Atheists tulionekana wa ajabu sana!

Atheists tulionekana wa ajabu sana!

Mungu Ana sifa hizo kwanini unasema hayupo?
Kupitia izo sifa zinaonesha tena kua hayupo ni kitu cha kufikirika tu

Achilia mbali kukosa ushahidi kuonesha yupo ambalo ndio njia kuu ilikujua uwepo wake
 
Nafkiria hatutaweza kuelewana ikiwa unakwepa kujibu swali langu, Hebu nijibu halafu tuendelee na maada. Kulikua na mabaya duniani kabla ya sisi binaadamu kuwepo?
Nyinyi ndio mnakwepa maswali magumu kwa style ya kishamba sana hachunguziki

Ukikosoa biblia au kuraan kwa kuonesha kasoro utasikia "biblia/kuraan haisomwi kama gazeti"

Vipi kama nasisi tutumie kichaka icho, yani ukiuliza swali nikujibu swali kwa kebei halafu ukiuliza ili upewe ufumbuzi nikuambie majibu yangu hayachunguziki kwa akili zenu

Tutaelewana kwa mtindo huu kweli???
 
Nafkiria hatutaweza kuelewana ikiwa unakwepa kujibu swali langu, Hebu nijibu halafu tuendelee na maada. Kulikua na mabaya duniani kabla ya sisi binaadamu kuwepo?
Unaelewa kwamba dunia ambayo inawezekana kuwa na mabaya kuumbwa wakati ingewezekana kuumbwa isiyowezekana kuwa na mabaya, tayari hiyo dunia inayowezekana kuwa na mabaya ina mabaya?

Unaelewa kwamba dunia hiyo imeumbwa kwa choyo cha kuwanyima watu dunia isiyo na mabaya na kuwapa dunia inayowezekana kuwa na mabaya?

Mungu wenu ana choyo? Kwa nini kaumba ulimwengu kwa choyo?

Kwamba huyu Mungu kakaa.

Anawaza. Niumbe dunia ipi? Inayowezekana kuwa na mabaya au isiyowezekana kuwa na mabaya?

Anaamua kuumba dunia inayowezekana kuwa na mabaya. Wakati angeweza kuumba dunia ambayo haiwezekani kuwa na mabaya.

Hapo tu, dunia aliyoiumba ina mabaya tayari.

Kaiumba kwa choyo. Choyo ni ubaya.

Kabla ya kuumbwa kiumbe chochote. Dunia hiyo imeumbwa kwa choyo.

Unaelewa hilo?
 
Sina elimu nalo hilo.
Ok

Panya huyo na paka aliyevishwa kengele hawapo

Kwani hujui kua mtunzi wa hadithi anaweza kutumia characters ambao ni finction ili kufikisha ujumbe kwa hadhira??
 
Nyinyi ndio mnakwepa maswali magumu kwa style ya kishamba sana hachunguziki

Ukikosoa biblia au kuraan kwa kuonesha kasoro utasikia "biblia/kuraan haisomwi kama gazeti"

Vipi kama nasisi tutumie kichaka icho, yani ukiuliza swali nikujibu swali kwa kebei halafu ukiuliza ili upewe ufumbuzi nikuambie majibu yangu hayachunguziki kwa akili zenu

Tutaelewana kwa mtindo huu kweli???
Hahah unajua huyo kiranga nimeanza nae vipi? nimempa majibu vizuri ya maswali yake ila mimi nimemuuliza hilo swali moja anakwepa kujibu, halafu unajua najaribu kwenda na nyie kwa upeo wa kifikra lakini nikikuletea mandishi katika kitabu cha Qur'an hutachomoka na utaishia kusema ni hadithi zilizotungwa
 
Mungu angekuwa hachunguziki kusingekuwa na Biblia wala Quran.

Ukisoma Biblia au Quran kwa kuamini ni vitabu vya Mungu tayari unamchunguza.

Sasa wanaji contradict.

Wanasema Mungu hachunguziki, kwa kutumia maneno ya vitabu ambavyo wanasoma kumchunguza Mungu.

Contradictions.
 
Wakuu salama, Kwanza kabisa nianze kwa kusema Elimu pekee ndio itakayomkomboa Mwanadamu katika sayari hii, Uwezo wa kutatua changamoto upo ndani yake mwenyewe, Hakuna Msaada wowote utakaotokea anga za juu kuja kusaidia hapa Dunia Hivyo Binadamu ni Mungu tosha kabisa ni Maarifa na yanazidi kupanuka na kukiweka Huru kiumbe Hichi.

Miaka kadhaa nyuma Baadhi ya sisi atheists humu tulionekana watu wa ajabu kwa imani Yetu kuwa Hakuna Mungu, Mkuu Kiranga ana thread moja imefikisha almost 3K Comments za Believers wakimshambuliwa kwa matusi nae akiwajibu kwa hoja.

