Atheists tulionekana wa ajabu sana!

Atheists tulionekana wa ajabu sana!

Kama njia zake hazichunguziki usingeweza hata kusema hazichunguziki.

Kusema hazichunguziki maana yake umeweza kuzichunguza na kugundua hazichunguziki, mpaka hapo ushazichunguza.

Huu ni uongo wa kufunika ukweli kwamba huyo Mungu hayupo, na huwezi kuthibitisha yupo.

Kama unabisha, thibitisha yupo.
Sijasema mini kasema mwenyewe Mungu katika vitabu vyake Kama ilivyo sifa ya kuwa muweza wa Yote,mjuzi wa yote
 
Hapo unaonesha jinsi gani ulivyotumia kila namna ya kuchunguza lakini uka shindwa, baada ya kushindwa ulitakiwa umalize kwa kusema hayupo sio kupendekeza majibu ya kisiasa

Kisicho kuwepo hakichunguziki hilo halina ubishi

Na ndio maana hua nasema huwezi kuchunguza kitu kisichokuwepo kua hakipo. leo hii ume prove
Kwani hizi sifa Mungu mnazozisema muweza wa Yote ,mjuzi wa yote,njia zake hazichunguziki nimempa Mimi?
 
Sijasema mini kasema mwenyewe Mungu katika vitabu vyake Kama ilivyo sifa ya kuwa muweza wa Yote,mjuzi wa yote
Unaweza kuthibitisha hayo ya kwenye vitabu kasema Mungu na hayajaandikwa na watu tu bila Mungu kusema wala kuwepo?
 
Naomba unipe sifa za jambo lisilo kuwepo huwa lina sifa gani ?
 
Walioandika wameyapata kwa manabi wa Mungu au walimsikia wenyewe
 
Naomba unipe sifa za jambo lisilo kuwepo huwa lina sifa gani ?
Unaweza kujua jambo halipo kwa kuangalia contradiction.

Kwa mfano. Katika Euclidean geometry planes, pembetatu ina nyuzi 180, duara lina nyuzi 360.

Hivi ni vitu viwili tofauti.

Mtu akisema katika Euclidean geometry planes kuna pembetatu ambayo hapo hapo ni duara, hiyo pembetatu ambayo ni duara itakuwa na contradiction.

Kwa sababu hapo hapo itakuwa na nyuzi 180 tu na pia itakuwa na nyuzi 360 tu.

Hivyo, contradiction hiyo inaonesha hakuna pembetatu ambayo hapo hapo ni duara.

Mungu wenu ni kama hiyo pembetatu ambayo ni duara pia.

Amejaa contradictions.

Kwa sababu hayupo.

Katungwa tu na watu.

Tena enzi za giza, watu walikuwa hawaoni contradictions hizi.

Kama unabisha, thibitisha Mungu yupo.
 
Sifa yake ya njia zake hazichunguziki mbona haujaiweka?
Hakichunguziki kwasababu hakipo, kikiwepo lazima kichunguzike na majibu kuonesha kipo yatatolewa bila utata wowote

Mungu achunguziki kwasababu hayupo, angekuwepo angechunguzika bila kipingamizi chochote
 
Hujathibitisha kama hayupo,unaleta mifano ya pembe ymtatu,uwepo wa pembe tatu ni makubaliano tu ya wana mahesabu.

Jikite katika uhalisia wa mada husika na usitafute kichaka.

Sio kila utata huonyesha kutokuwepo kwa jambo,bali kuna utata mwingine hutokea kwa ujinga wa watu na kuhisi kama jambo lina utata.

Sasa leta uthibitisho wa kuwa Mola hayupo kwa kutumia utata unao usema.
 
Katika maswali yako huwa unajenga hoja unayakumbuka?
 
Kwani hizi sifa Mungu mnazozisema muweza wa Yote ,mjuzi wa yote,njia zake hazichunguziki nimempa Mimi?
Umeona kua sifa hizi za muweza wa yote, mjuzi wa yote na mwenye upendo wote zinaonesha kua si kweli kwasababu kitu chenye sifa izo hakipo

Sio wewe wala sio mimi zinaonekana zimetungwa na watu tu ambao walishindwa kujua challenge watakayokua wanakumbana nayo pindi wakiulizwa

Na ndio maana inakua ngumu kuelezea pasipo kujipinga au kuacha utata kwasababu ni myths. Ndio maana waliotunga huu uongo wakasema hazichunguziki
 
Huu ndo uzi sasa, ila nimegundua wengi hatusomi contents za wachangiaji, tuna-attack watu na sio hoja, labda mchango wangu kwenye hili ni kwamba, kwanza hakuna muafaka utakaofikiwa kwa vile ni mada wazi sana, anaeamini Mungu yupo alete ushahidi wake na anayeamini hayupo alete ushahidi, lets go with facts sio hisia tu, mada kama hzi sio personal, lets take it positively.
 
Hujathibitisha kama hayupo,unaleta mifano ya pembe ymtatu,uwepo wa pembe tatu ni makubaliano tu ya wana mahesabu.

Jikite katika uhalisia wa mada husika na usitafute kichaka.

Sio kila utata huonyesha kutokuwepo kwa jambo,bali kuna utata mwingine hutokea kwa ujinga wa watu na kuhisi kama jambo lina utata.

Sasa leta uthibitisho wa kuwa Mola hayupo kwa kutumia utata unao usema.
Panya mabaka aliyeitisha mkutano kwa kujadili mbinu za kumfunga paka kengele baada ya familia yake kuuawa yupo???
 
Umeona kua sifa hizi za muweza wa yote, mjuzi wa yote na mwenye upendo wote zinaonesha kua si kweli kwasababu kitu chenye sifa izo hakipo

Sio wewe wala sio mimi zinaonekana zimetungwa na watu tu ambao walishindwa kujua challenge watakayokua wanakumbana nayo pindi wakiulizwa

Na ndio maana inakua ngumu kuelezea pasipo kujipinga au kuacha utata kwasababu ni myths. Ndio maana waliotunga huu uongo wakasema hazichunguziki
Mungu Ana sifa hizo kwanini unasema hayupo?
 
Unawezaje kuthibitisha Aadam ni binadam wa kwanza kuumbwa, na hili si hadithi tu?

Halafu, bin Adam maana yake ni mtoto aliyezaliwa na Adam, sasa Adam atakuwaje binadamu wa kwanza, wakati yeye ndiye Adam na hakuzaliwa na Adam?

Hivi unaelewa hata unachoandika wewe mwenyewe?
Nafkiria hatutaweza kuelewana ikiwa unakwepa kujibu swali langu, Hebu nijibu halafu tuendelee na maada. Kulikua na mabaya duniani kabla ya sisi binaadamu kuwepo?
 
Back
Top Bottom