Athari za kusamehe kodi kwenye ushindani wa kibiashara

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
13,663
18,037
Ifahamike kuwa wakati baadhi ya wafanyabiashara hawakuweza kulipa kodi, kuna wenzao waliweza kulipa kodi kwa aina hiyo hiyo ya biashara na soko hilo hilo.

Mfanyabiashara anapopanga bei ya bidhaa zake anatilia maanani gharama aliyotumia ikiwemo ulipaji wa kodi.

Sasa kama mfanyabiashara mmoja ukimsamehe kodi utakuwa umempa faida kwenye ushindani wa kibiashara dhidi ya yule mwaminifu aliyelipa kodi.

Matokeo yake huyu mwaminifu wa kodi bidhaa zake hazitanunukiwa maana bei yake itakuwa ni kubwa ukilinganisha na huyu ambaye amesamehewa kodi.

Huyu mlipa kodi utakuwa umemwandalia mazingira ya kushindwa kulipa kodi na tunarudi huko huko tunakotaka kuondoka!!

Kodi lazima ILIPWE cha msingi ni kuwaandalia utaratibu rafiki wa kulipa kodi hiyo aidha kwa kuwaongezea muda wa kulipa kodi hiyo.

Wasaidizi wa RAIS wanayajua yote haya lakini kwa sababu zao wenyewe wanamwacha mama afanye mambo yanayodhalilisha taasisi ya URAIS. Rais asivuke mamlaka yake ya kikatiba!
 
Hili ni TATIZO SUGU la wasaidizi wake. TRA inatimiza majukumu yake kwa mujibu wa sheria. Rais hana mamlaka ya kikatiba ya kusamehe mtu kulipa kodi!!

Akitaka kumsamehe inabidi huyo mtu ashitakiwe kwanza na kufungwa kisha yeye ndiye ampatie msamaha wa rais.

Vinginevyo irekebishwe katiba na kuongeza kipengere cha mamlaka ya Rais kuwa anaweza kumsamehe mfanya biashara kulipa kodi!!

Tatizo ni kwamba kama mfanya biashara mmoja umemsamehe kodi utakuwa umeharibu usawa kwenye soko.

Aliyesamehewa kodi atawapiku wenzake sokoni maana atashusha bei na wenzake hawawezi kushusha bei na hii si sawa.

Wasaidizi wake inabidi wamwambie ukweli!!
 
Katiba yetu haimpi mamlaka RAIS ya kusamehe mtu KABLA ya mtu huyo kuhukumiwa na mahakama. Soma mwenyewe mipaka ya mamlaka ya rais ya kutoa msamaha:

Uwezo wa kutoa msamaha Sheria ya 1984 Na.15 ib.9 45.-(1)
Bila ya kuathiri masharti mengineyo yaliyomo katika ibara hii, Rais anaweza kutenda lolote kati ya mambo yafuatayo:- (a) kutoa msamaha kwa mtu yeyote aliyepatikana na hatia mbele ya mahakama kwa kosa lolote, na aweza kutoa msamaha huo ama bila ya masharti au kwa masharti, kwa mujibu wa sheria; (b) kumwachilia kabisa au kwa muda maalum mtu yeyote aliyehukumuwa kuadhibiwa kwa ajili ya kosa lolote ili mtu huyo asitimize kabisa adhabu hiyo au asitimize adhabu hiyo wakati wa muda huo maalum; (c) kuibadilisha adhabu yoyote aliyopewa mtu yeyote kwa kosa lolote iwe adhabu tahafifu; (d) kufuta adhabu yote au sehemu ya adhabu yoyote Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyopewa mtu yeyote kwa ajili ya kosa lolote au kufuta adhabu yote au sehemu ya adhabu ya kutoza, au kuhozi (au kuchukua) kitu cha mtu mwenye hatia ambacho vinginevyo kingechukuliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano. (2) Bunge laweza kutunga sheria kwa ajili ya kuweka utaratibu utakaofuatwa na Rais katika utekelezaji wa madaraka yake kwa mujibu wa ibara hii. (3) Masharti ya ibara hii yatatumika kwa watu waliohukumiwa na kuadhibiwa Tanzania Zanzibar na kwa adhabu zilizotolewa Tanzania Zanzibar kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge inayotumika Tanzania Zanzibar, hali kadhalika, masharti hayo yatatumika kwa watu waliohukumiwa na kuadhibiwa Tanzania Bara kwa mujibu wa sheria.

Hawa wasaidizi wa Rais wanataka kumwingiza Rais katika kosa baya sana la KUVUNJA KATIBA aliyoapa KUILINDA.
 
Back
Top Bottom