Taswira ya JamiiForums sasa iko tofauti kabisa Watu kiukweli wametoka kwenye vifungo na kwa sasa wengi ni Free thinker ata kama Anaamini katika Mungu ila yuko tayari kusikiliza sera za wasio amini na kuchambua kidogo.

Tuliwahi ongea apa kwamba Mungu huyu tunaemsoma makanisani au Misikitini Hawezi kuwepo hata kwa bahati mbaya mana sifa tunazomjaza hayuko nazo hata punje. Nakaribisha mijadala zaidi.

Cc Free ideas Doyi Kiranga nusuhela @Areta ludovick Kifyatu

1. Huwezi kuwa 'atheist' kama huamini au hujui Mungu yupo. 2. Kama huamini au hujui kama Mungu huwezi kumjadili. By the way, utaanzia wapi kujadili kitu ambacho hakipo? 3 The fact kwamba atheists wanamjadili Mungu ni ushahidi mojawapo kuwa wanaamini au wanajua yupo. 4. Wanachokifanya wao ni kukana kwamba Mungu na haiwezekani ukane kitu kisichokuwepo maana utaonekana mtu wa ajabu sana. Kuna atheist mmoja anaitwa Richard Dawkins: kitabu chake kimojawapo kinaitwa "The God Delusion". Kwenye moja ya mijadala Youtube juu ya uwepo wa Mungu, alibishana na mwanamjadala mwenzake na yule bwana aliposema kitu ambacho Dawkins hakubaliani naye, Dawkins akajisahau na kusema: "Oh! My God!" Yaani kuonyesha kwamba alishangazwa na jinsi yule bwana alivyo'argu' na akajikuta amerudi kwenye senses na kumtaja "Mungu" ambaye anamkana "hayupo". Atheists wanacheza tu na akili zetu, lakini deep down in their heart they believe in God. Tulikuwa na Mtanzania mwenzetu Kingunge Ngombale Mwiru, ambaye tangu nikiwa mtoto nilisikia habari zake kwamba haamini kama Mungu yupo. Lakini nilisikia kwenye media kwamba alipokaribia kurudi kwa baba ilibidi aombe aonane na padri kwa lengo la kutubu na kurudi kwenye Kanisa Katoliki, ambalo alikuwa ameliacha miaka nenda rudi. Kwenye mambo ya imani ni vigumu kuchora mstari - maana tunaona waliokuwa wakiamini wanaacha imani/dini na pia wale walioacha wanarudi. Kama pia ilivyo kwa wafanyabiashara. Kuna waliokuwa wafanyabiashara wamefirisika na kuna waliokuwa maskini na hawana biashara wanatajirika katika mazingira yaleyale ya kutajirika na kuwa maskini.
 
Hahah unajua huyo kiranga nimeanza nae vipi? nimempa majibu vizuri ya maswali yake ila mimi nimemuuliza hilo swali moja anakwepa kujibu, halafu unajua najaribu kwenda na nyie kwa upeo wa kifikra lakini nikikuletea mandishi katika kitabu cha Qur'an hutachomoka na utaishia kusema ni hadithi zilizotungwa
Wewe unaelewa kwamba Quran inasema Allah atawaziba watu macho, masikio na kuwafanya mioyo yao iwe migumu, ili wasimuelewe.

Halafu atawahukumu vikali kwa sababu hawakumuelewa.

Yani Allah mwenyewe anajitekenya, halafu anacheka.

Anawaziba watu akili wasimjue, halafu anawahukumu kwa sababu hawamjui (wakati yeye mwenyewe ndiye iyewazibia wasimjue!).

Unaona hayo ni maneno ya Mungu kweli au ya watu wajinga tu?
 
Walioandika wameyapata kwa manabi wa Mungu au walimsikia wenyewe
Hujajibu swali nililokuuliza na ulilojibu sijakuuliza.

Unaweza kuthibitisha hayo ya kwenye vitabu kasema Mungu na hayajaandikwa na watu tu bila Mungu kusema wala kuwepo?
 
Kupitia izo sifa zinaonesha tena kua hayupo ni kitu cha kufikirika tu

Achilia mbali kukosa ushahidi kuonesha yupo ambalo ndio njia kuu ilikujua uwepo wake
Ushawahi kusikia jina la kitu ambacho hakipo duniani?
 
