Atayaweza majukumu huyu kweli?

Atayaweza majukumu huyu kweli?

Khantwe umeamua kuja kunisemea huku si ungeniambia tu kama haupendezwi na hiyo tabia.

Mbona huwa unachukia nisipokuja kula kwako...

Mbona nikikuambia niko bar na marafiki nakula nyama unanuna.

Mbona kodi ya nyumba nilikulipia mwaka mzima sikuona shida yoyote.

Ile tv na subwoofer nani alikununulia kama sio mimi.

Alie kutafutia hiyo kazi na akatoa pesa ya kuhonga ukaipata sio mimi mbona sikudai hiyo pesa.

Ukiugua huwa unamdekea nani kama sio mimi na huwa nagharamia matibabu yote, je nikudai?

Mbona nilikuambia nina mpango wa kuwa na kula hotelini ukasema nadharau chakula chako.

Chakula unakuja kunisemea huku, wakati nikila usiku asubuhi nakwenda kujisaidia msalani.

Sasa nikikuoa utavumilia kuishi na ndugu ambao wataishi kwetu wakiwa hawana kazi si utasema wanajaza choo.

Kweli Khantwe nilie kuita mke mwema leo unauvua utu wangu sababu ya chakula.

Ina maana kutochangia kununua chakula kwako kumefuta mema yangu yote.

Upendo wako uko wapi au nikwenye kuchangia chakula tu?[/B]
 
mwambie ukwel asipo badilika temana naye mkishaoana atakuachia majukumu yote sembuse ukienda restaurant unalipia huyu mwanaume tabia yake mbovu mpe makavu yake
Hahaaaa huyo bidada asipoangalia wakianza kuishi pamoja jamaa luku ikiisha atajikausha kimyaaa tena atachelewa kurudi siku hiyo, shopping ya vitu vya home atausugua huku anategemea kula wali kuku, maji, gesi, house girl mwanaume kavuuuu atajikausha. Akirudi ni kuoga maji ya moto uliomtengea, ale wali kuku, ashushie na juice huku anaangalia tv ya king'amuzi ulicholipia! Mahaba niue... hapo ni mpenzi wangu nakupenda, baby I loveeee youuuu nyiiingi... hata mie ingekuwa yeye ningeku lavu shostito, loh! Mwambie sina hela ya matumizi ya hapa home haniii niachie maisha gharama usiponipa wewe nani atanipa?! Tena muangalie usoni mkavuu...!
 
Heheheheh kimbiaaaaaaaaaaaa shaurilo

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Nlishawahi kumuambia naomba hela nikanunue gas nikaambiwa 'mwisho wa mwezi' heee! Kwa hyo nisipike mpaka mwisho wa mwezi? Nikanunua gas na siku alivyokuja hata hakuuliza nimeipataje na mwisho wa mwez ulifika akapiga kimya mpaka leo hii nnapoandika

Huyo mwanaume kakugeuza weww hoyeli

Hakufai

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Yaani unampa chakula ale ashibe na "chakula" ale ashibe!!!! Aiseeee sikubali

Hahahahaaaa....vyote anakula anashiba, chakula ya kwanza na chakula ya pili halafu anasepa
 
kabla ya kuleta malalamiko yako hapa jukwaani umeishawahi kuongea nae kuhusu hii kitu au umekurupuka tu?kama unajitosheleza pengine mwenzio anaona hana haja ya kubebana na misosi.wakati mwingine inabidi ufikirie mambo kwa mapana yake,unaweza kushangaa akaja kuwa msaada mkubwa sana kwako katika mambo makubwa na ya muhimu kabisa kuliko hata huo msosi unaouligia kelele.unadhani asipokula kwako hana sehemu nyingine ya kula?au elf 3 ya ugali samaki inamkosa hadi adoee kwako?THINK BIG SISTER.LIFE IS MORE THAN JUST FOOD

Yeah mkuu! Kitu kingine ambacho nahisi kinakosekana ni mawasiliano mazuri kati yao na uhuru pia sio wakutosha, ni kama wanaviziana.
 
Huyu ndo mwanaume anayejua anachokifanya; mmezoea kutuchuna mkichunwa nyie tabu
Mchunwe na nani hii karne nyingine. Unakuja kula kila siku mtu hakuombi chochote afu siku akisema gas imeisha unamwambia mwisho wa mwezi. Kuchunwa utachunwa mtungi wa gas bwanaa? Mwanaume wa hivi kwanza anaonekana mchoyo na mbinafsi. Samahani muomba ushauri ni mtazamo wangu najua unampenda Omera.
 
Mh kunamchujo umepita nini humu MMU.. yaani asilimia sabini wametoa ushauri toka mioyoni... wale aamatusi sija mwona hat mmoja. Tuendelee hivi kama zamani.
Bidada umepata ushauri wa kutosha chambua fanyia kazi.
 
Khantwe umeamua kuja kunisemea huku si ungeniambia tu kama haupendezwi na hiyo tabia.

Mbona huwa unachukia nisipokuja kula kwako...

Mbona nikikuambia niko bar na marafiki nakula nyama unanuna.

Mbona kodi ya nyumba nilikulipia mwaka mzima sikuona shida yoyote.

Ile tv na subwoofer nani alikununulia kama sio mimi.

Alie kutafutia hiyo kazi na akatoa pesa ya kuhonga ukaipata sio mimi mbona sikudai hiyo pesa.

Ukiugua huwa unamdekea nani kama sio mimi na huwa nagharamia matibabu yote, je nikudai?

Mbona nilikuambia nina mpango wa kuwa na kula hotelini ukasema nadharau chakula chako.

Chakula unakuja kunisemea huku, wakati nikila usiku asubuhi nakwenda kujisaidia msalani.

Sasa nikikuoa utavumilia kuishi na ndugu ambao wataishi kwetu wakiwa hawana kazi si utasema wanajaza choo.

Kweli Khantwe nilie kuita mke mwema leo unauvua utu wangu sababu ya chakula.

Ina maana kutochangia kununua chakula kwako kumefuta mema yangu yote.

Upendo wako uko wapi au nikwenye kuchangia chakula tu?[/B]

Duuuh kwa bahati mbaya au nzuri kati ya hayo ulitotaja hakuna hata moja alilolifanya
 
Back
Top Bottom