Naendelea... Pia ndugu Kiranga unaonekana unamkataa Mungu pekee kwa sababu ya matatizo unayoyaona na kusikia hapa duniani. Kumbe, basi, hupati kufikiri chanzo cha hayo matatizo ni nani? Je, ni Mungu? Je, ni dunia? Je, ni ulimwengu au mwanadamu?
Lakini pia, hufikiri na kujiuliza: nguvu, maarifa na ujuzi wa Mungu hauonekani katika yale unayomkataa Mungu? Kando na hayo, bado hujajifunza na kuelewa matatizo na raha!
Kwa ujumla, ndugu Kiranga, unaishi, unajifunza na unaelewa katika uzushi. Hilo kwa hakika lingeweza kukusaidia kama ungetumia hayo yanayo kwambia na kukusukuma kusema hakuna Mungu, kuyafanyia utafiti na majaribio. Bahiti mbaya wengi tunamkataa Mungu hata kwa mambo wazi ambayo ni dhihiri karika koo na familia zetu. Tunaweza kumjua Mungu kwa kufanya utafiti usio hitaji majaribio katika familia,koo na jamii zetu.