Hahah unajua huyo kiranga nimeanza nae vipi? nimempa majibu vizuri ya maswali yake ila mimi nimemuuliza hilo swali moja anakwepa kujibu, halafu unajua najaribu kwenda na nyie kwa upeo wa kifikra lakini nikikuletea mandishi katika kitabu cha Qur'an hutachomoka na utaishia kusema ni hadithi zilizotungwa
Huu mjadala mmeufanya dampo la kuongea vitu ambavyo wenyewe mkiulizwa mnashindwa kujibu, sasa hizi takataka tuzitupe wapi kama sio kwenu nyinyi zilikotoka??

Nilikuambia chanzo cha mabaya ni nini ukasema shetani, nikakuuliza kama chanzo cha mabaya ni shetani sasa kabla ya shetani kuasi alikua kiumbe chema kabisa sasa kiburi na majivuno vilimuingia kwa mechanism gani hadi akaasi? Ukasema kwanza chanzo cha dhambi ni nafsi hivyo nafsi ya shetani ndiyo sababu

Nikakuuliza nafsi ninini ulinijibuje???
 
Hujajibu swali nililokuuliza na ulilojibu sijakuuliza.

Unaweza kuthibitisha hayo ya kwenye vitabu kasema Mungu na hayajaandikwa na watu tu bila Mungu kusema wala kuwepo?
Kwa Imani nathibitisha
 
Unaelewa kwamba dunia ambayo inawezekana kuwa na mabaya kuumbwa wakati ingewezekana kuumbwa isiyowezekana kuwa na mabaya, tayari hiyo dunia inayowezekana kuwa na mabaya ina mabaya?

Unaelewa kwamba dunia hiyo imeumbwa kwa choyo cha kuwanyima watu dunia isiyo na mabaya na kuwapa dunia inayowezekana kuwa na mabaya?

Mungu wenu ana choyo? Kwa nini kaumba ulimwengu kwa choyo?

Kwamba huyu Mungu kakaa.

Anawaza. Niumbe dunia ipi? Inayowezekana kuwa na mabaya au isiyowezekana kuwa na mabaya?

Anaamua kuumba dunia inayowezekana kuwa na mabaya. Wakati angeweza kuumba dunia ambayo haiwezekani kuwa na mabaya.

Hapo tu, dunia aliyoiumba ina mabaya tayari.

Kaiumba kwa choyo. Choyo ni ubaya.

Kabla ya kuumbwa kiumbe chochote. Dunia hiyo imeumbwa kwa choyo.

Unaelewa hilo?
Hahaha unajaribu kutetea na kukwepa kujibu swali kwa ndio au hapana, sasa ngoja nikueleweshe. Kabla kuletwa wanaadamu katika dunia hapakua na mabaya yoyote na ulimwengu ulikua umetakasika na kulikuepo na ndege na wanyama wakiishi kwa amani. Baada ya sisi viumbe kuja duniani na kuambiwa na Mungu tufate maamrisho yake basi baadhi ndipo wakaanza kiburi na kukataa kufata maamrisho na kuanza kuichafua dunia, hivyo hayo mabaya yote yanasababishwa na binaadamu kwa kutotaka kufata mema aliambiwa na Mungu. Na huwezi kusema Mungu ameumba dunia kwa choyo ikiwa ameweka vitu kwa balance na vyenye manufaa kwa viumbe wake ikiwemo mimea nafkiri unaelewa mchango wake kwa viumbe ameweka ozone layer ambayo unaelewa faida yake na binaadamu ndio wanaiharibu leo hii na mengine mengi yenye manufaa kwa binaadamu.
 
Huu mjadala mmeufanya dampo la kuongea vitu ambavyo wenyewe mkiulizwa mnashindwa kujibu, sasa hizi takataka tuzitupe wapi kama sio kwenu nyinyi zilikotoka??

Nilikuambia chanzo cha mabaya ni nini ukasema shetani, nikakuuliza kama chanzo cha mabaya ni shetani sasa kabla ya shetani kuasi alikua kiumbe chema kabisa sasa kiburi na majivuno vilimuingia kwa mechanism gani hadi akaasi? Ukasema kwanza chanzo cha dhambi ni nafsi hivyo nafsi ya shetani ndiyo sababu

Nikakuuliza nafsi ninini ulinijibuje???
Hapa tunakwenda taratibu kwa kueleweshana mwisho wa siku wewe ndio utabaki kuamua uamini kipi na uache kipi. Mbona nilishakujibu nafsi ni mwili wa nnje na wa ndani kwa ujumla, yaani wewe hapo ulipo ni nafsi. Na nmeona maswali yako mengine na yote nakuletea majibu hapa mpaka tutafikia muafaka twende taratibu tu.
 
Ok

Panya huyo na paka aliyevishwa kengele hawapo

Kwani hujui kua mtunzi wa hadithi anaweza kutumia characters ambao ni finction ili kufikisha ujumbe kwa hadhira??

Hoja yako iko wapi sasa ?
 
Back
Top Bottom