Atheist wengi hawajui wanachokitafuta

So kuna allah

So Mungu wetu sisi wakristo si wa kweli

Mambo kama haya ndo hufanya wakina kiranga kutuona sisi waamini Mungu watu tusiojitambua

Tukianza kutetea uwepo wa Mungu tunaungana

Ila sasa baada ya hapo utasikia mkristo ni kafiri

What the fvck !
Mungu wa kweli ni mwenye sifa za kiungu. Wewe tetea hoja zako kwa kupitia Mungu unaemuamini, utakaposhindwa itabidi ujiulize.

Kwani umesikia wanasayansi wameungana wote? wapo wana sayansi ambao wanaamini kuwa LAZIMA kuwe na grand designer na ndio ukweli ulivo. Sasa tutatofautiana kwenye kumjua huyo grand designer. Kutofautiana kitu haimanishi kuwa hakipo.

Huyo Kiranga unamuuliza maswali anakimbia kuyajibu, nakushangaeni sana, mambo madogo tu mnashindwa, na akija na mfano wa pembe tatu mnaona kama kaja na hoja kubwa kumbe uchwara tu. Tatizo hamumjui Mungu.

Sasa ishu ni simple tu, anapokuja Atheist kujadiliana na muislam basi amzungumzie Mungu wa waislam. na anapokuja kujadiliana na mkiristo aulize mungu wa kikiristo. Sio ajenge hoja kupitia Yesu aitumie kwa muislam.
 
Hapa wakristo na waislamu tutaungana subiri baadae

Aisee ... Hizi issue ni complicated sana ukubali au ukatae

Nashangaa sana ani .. Tunatumia Nguvu nyingi kumtetea mtu ambaye hajaokba tumtetee

Hivi ni wapi aliwahi tuombe tumthibitishe kama yupo
Hapo ulipoquote, bila shaka umepata jibu lako kuwa Mungu hajajificha bali hatuna uwezo wa kumuona tu. Waislam hatumtetei Mungu, hatujawahi kumtetea Mungu, sisi tunatetea tunachamini tu. Mungu hana shida na sisi ila sisi tunashida na yeye
 
Kama anajua kuwa naenda motoni basi ameshajua kuwa nitaacha ibada
Sijasema ugeuza swali kisha ulitolee majibu

Sijauliza kama mungu alijua kua utaacha ibada, Nimekuuliza mungu akijua kua wewe ni wa motoni je kuenda kwako kanisani kufanya ibada kutakufanya uende peponi??
 
Binadamu ana intelligence ambayo kazi yake kuu ni kujiuliza maswali na kuyatafutia solution
kama ikiwa aidha hujiulizi hayo maswali au ukijiuliza ukiona hupati majibu una turn hicho kitu kuwa imani na kubakia na conclusion fulani zisizo na ushahidi wowote unakuwa huna tofauti na wanyama wengine wanaoishi tu kwa senses bila ya kureason
Imani ina sababu na dalili hivyo imani si hisia.
 
Inaonekana huelewi,vipi yawe mapya wakati yeye ndio ameamrisha...?
Kwaiyo ni mambo ambayo hayakwepeki hata ufanye jitihada gani kwasababu tayari umeshapangiwa iwe hivyo au una option ya kwenda kinyume?
 
Sasa kama anajua wewe utaishia wapi inamaana alishapanga tangu anakuumba kwamba utaingia motoni na kama kweli yeye ni mwenye huruma kwa nini asingekuokoa tangu mwanzoni kwa maana mwisho wako anaujua?
Kujua sio kupanga. Mfano, unaweza kumuona mtoto ukasema "huyo atazima tv saivi" Akiizima TV manake wewe umepanga?
 
Hukielewi unachokitetea.

Kujua au kutokujua kitu hakiondoa uhalisia wa jambo.

Mfano mtu anayehangaika kusukuma ukuta akitegemea kuuangusha huyu mtu tunasema anajichosha tu maana hatofanikiwa katika kusudio lake.

