ATCL anzisheni route ya Dar - Accra - Mumbai

eddy

JF-Expert Member
Dec 26, 2007
15,080
10,032
Jana Rais wa Ghana ametangaza kuruhusu safari za ndege za kimataifa na kuruhusu kufunguliwa kwa uwanja wa ndege wa Accra, na wiki ijayo China nao watafungua anga lao.

Kuna wanafunzi wengi wa Africa waliokuwa wanasoma China wanajiandaa kurudi shule, wafanyabiashara wengi mzigo hawana wanajiandaa kufuata mzigo. ATCL nao mna ndege mpya mgependa sasa kujitanua zaidi kwenye hili soko la usafirishaji wa anga. Napendekeza yafuatayo:

1. ATCL anzisheni usafiri wa Dar-Accra-Beijing Guangzhou, tuache kugombania abiria tuangalie namna gani tutashirikiana na Rwanda air, kenya airways na Ethiopia airlines. Hii route ya Accra - Guangzhou ni muhimu sana kulikamata soko la West Africa. Pia nchini Ghana tunaweza peleka bombardier mbili zikafanyakazi ya Accra Kumasi, Kumasi ni mji wakibiashara kama ilivyo Mwanza na abiria ni wengi kwa sasa hii route inashikiliwa na Flight540 ya Kenya.

2. Tufikirie pia kuanzisha route ya Accra - Dar Mumbai hii ni route muhimu kibiashara na wenzetu waghana wanasafiri nje zaidi kuliko sisi na fedha yao ina thamani huyu anaweza kuwa mshirika mzuri wa kibiashara. Seat zitakazo baki wazi baada ya abiria wa China ghana kushuka basi abiria wa Accra - Mumbai watajaza nafasi na tutakuwa na full board.
 
Hizo hela za kununulia midege ni bora wangezitumia kutrade forex na the like
 
Ni kweli maana waghana hawana ndege🤔🤔🤔 dona kantri kunavituko😂😂😂
 
Tatizo wanaongoza hilo shirika wapo kwa sababu tu wameteuliwa ila ukweli wengi hawajui nini kinahitajika kwenye biashara ya ndege
 
Sidhani kama inawezekana, nchi nyingi haziruhusu kutoa vibali vya ndege ambavyo ndege itaanzia safari kwenye nchi yako kwenda nchi tofauti na ile ndege inapotoka inaweza kupitia lakini haiwezi kupakilia abiria hapo...mpaka kuwe na makabuliano maalum...ndio maana lazima uende kwanza kwenye hub ya nchi husika kubadilisha mfano huwezi kwenda J'burg na KQ kutokea Dar lazima ukaanzie Nairobi....

Pia Accra - Dar hamna hiyo trafic kubwa hivyo....KQ wanaenda kutoka Nairobi lakini wanakusanya abiria kutoka kila mahali kwa route za nchi jiarni kama Uganda, Tz, Malawi, Zambia n.k
 
Back
Top Bottom