Si mchezo, unajua wakati ATC ilipogawanywa na kuuzwa (au ilikuwa kuazimwa) kwa makaburu kama ATCL, tulidhani ndio tumepata manake mambo yalikuwa ni bam bam... Cha ajabu ni kwamba tulipoingia ubia na SAA toute zote za ATC zilizokuwa na faida (so they said, including Lubumbashi, Dubai, ETB, NRB, Comorro na nyinginezo zikiwemo za ndani) ndio zilipokuwafa.... Soute iliyokuwa inasifika ilikuwa ni ile ya Dar-JHB-Dar... ambapo ukiangalia ni ruti yenye mpinzani mkubwa sana, SAA - ambaye kumbe ndio mbia mkuu..... Wajemeni, hapo ndipo tulipoanza kushituka lakini tukaambiwa kuna faida, cha ajabu ni kwamba miwshoni (is it 5 years) ndio tunaambiwa kumbe mambo yalikuwa rongorongo na ni hasara tupu!!!
Ukirudi kwenye point ni kama "Chiluba" aliposema hapo juu, kama tumeamua kulifufua shirika na kuliokoa kutoka kwa "mafisadi wa kusini" mbona ni kiraka kimoja tuu (Matakka) kilichowekwa na mengine yote yakawa ni yaleyale ya makaburu?? Nilipata wasaa wa kusafiri na ATC kwenda JHB wakati flani hapao nyuma (second half ya 2007) na niliyoyaona humo ndani niliapa sitasafiri tena na ATCL sababu kwa kweli hata kama ni uzalendo pale nilishindwa (vyoo vichafu, chakula bomu, wahudumu wenye nyodo.... hata duty free ya vipafyumu haikuwepo) na hata kurudi nilibidi nikaombe SAA (code share).......
Hivyo, jamani wanaJambo wenzangu "ATCL" imepewa na inaendelea kupea udhamini wa serikali ili ifufuke lakini kwa mtaji huu mimi nasema hakuna kufufuka bali ni kuichimbia kaburi kabisaaaaa....... Hivyo tuendelee kuweka hili na uhakika ni kwamba tukilipigia kelele humu kwenye JamboF nina uhakika Muungwana atadondoshewa nyeti na atafanya kama lilivyokuwa lile la BoT............