Au tuchukulie mfano mwingine, dini za watu wanaoabudu masanamu,miti, wanyama nk ,watu hawa nao wana imani ipo siku nao wataingia peponi jambo ambalo Mungu anajua fika kuwa hawa mwisho wao utakuwa motoni maana wameshindwa kumuabudu yeye na wanaabudu vitu vingine wakidhani wanamuabudu Mungu halisi.
Kipi nnachoteteta na wapi pamekufanya kuona kuwa sijui nnachotetea?
 
Sijasema ugeuza swali kisha ulitolee majibu

Sijauliza kama mungu alijua kua utaacha ibada, Nimekuuliza mungu akijua kua wewe ni wa motoni je kuenda kwako kanisani kufanya ibada kutakufanya uende peponi??
Nimekujibu, sema hivi "SITAKI JIBU ULONIPA KWA SABABU SIVYO NNAVOTAKA LIWE"

Mungu kama anajua mimi naenda motoni, ibada nnazofanya hazitasaidia kitu kwa sababu ameshajua kuwa nitakuja kufanya maovu ambayo hizo ibada hazitosaidia kitu.
 
Kujua sio kupanga. Mfano, unaweza kumuona mtoto ukasema "huyo atazima tv saivi" Akiizima TV manake wewe umepanga?
Ujuzi wako unaufananisha na ujuzi wa mungu ambaye hakosei na ndiye mpangaji wa maisha ya binadamu ambaye hakuna kitu kitachotokea bila kuruhusiwa na mungu kwasababu yeye ndiye muamuzi wa mwisho???

Ngoja nitumie mfano huo huo wa mtoto na baba kama ulivyofanya

Unaweza kumuadhibu mtoto kwa kosa ambalo ulijua kua atalifanya na ukaset mazingira ya kumfanya afanye hilo kosa kwa makusudi ili akifanya tu umuadhibu???
 
Kwaiyo ni mambo ambayo hayakwepeki hata ufanye jitihada gani kwasababu tayari umeshapangiwa iwe hivyo au una option ya kwenda kinyume?
Hujapangiwa wewe uwe muovu bali Mola wetu anajua kila kitu.

Yaani kujua kwake ni katika Elimu yake,na kujua kwake hakukuzuii wewe kutenda unachotaka yaani ametupa uhuru na uwezo wa kufanya tunayotaka.
 
Ujuzi wako unaufananisha na ujuzi wa mungu ambaye hakosei na ndiye mpangaji wa maisha ya binadamu ambaye hakuna kitu kitachotokea bila kuruhusiwa na mungu kwasababu yeye ndiye muamuzi wa mwisho???

Ngoja nitumie mfano huo huo wa mtoto na baba kama ulivyofanya

Unaweza kumuadhibu mtoto kwa kosa ambalo ulijua kua atalifanya na ukaset mazingira ya kumfanya afanye hilo kosa kwa makusudi ili akifanya tu umuadhibu???
Nijibu swali langu uliloquote tafadhali, then nikujibu lako.
 
Nimekujibu, sema hivi "SITAKI JIBU ULONIPA KWA SABABU SIVYO NNAVOTAKA LIWE"

Mungu kama anajua mimi naenda motoni, ibada nnazofanya hazitasaidia kitu kwa sababu ameshajua kuwa nitakuja kufanya maovu ambayo hizo ibada hazitosaidia kitu.

At least saizi umejaribu kujibu

Kwaiyo leo ukiamua kuenda au kutoenda kanisani au msikitini hujabadili chochote alichokiona mungu kwasababu hakuna kipya kitachofanyika ambacho yeye hakukijua kabla kwasababu hauna uhuru wa kubadili chochote kiwe unavyotaka mpaka upangiwe na mungu siyo??
 
Nijibu swali langu uliloquote tafadhali, then nikujibu lako.
Mwanzo ulianza kulalama kua atheist wanakimbia maswali, nilipokuuliza swali ukakimbia kulijibu kwa kusema unajibu kwa mtindo wa kuuliza swali

Sasa namimi nikikwambia nimekujibu kwa mtindo wa swali utakubali?
 
Back
Top Bottom