Scars
JF-Expert Member
- Apr 8, 2017
- 53,201
- 132,376
Usikifanye kichwa chako kua kigumu jaribu kuelewa jibu niliokupa. Mwenyezi Mungu hakumuumba binaadamu kwa lengo la kufanya maovu wala ulimwengu haukuumbwa ili maovu yafanyike.
Kama mungu hakumuumba binadam kwa lengo la kufanya maovu, ina maana maovu yalikua sio mategemeo ya mungu?? Inamaana maovu yaliingia kwa bahati mbaya katika ulimwengu kwamba ilikua ni tofauti na mategemeo yake??
kwaiyo mungu alifanya betting hakujua kama mkeka utachanika??
Lengo la kutuumba sisi ni kuja kumuabudu hakutuumbwa kwa lengo la kuja kufanya maovu, mpaka hapo unashindwa kuelewa kua tuliumbwa kwa lengo gani. Baada ya kuumbwa Adam alipewa akili na akaletwa duniani kuja kumuabudu.
Kama ilikua sio lengo lake ulimwengu utawaliwe na maovu je baada ya kuona maovu kwanini hakuyaondoa ili aabudiwe katika ulimwengu mtakatifu??
Kama alijua kua kuna maovu yatakuwepo, utasemaje kua ulikua sio mpango wake??
Kama alijua kua kutakua na maovu utasemaje kua anaupendo wote kwa viumbe vyake??