Atheists tulionekana wa ajabu sana!

Atheists tulionekana wa ajabu sana!

Binaadamu amepewa akili na Muumba wake ambae na Mungu, hebu niulize swali lako linalokufanya usiamini uwepo wa Mungu.
Akili gani hiyo?

Alishindwa kunipa akili ya kumjua bila utata wowote?
 
Kama chanzo cha uovu ni shetani

Shetani tunaambiwa alikua ni mwema ila ghafla akapata kiburi anbacho ni uovu akamsaliti mungu.

Sasa huo uovu wa icho kiburi cha shetani ulitoka wapi na hapa umesema chanzo cha uovu ni shetani?
Mungu aliumba majini kwa moto na binaadamu kwa udongo, hivyo baada kuumbwa Adam Mungu aliamrisha majini na Malaika kumsujudia, Shetani alikataa kumsujudia kwasababu yeye alijiona ameumbwa kwa moto hawezi kujishusha ndipo alipofukuzwa katika utukufu wa Mungu na kuahidi alioyaahidi
 
Akili gani hiyo?

Alishindwa kunipa akili ya kumjua bila utata wowote?
Hiyo akili ulionayo wewe ikafanya usiamini uwepo wake ungeiweza pia kuitumia na kufahamu uwepo wake. Au wewe hauna akili mpaka unauliza akili gani??
 
God is nature and nature cant be changed, we have to respect the nature.
Ndo maana mababu zetu waliabudu waliowatangulia coz waliamini kuwa waliwatangulia hapa duniani.
Each and every living organism on this earth always think of its existence and that is the only way you can believe there is something caused you to exist in this world(God) or Nature. Respect the Nature......baaaas
 
Hiyo akili ulionayo wewe ikafanya usiamini uwepo wake ungeiweza pia kuitumia na kufahamu uwepo wake. Au wewe hauna akili mpaka unauliza akili gani??
Wewe akili ya kumjua mungu umeipata wapi?
 
Chanzo cha uovu ni shetani ambae alimuahidi Mungu kupotosha wanaadamu
Mkuu, mm sitaki kujibiwa kulingana na Mungu. Mm nataka wasioamini kuwa Mungu yupo, wanipe chanzo cha uovu.
 
Mungu aliumba majini kwa moto na binaadamu kwa udongo, hivyo baada kuumbwa Adam Mungu aliamrisha majini na Malaika kumsujudia, Shetani alikataa kumsujudia kwasababu yeye alijiona ameumbwa kwa moto hawezi kujishusha ndipo alipofukuzwa katika utukufu wa Mungu na kuahidi alioyaahidi

Icho kiburi cha shetani kilitoka wapi?
 
Kilitokana na nafsi yake, Mbona nimeshakueleza tayari kua aliumbwa kwa moto hivyo aliona binaadamu aliembwa kwa udongo ni dhalili kwake
Kilitokana na nafsi yake baada ya kushawishiwa na nini?

Kitu gani kilishawishi nafsi yake hadi akafanya ule uovu?
 
Ili Mjadala wowote uwe na Maana,Kwanza inabidi uwe na tafsiri ya Kila maneno yatakayo tumika katika Mjadala huo(Keywords)
Huyo Ni Socrate

Sasa tuanzie Hapa "Mungu Ni Nini?...Nipe tafsiri yake?
Mungu sio kiumbe, ni muweza wa yote na hakuna zaidi yake
 
Hujathibitisha, umelazimisha tu pasipo kuelezea ni namna gani

Hapo unamaanisha Kabla ya uwepo wangu mungu huyo hakuwepo

Uwepo wangu unathibitisha mungu yupo, nisipo kuwepo itatupa jibu gani?
Wewe umetaka ushahidi, nimekwambia uwepo wako tu tayari ni ushahidi kama kuna Mungu. sasa kama wewe hupo au hakuna kiumbe chochote, tena angejadiliwa vipi? ungekuwa wewe hupo na mimi sipo tena vipi mimi na wewe tujue kama mungu yupo au hayupo ikiwa hatupo ulimwenguni?
 
Ujeuri ulitokana na nafsi yake mwenyewe kwa kujiona
Kilitokana na nafsi yake baada ya kushawishiwa na nini?

Kitu gani kilishawishi nafsi yake hadi akafanya ule uovu?
Kiburi na majivuno ya shetani ndizo sifa zilizompekea yeye kufukuzwa peponi na kulaaniwa na Mwenyezi Mungu. Hili ni mojawapo ya mafunzo tunayopaswa kujifunza kama wanadamu na kuepukana na kiburi. Hatupaswi kuwadharau wanadamu wengine wala viumbe wengine wa Mwenyezi Mungu kwa kujiona kuwa bora zaidi yao.
 
Ujeuri ulitokana na nafsi yake mwenyewe kwa kujiona

Kiburi na majivuno ya shetani ndizo sifa zilizompekea yeye kufukuzwa peponi na kulaaniwa na Mwenyezi Mungu. Hili ni mojawapo ya mafunzo tunayopaswa kujifunza kama wanadamu na kuepukana na kiburi. Hatupaswi kuwadharau wanadamu wengine wala viumbe wengine wa Mwenyezi Mungu kwa kujiona kuwa bora zaidi yao.

Unakwama wapi mtumishi??

Kiburi na majivuno ya shetani yalimuingiaje? Kulikua na shetani mwingine aliyempandikiza hayo majivuno?

Maana tumeona ili uovu utokee lazima awepo shetani wakusababisha sasa hayo majivuno na kiburi kilisababishwa na kitu gani hadi kikamuingia shetani??
 
Wewe umetaka ushahidi, nimekwambia uwepo wako tu tayari ni ushahidi kama kuna Mungu. sasa kama wewe hupo au hakuna kiumbe chochote, tena angejadiliwa vipi? ungekuwa wewe hupo na mimi sipo tena vipi mimi na wewe tujue kama mungu yupo au hayupo ikiwa hatupo ulimwenguni?
Huo sio ushahidi

Huwezi kuchukua kitu ambacho kipo halafu ukatolea maelezo ambayo hayapo kama ushahidi?

Wazee vijijini waliuliwa kwa kudaiwa kua ni wachawi kwasababu macho yao ni mekundu, hapa utaona kua walichukua kitu ambacho kipo kutolea sababu isiyokuwepo kama ushahidi, ni kweli wale wazee wanamacho mekundu lakini kua na macho mekundu hakumaanishi ni mchawi
 
Back
Top Bottom