kabisa nianze kwa kusema Elimu pekee ndio itakayomkomboa Mwanadamu katika sayari hii, Uwezo wa kutatua changamoto upo ndani yake mwenyewe, Hakuna Msaada wowote utakaotokea anga za juu kuja kusaidia hapa Dunia Hivyo Binadamu ni Mungu tosha kabisa ni Maarifa na yanazidi kupanuka na kukiweka Huru kiumbe Hichi.

Miaka kadhaa nyuma Baadhi ya sisi atheists humu tulionekana watu wa ajabu kwa imani Yetu kuwa Hakuna Mungu, Mkuu Kiranga ana thread moja imefikisha almost 3K Comments za Believers wakimshambuliwa kwa matusi nae akiwajibu kwa hoja.

Taswira ya JamiiForums sasa iko tofauti kabisa Watu kiukweli wametoka kwenye vifungo na kwa sasa wengi ni Free thinker ata kama Anaamini katika Mungu ila yuko tayari kusikiliza sera za wasio amini na kuchambua kidogo.

Tuliwahi ongea apa kwamba Mungu huyu tunaemsoma makanisani au Misikitini Hawezi kuwepo hata kwa bahati mbaya mana sifa tunazomjaza hayuko nazo hata punje. Nakaribisha mijadala zaidi.

Cc Free ideas Doyi Kiranga nusuhela @Areta ludovick Kifyatu
Kwa zamani sawa!ila now mepuuzwa mnaonekana ni kundi litakalo kwenda kwenye shimo la tewa!!!!
 
Unazungumza kama unazungumzia kakundi tu kadogo cha watu chenye hali zenye kufanana,kiuhalisia wenye msimamo wa kwamba Mungu yupo ni wengi kutoka jamii mbalimbali tena ni watu wenye hali tofauti tofauti hivyo ni ajabu kutaka tuwachukulie kuwa hao watu ni kama vile hawajielewi elewi wapo wapo tu. Sababu zako sioni kukubalika kwenye uhalisia.

Wenye msimamo wa uwepo wa Mungu ni watu ambao hawana tofauti na wapingaji Mungu,sioni tofauti yeyote waliyonayo wapingaji Mungu.
Unaelewa kwamba wingi wa watu kukubali jambo haufanyi jambo kuwa kweli?

Unaelewa kwamba kuna wakati watu wengi walikubali jua linazunguka dunia, na wingi wao haukufanya jua lizunguke dunia?

Tunaweza kujadili hoja kwa uzito wa hoja, si kwa wingi wa watu wanaosema wanaamini hivi au vile?

Unaelewa kwamba ukiangalia matendo ya watu (ukiacha maneno yao wanayosema wanaamini Mungu), watu wasioamini Mungu ni wengi kuliko wanaoamini Mungu?

Unaelewa kwamba kama kweli watu wangekuwa wanaamini Mungu kama anavyosemwa kwenye vitabu vya dini, kwa mfano, hata kwa Wakristo kufuata amri kumi tu, maasi mengi yasingekuwepo?
 
Mtu anayechukia familia yake ikiuwawa ndio sifa pekee ya mtu wa kawaida?
Kwa nini swali la sifa peke ni muhimu? Kwani mimi nimesema ni sifa pekee? Swali lako linatoka wapi?

Sijaelewa mantiki ya swali lako.

Ni kama nimekukuta umeiba, nimekwambia wewe mwizi umeiba, halafu unaniuliza, kwani wizi ndiyo sifa yangu pekee?

What has that got to do with my case. My case ni kwamba wewe ni mwizi, whether ni sifa yako pekee au si sifa pekee si tatizo langu, tatizo langu wewe mwizi.

Sasa ukianza "kwani wizi ndiyo sifa yangu pekee" nakuona unataka kubadilisha mjadala.

Hujajibu swali.

Kwa nini Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote kaumba ulimwengu ambao mabaya

yanawezekana, wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani?

Hujajibu swali hili.
 
sasa kama huwez kuthibitisha origin ya mwanadamu..vipi nikisema ww hau exist ????/
Hilo pia halitathibitisha kwamba Mungu yupo.

Nataka uthibitishe Mungu yupo.

Hujajibu swali.

Kwa nini Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote kaumba ulimwengu ambao mabaya

yanawezekana, wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani?

Hujajibu swali hili.
 
thibitisha ni nan aliumba ulimwengu???/

Kwa nini unafikiri ni "nani" ?

Hujajibu swali.

Kwa nini Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote kaumba ulimwengu ambao mabaya

yanawezekana, wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani?

Hujajibu swali hili.
 
Unaelewa kwamba wingi wa watu kukubali jambo haufanyi jambo kuwa kweli?R
Unaelewa kwamba kuna wakati watu wengi walikubali jua linazunguka dunia, na wingi wao haukufanya jua lizunguke dunia?
Tunaweza kujadili hoja kwa uzito wa hoja, si kwa wingi wa watu wanaosema wanaamini hivi au vile?
Unaelewa kwamba ukiangalia matendo ya watu (ukiacha maneno yao wanayosema wanaamini Mungu), watu wasioamini Mungu ni wengi kuliko wanaoamini Mungu?
Unaelewa kwamba kama kweli watu wangekuwa wanaamini Mungu kama anavyosemwa kwenye vitabu vya dini, kwa mfano, hata kwa Wakristo kufuata amri kumi tu, maasi mengi yasingekuwepo?
Sijasema wingi ndio usahihi bali nimesema hoja zako zilikuwa kama zinazungumzia kakundi ti kidogo cha watu wakati hao watu,maana jinsi ulivyowaelezea ni kama watu ambao wanapelekeshwa tu hawajielewi na ndiyo nikaingiza habari ya wingi kwa maana wao ndio wengi hivyo wanapatikana kila aina ya watu kupitia wao.

Huwezi kusema mtu haamini Mungu kisa anafanya kinyume na vitabu vya dini vinavyosema,kwa sababu kuamini Mungu ni jambo moja (ambalo wengine hawana) na kufuata maamrisho na makatazo ni jambo la pili. Anayeamini Mungu lakini hufanya yaliyokatazwa na Mungu kumbuka kwake hayo anayoyafanya huyatambua kuwa ni dhambi hivyo ni tofauti na wewe asiyeamini Mungu.
 
Wingi ndio usahihi au si usahihi?

Ukishasema wingi si usahihi, point ya kuongelea "kikundi kidogo cha watu" ni moot, haina maana.

Kama wingi si usahihi, usahihi unajali nguvu ya hoja, si wingi wa watu, suala la kikundi kidogo au kikubwa si muhimu, suala la muhimu ni nguvu ya hoja.

Kwa hiyo, andika upya habari yako.

Kama unasema wingi si usahihi, ondoa kabisa habari za "kikundi kidogo cha watu" (ambacho hata huwezi kuthibitisha kwamba ni kidogo).

Kama unataka kuandika habari za "kikundi kidogo cha watu", ondoa habari za "sijasema kwamba wingi ndiyo usahihi".

Hutakiwi kuambatanisha habari ya "sijasema wingi ndiyo usahihi" halafu hapo hapo ukaendeleza na "kikundi kidogo cha watu".

Utakuwa una ji contradict kwa kutaka kusema wingi si usahihi, halafu hapo hapo unahesabu ukubwa wa kikundi cha watu katika ku validate hoja yako.

You can't eat your cake and still have it.

You are contradicting yourself.
 
Back
Top Bottom