Kitu Cha kuchekesha zaidi kuhusu hii mijadala ni kwamba watu wa dini zote tena zinazokinzana huungana na kumshambulia Atheist kwa Hoja zilezile za kizamani zisizokua na Mashiko yoyote Wala facts
Wanasahau kuwa hata wao wenyewe wanapingana
Assume Sasa Atheist kaamua kukubali Sasa kuwa Mungu yupo na anataka awe muumini mzuri wa huyo Mungu ili aurithi huo uzima wa Milele
Bro guess what?...."World war 3" itatokea
Kutazuka mjadala mwingine mkali kuwa yupi yupo sahihi Kati yao
Mwengine watamwambia akabidhi Maisha yake kwa Yesu,mwana pekee wa Mungu
Hapa wenzake watambishia,"Sio Yesu,ni Issa bin Mariam na Ni nabii tu,Njoo kwenye Uisalam dini ya haki"
Akikubali kuwa Ukristo ndio dini ya haki hivyo atampa Yesu Maisha yake....hapa pia watagawanyika Kuna watakao taka awe Roman Catholic,wasabato watakuja jua pia na kuanza kupingana na Roma
Nyie ni waabudu shetani....mnaabudu sanamu hamfai
Wakati hao wanaendelea kubishana Jehovah witnesses watamshika mkono na kumpeleka pembeni
Bwana Eeh,fata njia yetu ila yesu Sio Mungu,ni malaika Aliyeumbwa na Mungu
Hapa waislam watadakia,"Sasa we kafiri ulikataa nini, si tulikwambia yesu sio Mungu,Njoo kwetu
Hapa Sasa itazuka Vita nyingine Kati ya Shia na suni
Kwanini Kuna Mkanganyiko mkubwa ivyo
Soma Hoja inaitwa "Argument from inconsistent beliefs"
Na nyingine "Argument from Locality"
Utagundua kwanini Wasomi na wenye hekima wengi ni Atheist
NB:Mwenye Uzi Eeh?...unaweza ibandika hii comment hapo Juu...ili watu pia waone maoni ya Atheist Juu ya swali lako
Atheist hajui anachotafuta, kwasababu Hakuna Cha kutafuta
Asante
Edition:Iblis Bin Shetan amekuwa wa Kwanza ku like hii comment



Mpaka shetani kapenda
No sorry...Hakuna shetani
Kwa waumini wenye mioyo migumu tu,na wanaopenda kuchallenge imani Yao
SOMA HIOOO
"Argument From Inconsistent Revelation/Avoid the wrong Hell problem"
Source: Wikipedia
Tahadhari:Atheists hatutahusika na upotevu wowote wa Imani yako
READ AT YOUR OWN RISK