Atayaweza majukumu huyu kweli?

Atayaweza majukumu huyu kweli?

Khantwe

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2012
Posts
61,112
Reaction score
124,671
Habari zenu wanaMMU. Nina mpenzi wangu ambae nnategemea kuwa atakuwa baba watoto ila ana tatizo (mimi naliita tatizo). Ni kwamba yeye ni mfanyakazi wa kampuni moja binafsi,ni kawaida yake huwa anakuja kwangu mara nyingi nampikia chakula.

Anaweza akatoka kazini anapitia kwangu anakula then anaenda kwake.

Hakuna siku utamsikia anasema dia hela hii hapa kanunue mchele au hata yeye mwenyewe kwamba anapokuja abebe walau maji ya uhai, hana muda huo kabisa. Gharama zote nazijua mimi. Tena anaweza kudiriki hata kusema chakula nlichopika ye hakipendi.

Sasa nauliza eti huyu mtu majukumu anayajua? Hata tukiingia ndoani si atanitwisha majukumu yote huyu? Au labda nyie wenzangu mnaonaje tabia hii, ni ya kawaida?
 
^^
Uchumba ni kipindi cha kupendana kwa nia ya kufikia ndoa. Ni wakati wa kujiridhisha kama uliyenae atakufaa baadae, ukiona hafai off you go!
Kwa mfano, unapojiuliza wakati huu kama mwenzako atamudu, hata wewe jiulize utaweza kufanya haya unayofanya?
Tujipime Tuwapimapo na wengine. Vingnevyo tatizo lako linazungumzika. Kaeni mlijadili
^^
 
Habari zenu wanaMMU. Nina mpenzi wangu ambae nnategemea kuwa atakuwa baba watoto ila ana tatizo (mimi naliita tatizo). Ni kwamba yeye ni mfanyakazi wa kampuni moja binafsi,ni kawaida yake huwa anakuja kwangu mara nyingi nampikia chakula. Anaweza akatoka kazini anapitia kwangu anakula then anaenda kwake. Hakuna siku utamsikia anasema dia hela hii hapa kanunue mchele au hata yy mwenyewe kwamba anapokuja abebe walau maji ya uhai, hana muda huo kabisa. Gharama zote nazijua mimi. Tena anaweza kudiriki hata kusema chakula nlichopika ye hakipendi. Sasa nauliza eti huyu mtu majukumu anayajua? Hata tukiingia ndoani c atanitwisha majukumu yote huyu? Au labda nyie wenzangu mnaonaje tabia hii, ni ya kawaida?

aanze kukuhonga hata hajatoa mahali hata mimi siwezi ukiniacha
 
^^
Uchumba ni kipindi cha kupendana kwa nia ya kufikia ndoa. Ni wakati wa kujiridhisha kama uliyenae atakufaa baadae, ukiona hafai off you go!
Kwa mfano, unapojiuliza wakati huu kama mwenzako atamudu, hata wewe jiulize utaweza kufanya haya unayofanya?
Tujipime Tuwapimapo na wengine. Vingnevyo tatizo lako linazungumzika. Kaeni mlijadili
^^

Asante kwa ushauri ila mm huwa naogopa kuanza kulizungumzia maana ataona km namnyanyasa vile
 
Si watu wote ni wakujituma na kujitolea…wewe siku mpigie sim mwambie dia pitia dukani/sokoni uninunulie bidhaa hizi…Kama ni mtu wa kuelewa ataelewa kuwa chakula hakishushwi kutoka mbiguni na atakumbuka kama kuna kitu alikuwa anakosea….
 
''wasema chai ina chumvi, chakula hiki kina sisimizi..!

you know i'm crazy over you, crazy, crazy, crazy over you, lakini sasa nachoka, oh no!- usipoacha vituko, kwani mimi nitaondoka!''

talk back to your man, msome kama miezi sita hivi, asipojirudi then chukua hatua!
 
Asante kwa ushauri. Nilishawahi kujaribu hii ila anafanya siku hiyohiyo uliyomwambia baada ya hapo km kawaida
 
Hahaaaa thanx kwa ushauri ila
 
Asante kwa ushauri. Nilishawahi kujaribu hii ila anafanya siku hiyohiyo uliyomwambia baada ya hapo km kawaida

Mmh hapa kunakitu kilichojificha mbona hali hii siyo ya kawaida.Jaribu kutafuta namna nzuri ya kumwambia ukweli wote uone atasemaje .Hapa ni kumwambia ukweli tu kwa busara zaidi .Ukiona anauchukia ukweli unaomwambia mkifunga ndoa sijui kama itadumu kweli.Mwambie ukweli lakini tumia busara sana.
 
Back
Top Bottom